Qatar

Qatar (kwa Kiarabu: قطر ) ni emirati ndogo wa Uarabuni kwenye rasi ya Qatar ambayo ni sehemu ya rasi kubwa ya Uarabuni.

Qatar

Imepakana na Saudia upande wa kusini. Mipaka mingine ni ya Ghuba ya Uajemi. Kisiwa cha Bahrain kiko karibu.

Mji mkuu wa Qatar ni Doha.

Historia

Maeneo ya Qatar, pamoja na Falme za Kiarabu na Bahrain yalikuwa nyumbani kwa makabila madogo na chifu zao.

Tangu mwaka 1820 walikuwa na mikataba na Uingereza walipoahidi kuachana na uharamia na kupokea ulinzi wa Uingereza. Ulinzi huo ulizuia uvamizi wa Saudia katika karne ya 20.

Falme hizo zilikuwa nchi lindwa chini ya Uingereza hadi mwaka 1971, ambapo madola hayo madogo yalipata uhuru.

Siasa

Miaka ya mwisho Qatar imejihusisha na siasa ya Mashariki ya Kati kwa kuwapa silaha Waislamu wenye itikadi kali kama vile huko Palestina, Syria na Iraq, na hata DAISH.

Kwa sababu hiyo imetengwa na nchi jirani, hasa Saudia.

Watu

Wananchi wengi wa Qatar kwa asili ni Waarabu na Waafrika (utumwa nchini ulichelewa sana kufutwa). Lakini kati ya wakazi wote, wenyeji hao ni asilimia 12 tu (313,000), yaani idadi kubwa sana si Waqatari wenyewe bali ni wafanyakazi kutoka nchi mbalimbali, hasa India (zaidi ya 21%) na nchi za kandokando yake (Nepal 16.6%, Bangladesh 12.5%, Pakistan 4.5%, Sri Lanka 4.3%), halafu Ufilipino (10%), Misri (9%) n.k.

Kiarabu ni lugha rasmi ya nchi lakini Kiingereza hutumiwa mara nyingi kwa mawasiliano ya biashara na ofisini.

Waqatari wenyewe ni Waislamu (hasa Wasuni) lakini watu kutoka nje hufuata pia dini mbalimbali: hivyo kati ya wakazi wote 65.5% ni Waislamu, 15.1% ni Wahindu, 14.2% ni Wakristo, 3.3% ni Wabuddha n.k.

Uchumi

Uchumi wote wa Qatar una msingi wa mafuta ya petroli na gesi yake. Kwa wastani wakazi wake wana kipato kikubwa kuliko watu wa nchi zote duniani.

Tazama pia

Viungo vya nje

Qatar 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Qatar  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Qatar kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Qatar HistoriaQatar SiasaQatar WatuQatar UchumiQatar Tazama piaQatar Viungo vya njeQatarEmiratiKiarabuRasi ya UarabuniUarabuni

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Uwanja wa Taifa (Tanzania)Fasihi andishiChelsea F.C.Bendera ya TanzaniaApril JacksonMobutu Sese SekoMizunguNguzo tano za UislamuAsili ya KiswahiliAngahewaAbrahamuOrodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watuHifadhi ya mazingiraNileUchumiOrodha ya majimbo ya MarekaniTiktokOrodha ya watu maarufu wa TanzaniaAlama ya barabaraniOrodha ya Makamu wa Rais TanzaniaKalenda ya KiislamuLuhaga Joelson MpinaKhadija KopaUajemi ya KaleSelemani Said JafoKilimanjaro (volkeno)MunguRushwaBenjamin MkapaOrodha ya milima mirefu dunianiAdolf HitlerNdovuLigi ya Mabingwa UlayaPaul MakondaKiimboMkopo (fedha)FamiliaTashihisiKitunda (Ilala)Biashara ya masafa marefu ya Afrika MasharikiRoho MtakatifuUsafi wa mazingiraKito (madini)RaiaMishipa ya damuAdhuhuriTabianchi ya TanzaniaTwigaVisakaleMaradhi ya zinaaKassim MajaliwaWazaramoKadi za mialikoUchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2020Wabena (Tanzania)MajiHistoria ya KiswahiliSikioMariooMatumizi ya LughaMkoa wa TaboraMuunganoSteven KanumbaMuungano wa Tanganyika na ZanzibarMlima wa MezaTume ya Taifa ya UchaguziUfupishoKamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniZuhuraUongoziManchester United F.C.Viungo vinavyosafisha mwiliAgano la Kale🡆 More