Dar Es Salaam

Kwa maana nyingine, tazama Mkoa wa Dar es Salaam


Dar es Salaam
Jiji la Dar es Salaam
Jiji la Dar es Salaam
Jiji la Dar es Salaam
Dar Es Salaam
Nembo
Mahali paDar es Salaam
Mahali paDar es Salaam
Majiranukta: 6°48′0″S 39°17′0″E / 6.80000°S 39.28333°E / -6.80000; 39.28333
Nchi Tanzania
Mkoa Dar es Salaam
Tarafa 12
Kata 102
Mitaa 565
Serikali
 - Aina ya serikali Jiji
 - Mstahiki Meya Omary S. Kumbilamoto
 - Mkurugenzi wa Jiji Jumanne K. Shauri
Idadi ya wakazi (2022): 74 
 - Wakazi kwa ujumla 5,383,728
EAT (UTC+3)
Msimbo wa posta 11xxx
Kodi ya simu 022
ISO namba TZ-02
Tovuti:  Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

Dar es Salaam ni jiji kubwa kuliko yote nchini Tanzania. Pia ni jina la mkoa wake. Dar es Salaam ni mji mkongwe na wenye watu wengi zaidi katika Jumuia ya Afrika Mashariki. Katika Tanzania ndio mji wenye vitega uchumi vingi na ndio mji unaoangaliwa na watu wengi.

Ni mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania wakati Dodoma ni mji mkuu wa Tanzania (kinadharia tangu mwaka 1973). Mpango wa kuhamishia serikali mjini Dodoma unaendelea kwa kasi chini ya rais John Magufuli, japokuwa bado ofisi kadhaa za serikali, ikiwa ni pamoja na Ikulu, zipo Dar es Salaam.

Mji una wakazi wapatao 5,383,728 kwa hesabu ya sensa iliyofanyika katika mwaka wa 2022.

Jina

Dar Es Salaam 
Picha kutoka angani ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Jina la Dar es Salaam linatoka katika Kurani ambako linamaanisha mahali patulivu au hata paradiso. Surah Al-Anam (Korani 6:127) ina maneno لَهُمْ دَارُ‌ السَّلَامِ عِندَ رَ‌بِّهِمْ lahum dāru as-salāmi `inda rabbihim yanayomaanisha "Hao watapata nyumba ya salama kwa Mola Mlezi wao." . Jina linafanywa na maneno mawili ya Kiarabu; دار dar inayomaanisha "nyumba, jengo, makazi, eneo", "es" ni silabi ya kuunganisha sehemu za jina linalounganishwa na maneno mawili, سلام salaam inamaanisha "amani, raha, usalama".

Dar Es Salaam 
Sehemu ya Dar es Salaam.

Mara nyingi jina limetafsiriwa kama "Bandari ya Amani" lakini hii ni kosa kutokana na kuchanganya maneno ya Kiarabu دار "dar" (nyumba) na بندر "bandar" (bandari) maana kwa matamshi ya Kiswahili tofauti ya tahajia katika Kiarabu haitambuliki.

Jina la Daressalaam limetumiwa kwa maumbo tofauti kwa mahali mbalimbali katika mazingira ya Kiislamu, kwa mfano huko Brunei Darussalaam, Dar El Salam (Misri), Dar os Salam (Iran), pia kama majina ya taasisi mbalimbali.

Historia

    Makala kuu: Historia ya Dar es Salaam

Jiji hili zamani lilikuwa kijiji na kuitwa Mzizima. Sultani Seyyid Majid wa Zanzibar aliamua kujenga ikulu ya pili barani kando la Mzizima akachagua jina "Dar es Salaam". Hadi leo kuna majengo mawili yaliyobaki ya vyanzo hivi ambayo ni Boma la Kale na Nyumba ya Atiman House.

