Wahaya: Watu wa Tanzania

Wahaya ni kabila la watu linalopatikana katika Mkoa wa Kagera, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, kandokando ya Ziwa Victoria hadi mpakani kwa Uganda.

Lugha yao ni Kihaya.

Wahaya: Watu wa Tanzania
Mushonge Museum, Kamachumu Plateau, Mkoa wa Kagera, TZ.

Kabila hilo ndilo linalojulikana kuliko yote ya mkoa wa Kagera, ila ndani yake kuna vijikabila vidogovidogo, kama vile Waziba wa Kiziba, Wahamba wa Muhutwe, Wayoza na Waendangabo wa Bugabo, Wanyaiyangilo wa Muleba, Wasubi wa Biharamulo, Walongo wa Geita. Wengine wanawahesabu mle pia Wanyambo wa Karagwe na Kyerwa.

Tofauti kati ya vijikabila zinatambulika kutokana na mabadiliko madogo madogo tu ya maneno na pia lafudhi ya Kihaya ya hiyo sehemu, chakula, ngoma za asili, majina ya asili.

Mfano: Viazi vitamu (Kiswahili) = ebitakuli (Kiziba) = enfuma (Kihamba, Kiyoza na Kinyaihangilo )

Wahaya ni maarufu kwa uzalishaji wa ndizi na kahawa. Ni kabila ambalo hupenda sifa, kujisifu na kusifiwa. Pia kabila hilo halitasahaulika kwa jinsi walivyopata shida mwaka 1978 kutokana na vita vya Kagera.

Elimu: kuingia kwa wamisionari katika karne ya 19 ambao walianzisha shule nyingi za awali na za kati ambapo ilibidi mtu abatizwe ili aweze kupata elimu. Wazazi wengi walipeleka watoto wao kubatizwa na hapo kukaanza mvutano, sababu wamisionari walikuwa Wakatoliki kutoka Ufaransa na Uswisi na Walutheri kutoka Ujerumani na Uholanzi. Ndipo kukaanza mashindano ya kuanzisha shule nyingi ili kupata waumini wengi.

Wamisionari pia wakawa mstari wa mbele kufungua hospitali nyingi kila wilaya na vyuo vya ufundi.

Ndiyo maana maeneo hayo ya Kagera elimu ni ya juu kwa wakazi wake na huduma za afya kuliko mikoa jirani. Na kilimo cha kahawa kiliwapa wenyeji fedha za kujenga nyumba bora na kupeleka watoto wao kwenye elimu ya juu zaidi. Pia kulianzishwa chama cha ushirika cha mkoa ambacho kilianzisha shule za watoto wa wakulima kuwasomesha na kutoa mikopo. Eneo hilo lilizidi kurutubishwa kushinda maeneo mengine mengi ya nchi kutoa Uchagga.

Pia wamisionari walianzisha shule za utawa, seminari na chuo cha kutoa mapadri wao wenyewe.

Wahaya: Watu wa Tanzania Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wahaya kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

KabilaKihayaLughaMkoa wa KageraTanzaniaUgandaWatuZiwa Victoria

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Mkoa wa ShinyangaKamusi ya Kiswahili sanifuHadhiraShengPemba (kisiwa)ShangaziMfumo wa JuaMichezoMange KimambiMakaburuKiingerezaYakobo IsraeliKwaresimaMkoa wa MorogoroMpira wa kikapuMofolojiaAmfibiaUsafi wa mazingiraMkoa wa MaraMobutu Sese SekoOrodha ya watu maarufu wa TanzaniaMaliasiliUkomeshaji wa Biashara ya WatumwaBiblia ya KikristoMkoa wa MbeyaKomaAlhamisi kuuWanyamaporiInjili ya LukaFutiHistoria ya KanisaUjasiriamaliNdimuKiboko (mnyama)Barack ObamaChuraTovutiOrodha ya Makamu wa Rais TanzaniaWachaggaVidonda vya tumboHektariNembo ya TanzaniaMaudhuiMkoa wa DodomaMaradhi ya zinaaHistoria ya TanzaniaCristiano RonaldoRisalaVita Kuu ya Pili ya DuniaBonde la Ufa la Afrika ya MasharikiHaitiFonimuYouTubeUongoziKifaduroKrismaAfrika KusiniKengeKifua kikuuTungo kishaziNabii IsayaMkunduUnyenyekevuAmri KumiMlongeDivaiUshogaSean CombsFaraja KottaOrodha ya wanamuziki wa hip hopMexikoHoma ya mafuaSadakaAfande SeleDjigui DiarraVielezi🡆 More