Uzbekistan

Uzbekistan ni jamhuri ya Asia ya Kati.

Uzbekistan
Uzbekistan

Imepakana na Afghanistan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan na Turkmenistan.

Mji mkuu na pia mji mkubwa ni Tashkent.

Uzbekistan
Madrasa ya "Sherdor" mjini Samarkand

Historia

Uzbekistan ni nchi yenye historia ndefu. Ferghana, Tashkent, Bukhara, Khwarezm na Samarkand zilikuwa vitovu vya utamaduni wa binadamu tangu milenia ya 2 KK.

Katika karne kabla na baada ya Kristo eneo lilijulikana kama Sogdiana na Baktria. Miji yake ilikuwa na utajiri kutokana na biashara ya misafara kwenye barabara ya hariri kati ya China na Mashariki ya Kati.

Baadaye ilitawaliwa na milki mbalimbali za nje kama Uajemi.

Kuanzia uenezi wa Uislamu watu ba Uzbekistan waligeukia dini hiyo mpya.

Katika karne ya 14 jemadari Timur alijenga milki kubwa na kuharibu nchi za magharibi hadi Uturuki. Alipamba mji mkuu wake Samarkand kwa majengo mazuri.

Baada ya Timur milki yake iliporomoka na Uzbekistan ilitawaliwa na madola mbalimbali ya kieneo yaliyokuwa hasa eneo la mji muhimu.

Katika karne ya 19 Urusi ulieneza athira yake kuelekea kusini na kuunganisha madola ya Uzbekistan na milki yake.

Baada ya mapinduzi ya Urusi ya mwaka 1917 Uzbekistan ikawa sehemu ya Umoja wa Kisovyeti hadi kuporomoka kwake mwaka 1991. Ilijulikana kwa jina la "Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiuzbeki" hadi 1991.

Tarehe 31 Agosti 1991 ilijitangaza huru na kudai kufuata demokrasia na kuelekea soko huria, lakini hadi sasa haki za binadamu haziheshimiwi sana.

Watu

Kuna wakazi 32,768,725 (2019).

Walio wengi (zaidi ya 83%) hutumia lugha ya Kiuzbeki ambacho ni kati ya lugha za Kiturki na ndiyo lugha rasmi. Angalia pia orodha ya lugha za Uzbekistan.

Kuna makundi mengi vidogo zaidi vya utamaduni tofauti kama vile Watajiki (4.8%), Wakazakhi (2.5%), Warusi (2.3%), Wakarakalpaki (2.2%), Watartari (1.5%), Wakorea (1,1%) na mengine.

Upande wa dini, 88.6% ni Waislamu, lakini wengi wao hawana madhehebu maalumu; Wasuni ni 18% na Washia 1%. Wakristo ni 9.4%, wengi wakiwa Warusi Waorthodoksi; Waprotestanti na Wakatoliki hawafikii 3%.

Tazama pia

Viungo vya nje

Uzbekistan 
Wiki Commons ina media kuhusu:

Uzbekistan  Uzbekistan travel guide kutoka Wikisafiri

    Taarifa za jumla
    Vyombo vya habari

Vyanzo vingine

Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Uzbekistan  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Uzbekistan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Uzbekistan HistoriaUzbekistan WatuUzbekistan Tazama piaUzbekistan Viungo vya njeUzbekistanAsia ya KatiJamhuri

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

TanganyikaKipepeoKontuaYvonne Chaka ChakaMbuga wa safariJohn MagufuliTarakilishiNandyHekaya za AbunuwasiHekimaMaliasiliMkoa wa IringaUhifadhi wa fasihi simuliziHaki za wanyamaMisemoMfumo wa nevaMartha MwaipajaMfumo wa homoniMkoa wa SimiyuHussein KaziPaul MakondaDaktariRedioOrodha ya vitabu vya BibliaMbuyuUkatili wa kijinsiaKampuniNadhariaMkoa wa KigomaMashariki ya KatiKihusishiMfumo wa mzunguko wa damuWilaya ya MboziKiingerezaWikipedia ya KiswahiliMbooMnara wa BabeliMatiniJokate MwegeloHistoria ya Kanisa KatolikiPemba (kisiwa)ItikadiTetemeko la ardhiAfro-Shirazi PartyKamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniMkonoBikiraRaiaMimba kuharibikaGhanaMavaziMvuaLionel MessiPentekosteNambaUmoja wa AfrikaLady Jay DeeMaishaAfrika Mashariki 1800-1845WanyaturuMsalaba wa YesuMkoa wa MwanzaBilioniPasaka ya KiyahudiMazoezi ya mwiliKongoshoMweziSteve MweusiNyanda za Juu za Kusini TanzaniaUshairiUvimbe wa koromeo usababishwao na streptokokiMadhehebuKanisa KatolikiJulius Nyerere🡆 More