Mfalme ni mtawala wa kiume juu ya nchi katika utaratibu wa ufalme.
Kwa kawaida amerithi cheo chake kutoka kwa mzazi wake aliyekuwa mfalme pia. Lakini kuna pia wafalme waliochaguliwa au kuteuliwa kwa namna nyingine, hasa kama mfalme aliyetangulia alikufa bila kuacha mrithi.
Utawala wa kifalme ulikuwa wa kawaida katika nchi nyingi za dunia kwa muda mrefu.
Mwanamke anayeshika nafasi ya mfalme huitwa "malkia".
Kama cheo kinaendelea katika ukoo mmoja kutoka mababa kwa watoto wao familia hiyo huitwa nasaba.
Madaraka ya wafalme yalitofautiana kati ya nchi na nchi na kati ya kipindi na kipindi cha historia. Mifano ni:
Katika Kiswahili hakuna utaratibu sanifu mtawala gani anastahili kuitwa "mfalme". Kwa kawaida anasimamia eneo au nchi ya kujitegemea lakini wengine huweka pia masharti kuhusu ukubwa wa eneo lake.
Kwa maeneo fulani kuna vipindi katika historia ambapo si rahisi kutofautisha kati ya wafalme na watawala wadogo wengine kama watemi, machifu n.k.. Mara nyingi watawala wa Waswahili ambao hawakuwa na mamlaka nje ya eneo dogo la mji wao walijiita Sultani na Wareno waliwaita "reyes" (wafalme). Hali hii ililingana na mifano mingine kama kati ya Wagiriki wa Kale ambapo vilevile watawala wadogo juu ya miji walitumia cheo cha "mfalme".
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Mfalme, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.