Mzeituni au mzaituni (jina la kisayansi kwa Kilatini Olea europaea, yaani mzeituni wa Ulaya, au Olea sylvestris, yaani mzeituni mwitu) ni mti mfupi wa familia ya Oleaceae unaopatikana hasa kandokando ya Bahari ya Kati, lakini pia sehemu nyingine za Afrika na Asia.
Mzeituni (Olea europaea) | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mzeituni | ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Matunda yake (zeituni au zaituni) ni muhimu hasa kwa utengenezaji wa mafuta (90%), ingawa yanaliwa pia bila kushindiliwa (10%).
Inaonekana asili ya ulimaji wake ni Uajemi na Mesopotamia miaka 6,000-7,000 iliyopita. Kutoka huko ulienezwa sehemu nyingine.
Leo uzalishaji ni mkubwa hasa Hispania, halafu Italia, Ugiriki, Uturuki n.k.
Mbali ya faida hiyo, toka zamani tawi la mti huo linatazamwa kama ishara ya wingi, utukufu na amani. Kwa sababu hiyo lilitolewa kwa miungu na kwa washindi.
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mzeituni kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Mzeituni, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.