Muhimbili

Muhimbili ni mahali maarufu jijini Dar es Salaam na nchini Tanzania kwa jumla, hasa kutokana na hospitali na chuo kikuu vinavyopatikana huko.

Ipo barabara ya Umoja wa Mataifa mtaa wa Upanga Magharibi.

Muhimbili
Muonekano wa Chuo kikuu Muhimbili

Historia

Chanzo cha Muhimbili ni Hospitali ya Sewa Haji iliyoanzishwa mwaka 1897 na mfanyabiashara Sewa Haji Paroo kutoka Bagamoyo aliyegharimia ujenzi na kuiachia mali ya kutosha kuiendesha katika wosia wake. Iliendeshwa na serikali ya kikoloni ya Kijerumani kutokana na mali hiyo.

Mwaka 1919 ilikabidhiwa mikononi mwa serikali ya kikoloni ya Waingereza walioendelea kuiendesha kama hospitali kwa Waafrika. Mwaka 1956 majengo yaliongezeka yaliyofunguliwa rasmi kama "Dar Es Salaam General Hospital" na Margaret binti wa mfalme wa Uingereza na muda mfupi baadaye ilipokea jina la "Princess Margaret Hospital".

Baada ya uhuru ilipata jina la "Muhimbili", ambalo limetokana na neno la Kizaramo "mibili" likimaanisha kiungo cha mtoto tumboni na mama yake (plasenta) Hospitali ilipoanza Wazaramo walisema "Hapo ndipo wanawake wanapokwenda kuacha mibili yao". Neno Muhimbili likazaliwa hivyo, nalo ladumu hadi leo.

Chuo kikuu cha Muhimbili kilianzishwa mwaka 1963: kilifunguliwa kama "Chuo cha Afya Dar es Salaam" ndani ya hospitali iliyoitwa awali Princess Margaret Hospital na wanafunzi 10 waliofuata kozi za uganga au upasuaji.

Mwaka 1968 kikafanywa ni kitengo cha tiba katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Tangu 2007 imeandikishwa kama Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (kwa Kiingereza: Muhimbili University of Health and Allied Sciences; kifupi: MUHAS).

Leo hii Muhimbili ina shule ya madaktari, wauguzi, mafamasia, waganga wa meno, maafisa afya mazingira, maafisa mazingira na elimu ya juu ya afya.

Marejeo

Viungo vya nje

Tags:

BarabaraChuo kikuuDar es SalaamHospitaliJijiMtaaTanzaniaUpanga Magharibi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Abedi Amani KarumeMamba (mnyama)Injili ya YohaneKiarabuMohammed Gulam DewjiTiktokOrodha ya Marais wa UgandaSiasaMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaUyahudiBukayo SakaUongoziKorea KaskaziniLuis MiquissoneMawasilianoMadinaNomino za kawaidaIdi AminSkautiKontuaVita Kuu ya Kwanza ya DuniaHistoria ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoFamiliaHaitiShetaniKalenda ya KiislamuChombo cha usafiriMachweoMalariaUkoloniOrodha ya nchi za AfrikaWasukumaMkataba wa Helgoland-ZanzibarBaruaHistoria ya WasanguAfrika Mashariki 1800-1845HektariAsiliAdolf HitlerManchester CityMapinduzi ya ZanzibarBikira MariaMagonjwa ya machoDhamiriMarekaniMajiChama cha MapinduziJay MelodyWameru (Tanzania)Jumamosi kuuInshaNyweleWimboUzazi wa mpango kwa njia asiliaHistoria ya AfrikaMsamiatiPasifikiMafarisayoMkoa wa ShinyangaHekalu la YerusalemuKumaMsukuleChombo cha usafiri kwenye majiIsraelMvuaShirika la Utangazaji TanzaniaBustani ya EdeniSalaChadOrodha ya vyama vya kisiasa nchini KenyaNchiFid QKukuJohn MagufuliOrodha ya miji ya MarekaniMapambano ya uhuru Tanganyika🡆 More