Japani ni nchi ya visiwa katika Pasifiki, mkabala wa mwambao wa mashariki ya Asia.
Wajapani wenyewe hutumia jina la "Nihon" au "Nippon" lenye maana ya "Mwanzo wa jua". Hivyo Japani huitwa pia "Nchi ya Macheo".
Japani |
---|
Nchi ina eneo la km² 377.944; na wakazi milioni 127; idadi hiyo imeanza kupungua.
Japani ni kati ya nchi za dunia zilizoendelea sana upande wa sayansi, teknolojia na uchumi. Ilikuwa nchi ya kwanza nje ya Ulaya iliyofaulu kujenga jamii ya viwanda.
Japani ni funguvisiwa lenye visiwa 14,125 mbele ya pwani ya Uchina, Korea na Urusi (Siberia).
Visiwa vikubwa na muhimu zaidi ni vinne tu; ndivyo Honshu, Hokkaido, Shikoku na Kyushu. Safu ya milima inapita visiwa vyote vikubwa na kusababisha msongamano mkubwa wa wakazi katika miji kutokana na uhaba wa ardhi ya kukalia. Hali halisi Japani yote ni safu ya milima tu inayopanda juu kutoka sakafu ya bahari na vilele vya milima yake huonekana juu ya uso wa bahari kama visiwa vikubwa au vidogo.
Kijiolojia eneo hili liko kwenye mstari ambako mabamba ya gandunia ya Ulaya-Asia, Pasifiki na Ufilipino hukutana. Hii ni sababu ya kuwepo kwa volkeno 240 katika Japani na takriban 40 kati ya hizo ni hai pia kutokea kwa matetemeko ya ardhi ya mara kwa mara. Hivyo Japani ni sehemu ya pete ya moto ya Pasifiki inayozunguka bamba la Pasifiki.
Japani inapatwa kila mwaka na dhoruba kali aina ya taifuni. Hata tsunami (ni neno la Kijapani) ni kawaida. Nchi inajikinga na mitambo mengi ya kutoa taarifa ya tsunami kuanza pia mitambo ya kufunga milango ya mabandari.
Wajapani wengi hukalia sehemu ndogo ya 10% za nchi. Kuna miji kumi yenye wakazi zaidi ya milioni moja. Miji mikubwa ni Tokyo, Yokohama, Nagoya, Osaka, Kyoto, Kobe, Hiroshima, Fukuoka, Kitakyushu, Sendai na Sapporo. Usafiri ndani ya Japani ni hasa kwa treni, mabasi na ndege. Treni ya Shinkansen visiwani Honshu na Kyushu ni kati ya treni zenye mkasi mkubwa duniani.
Japan ina mikoa arubaini na saba. Kila mkoa unasimamiwa na gavana mmoja, bunge na urasimu utawala. Kila mkoa umegawanyika katika miji na vijiji.
1. Hokkaidō | 2. Aomori | 8. Ibaraki | 15. Niigata |
Kansai 24. Mie | 31. Tottori | 36. Tokushima | Kyūshū and Okinawa 40. Fukuoka |
Kwa sasa manispaa za Japani zinaundwa upya kwa kuunganisha mikoa, miji na baadhi ya vijiji. Mabadiliko hayo yatapunguza idadi ya miji nchini Japani.
Visiwa vilikaliwa na binadamu tangu miaka 30,000 KK.
Wakazi wa sasa wametokana na mchanganyiko wa makabila asili (kama Waainu) na Wakorea waliovamia visiwa hivyo.
Japani ni nchi ya tatu duniani kwa ukubwa wa uchumi.
ni vyakula kama vile kobe,jongoo, na mbpga za majani....pia njia za kiasili za kuabudu kama kwenye matempo mbalimbali
Wajapani wanaweza kushiriki ibada za dini mbalimbali kadiri wanavyojisikia, lakini asilimia 60 hawana dini maalumu. Wabuddha ni asilimia 34, wafuasi wa madhehebu ya Shinto ni asilimia 4, Wakristo sanasana ni asilimia 2.3.
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |
Makala hii kuhusu maeneo ya Japani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Japani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Japani, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.