Shahawa ni kioevu cha mwili kilichoumbwa ili kubeba spermatozoo ndani yake.
Mchanganyiko wa kioevu hicho na spermatozoo huitwa shahawa pia. Kinatolewa na tezi za shahawa na kwa kadiri ndogo zaidi na kibofushahawa ambazo zote mbili zimo katikati ya fupanyonga. Mchakato unaosababisha kutoka kwa shahawa kwenye kipenyo cha mrija wa mkojo unaitwa kumwaga. Kwa wanadamu kioevu cha shahawa kina vijenzi kadhaa badala ya spermatozoo: vimeng'enya, vinavyomeng'enya protini na molekuli nyingine, pamoja na fruktosi ni sehemu za kioevu vya shahawa ambazo zinasaidia spermatozoo kudumu na kuzipatia chombo ambamo zinaweza kusogea au "kuogelea". Kioevu hicho kimegeuka ili kutolewa ndani kabisa ya kuma, kwa hivyo spermatozoo zinaweza kupita kwenye uterasi na virijaova ili mojawapo iunde zigoti pamoja na yai.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Shahawa, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.