Pakistan

Pakistani ni nchi ya Asia ya Kusini.

Imepakana na Ghuba ya Uarabuni upande wa kusini, Afuganistani na Uajemi upande wa magharibi, Uhindi upande wa mashariki na Uchina kaskazini-mashariki.

Pakistan
Ramani ya Pakistan
Ramani ya Pakistan

Mipaka yake na Uhindi na Uchina haitambuliki kimataifa. Pakistan na Uhindi zote mbili zinadai eneo la Kashmir zikitawala kila moja sehemu za eneo hili.

Jina la Pākistān lina maana ya "nchi ya watu safi" kwa Kiurdu.

Pakistani ina nafasi ya sita kati ya nchi duniani zenye watu wengi.

Ni nchi yenye Waislamu wengi duniani baada ya Indonesia.

Historia

Wakati wa ukoloni

Pakistani ilikuwa sehemu ya Uhindi wa Kiingereza hadi 1947.

Mwaka 1857 Wahindi walipinga utawala wa Kampuni ya Kiingereza kwa Uhindi wa Mashariki. Matokeo yake utawala ulishikwa na serikali yenyewe ya Uingereza kama koloni (1858).

Mwisho wa karne ya 19 harakati za Wahindi kutafuta uhuru zilianza upya. Mwaka 1885 chama cha INC (Indian National Congress) kiliundwa na Wahindu na Waislamu pamoja waliodai uhuru.

Mwaka 1906 viongozi Waislamu walitoka katika INC na kuunda "Shirikisho la Waislamu".

Mwaka 1917 Uingereza ulitamka ya kwamba ulitaka kuelekea polepole hali ya kujitawala kwa Wahindi. Viongozi wa wenyeji hawakuridhika na mkasi wa mabadiliko. Chini ya uongozi wa Mahatma Ghandi mwendo wa kupigania uhuru bila mabavu ulipata nguvu. Ghandi alipigania hasa umoja wa Wahindu na Waislamu lakini alipingwa na viongozi wenye itikadi kali wa pande zote mbili.

Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia Waingereza walikubali kujiondoa katika Uhindi. Swali kubwa lilikuwa kama nchi itabaki kama nchi moja au kama maeneo ya Waislamu yatajitenga.

Baada ya uhuru

Tarehe 14/15 Agosti 1947 utawala wa Uingereza ulikwisha. Bara Hindi iligawanywa katika nchi mbili za Uhindi na Pakistan. Mgawanyo wa Uhindi ulikuja na vita na kumwaga kwa damu nyingi.

Tarehe 30 Januari 1948 Ghandi mwenyewe aliuawa na Hindu mkali aliyemchukia kwa sababu alitaka usawa wa Waislamu na Wahindu.

Wakati ule ilikuwa nchi moja pamoja na Bangla Desh ya leo, lakini mwaka 1971 hizo pande mbili zilitengana baada ya vita kati yao.

Utawala

Nchi ni shirikisho la majimbo manne ya Punjab, Sindh, Jimbo la mpaka wa kaskazini-magharibi na Baluchistan, mbali ya maeneo matatu.

Watu

Lugha rasmi nchini Pakistan ni Kiurdu na Kiingereza. Lugha nyingine ni zaidi ya 60, lakini ni ndogo, zenye wasemaji wachache; karibu zote ni lugha za Kihindi-Kiulaya (angalia orodha ya lugha za Pakistan). Robo tatu za wakazi wanaelewa Kiurdu.

Asilimia 96.4 za wakazi ni Waislamu, hasa Wasuni. Ndiyo dini rasmi. Wahindu ni 2.14% na Wakristo 1.27%.

National symbols of Pakistan (Official)
National animal Pakistan 
National bird Pakistan 
National tree Pakistan 
National flower Pakistan 
National heritage animal Pakistan 
National heritage bird Pakistan 
National aquatic marine mammal Pakistan 
National reptile Pakistan 
National amphibian Pakistan 
National fruit Pakistan 
National mosque Pakistan 
National mausoleum
National river Pakistan 
National mountain Pakistan 

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Pakistan  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Pakistan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Pakistan HistoriaPakistan UtawalaPakistan WatuPakistan Tazama piaPakistan MarejeoPakistan Viungo vya njePakistanAfuganistaniAsia ya KusiniGhuba ya UarabuniMagharibiUajemiUchinaUhindi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Lahaja za KiswahiliUbepariSemiKishazi huruMlongeBongo FlavaOrodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaJumuiya ya Afrika MasharikiMashuke (kundinyota)Umoja wa MataifaBendera ya TanzaniaMlo kamiliKihusishiMwarobainiWaluguruKataVichekeshoWizara za Serikali ya TanzaniaInsha ya wasifuIdara ya Usalama wa Taifa (Tanzania)KipepeoDiamond PlatnumzTashihisiMoses KulolaUjuziNyimbo za jadiShabuOrodha ya kampuni za TanzaniaSimbaVivumishi vya pekeeKiambishiWamasaiUzazi wa mpangoMofolojiaHerufiEdward Ngoyai LowassaMahakama ya TanzaniaAfrika KusiniKisimaMauaji ya kimbari ya RwandaMsongolaNgonjeraMaishaMkoa wa ShinyangaMbuJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaWabunge wa Tanzania 2020Adolf MkendaMisaMuungano wa Tanganyika na ZanzibarUhuru wa TanganyikaArudhiVipaji vya Roho MtakatifuMaji kujaa na kupwaWakingaNyotaSarufiBarua rasmiBiashara ya masafa marefu ya Afrika MasharikiOrodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifaJamhuri ya Watu wa ZanzibarMmeaBenjamin MkapaSitiariUhindiUfupishoBilioniUkabaila🡆 More