Khadija Kopa: Mwanamziki kutoka Zanzibar, Tanzania

Khadija Omar Abdallah Kopa (alizaliwa Zanzibar, 1963) ni mwimbaji wa muziki wa Taarab na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Tanzania.

Mbali ya muziki, Kopa ni mama wa nyumbani, mfanyabiashara na pia mwanaharakati wa kisiasa nchini Tanzania.

Khadija Kopa
Jina la kuzaliwaKhadija Omar Abdallah Kopa
Amezaliwa1963
Kazi yakeMwimbaji, mtunzi wa nyimbo, Mtayarishaji wa rekodi, mwanamuziki
AlaSauti
Miaka ya kazi1990–hadi sasa
Ameshirikiana naDiamond Platnumz, Abdul Misambano, Ali Star, Mzee Yusuph, TOT

Anafahamika zaidi kwa ushirikiano wake mkubwa na bendi ya TOT. Ameanza kuimba Taarab tangu mwaka 1990 na bendi ya kwanza kujiunga nayo ilikuwa Culture Musical Club.

Mtoto wake wa kike Zuhura Othman Soud, afahamikaye kwa jina la kisanii kama Zuchu ni mwimbaji pia. Alijiunga na Wasafi Classics na kutoa nyimbo maarufu kama vile: Nisamehe, Sukari, Yalaa, Cheche, Wana.

Maisha na kazi

Khadija Kopa alizaliwa mwaka 1963 kisiwani Zanzibar na ni mtoto wa pekee katika familia ya Kopa. Ameolewa na ana watoto wanne na wajukuu wawili.

Khadija alikuwa akipenda kuimba tangu akiwa mdogo, akisomea madrasa Zanzibar. Akiwa chuoni (madrasa) alikuwa msomaji mzuri wa qaswida, halafu vilevile alipokuwa Young Pioneer, alikuwa kwenye kikundi cha kwaya.

Hali kadhalika shuleni alikuwa kwenye mambo ya ngoma, mambo ya utamaduni na kwaya. Shule yao ilikuwa bingwa kwa kwaya Zanzibar. Aliendelea hivyo hadi katika shule ya upili.

Kazi ya sanaa alianza mwaka 1990 katika Kikundi cha Culture Musical Club. Siku moja alikuwa amekaa huku akiiga wimbo. Akapita babu yake aliye katika kikundi cha Culture Musical Club cha Zanzibar. Akamsifia ya kwamba anajua kuimba. Basi akachukua hatua ya kuandika barua kwa niaba yake bila ya kumshauri, akaipeleka Culture Musical Club kuomba ajiunge nao.

Khadija pia amepata kushirikiana na waimbaji wengine wa kike kama vile Mwanamtama Amir, marehemu Leila Khatib na wanaume kama akina Abdul Misambano na Ali Star, waliporomosha nyimbo ambazo zilitamba miaka hiyo katika ulimwengu wa Taarab.

Tazama pia

Viungo vya Nje

Khadija Kopa: Mwanamziki kutoka Zanzibar, Tanzania  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Khadija Kopa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

1963MamaMfanyabiasharaMtunzi wa nyimboMuzikiMuziki wa TaarabMwanaharakatiMwimbajiTanzaniaZanzibar

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

PapaRwandaUandishi wa barua ya simuAfrika KusiniUajemiNathariOrodha ya vyama vya siasa TanzaniaKarneKhadija KopaBinadamuMmeng'enyoChristina ShushoFasihi simuliziOrodha ya milima ya AfrikaAfrika ya MasharikiMsumbijiAina za manenoMbuga za Taifa la TanzaniaHisiaElimuVivumishi vya jina kwa jinaOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaKichochoUmoja wa AfrikaNuktambiliMkutano wa Berlin wa 1885Tundu Antiphas Mughwai LissuVitenzi vishiriki vipungufuMajiJumuiya ya Afrika MasharikiMawasilianoUkoloni MamboleoAlomofuWimbiMfumo wa mzunguko wa damuJohn MagufuliUsultani wa ZanzibarVielezi vya idadiHistoria ya AfrikaUandishi wa ripotiKigugumiziViwakilishi vya kuulizaUpendoOsama bin LadenMichezo ya watotoUturukiMisemoLigi ya Mabingwa UlayaMiundombinuWaduduVitenzi vishirikishi vikamilifuMweziMatamshiZabibuUtohoziTanganyikaNdoa katika UislamuMachweoWilaya ya HandeniJamhuri ya Watu wa ChinaMkoa wa ArushaBendera ya KenyaBahari ya HindiJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaMV BukobaUngujaVita ya Maji MajiUfahamuAdhuhuriDagaaChama cha MapinduziMlongeJay MelodyJokofuIsraeli ya KaleUongoziZuchu🡆 More