Dar es Salaam ilichaguliwa na wakoloni Wajerumani kuwa mji mkuu wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kwa sababu ya bandari asilia yenye mdomo mpana wa mto Kurasini. Hivyo kuanzia mwaka 1891 Dar es Salaam ilichukua nafasi ya Bagamoyo kama makao makuu ya utawala.

Bandari pamoja na ujenzi wa reli ya kati kwenda Kigoma tangu mwaka 1904 viliimarisha nafasi ya mji ulioendelea kama mji mkuu baada ya Tanzania bara ya leo kuwa eneo lindwa la Tanganyika chini ya Uingereza.

Dar Es Salaam 
Sanamu ya Askari mjini Dar es Salaam

Utawala

Utawala wa Dar es Salaam uliona mabadiliko kadhaa ambapo mwanzoni mji ulitawaliwa na halmashauri yake na baadaye serikali ya kitaifa ilichukua utawala mikononi mwake au kuukabidhi kwa tume ya serikali.

Mwaka 2000 eneo la jiji liligawanywa kwa mamlaka tofauti ambazo mwanzoni zilikuwa nne, ambazo zilikuwa manisipaa za Ilala, Temeke na Kinondoni. Baadaye Ubungo na Kigamboni zilikuwa manisipaa za pekee, kila moja na halmashauri yake. Kwa jiji lote Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iliundwa. Kwa hiyo hadi 2021 Dar es Salaam ilikuwa na Halmashauri 6.

  • Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
  • Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
  • Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni
  • Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
  • Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
  • Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

Kwenye Februari 2021 Halmashauri ya Dar es Salaam ilivunjwa na serikali, na Ilala ilibadilishwa jina kuwa Dar es Salaam.

Wakazi na uchumi

Dar es Salaam inakadiriwa kuwa na wakazi wapatao milioni tatu. Ingawa Dodoma inafahamika kama ndio mji mkuu wa Tanzania, Dar es Salaam ndiko ziliko ikulu, mabalozi, mashirika ya kimataifa, n.k.

Uwanja wa ndege mkuu wa Tanzania uko pia mjini hii ni Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.

Bandari ya Dar es Salaam katika bahari ya Hindi, ndio bandari kubwa nchini Tanzania inayojihusisha na usafirishaji na uingizaji wa bidhaa mbalimbali za kilimo, ufugaji, ujenzi, magari, madawa, n.k.

Kiutawala, Dar es Salaam imegawanywa katika manisipaa za Temeke, Ilala, Kinondoni, Kigamboni na Ubungo.

Wakazi na uchumi

Dar Es Salaam 
Nyerere Bridge huko Kigamboni, Dar es Salaam, ni daraja pekee la Afrika Mashariki lisilo na nguzo majini.

Dar es Salaam ni mji unaosemekana kuwa mkubwa kuliko yote kwa sababu ya maendeleo mbalimbali ya viwanda, uwepo wa bahari, uwepo wa sehemu mbalimbali za kihistoria n.k.

Huduma za jiji

Huduma ya maji Dar es Salaam imekuwa na tatizo kubwa katika kudhibiti mfumo wa maji taka katika mkoa wa Dar es Salaam kwa muda mrefu. Tangu shirika la maji DAWASCO (Dar es Salaam Water Supply Company) lilipowekwa rasmi kama shirika husika katika kuratibu utaratibu mzima wa mfumo wa maji safi na maji taka, kumekuwa na nafuu kidogo tu, lakini baada ya muda, liliibuka tatizo la kuibiwa kwa mabomba na uharibifu wa vyanzo mbalimbali vya maji.

Elimu

Kwenye suala hili la elimu vijana wanatakiwa kupewa elimu; hasa vijana wa mitaani wasioingiza kipato inabidi wapewe elimu kwa kazi fulani ili waweze kuajiriwa na kulipa faida taifa kwa kuingizia kipato na kukuza uchumi wa taifa. Mfano wa kazi hizo ni kama ujenzi wa nyumba n.k.

Picha

Marejeo

Viungo vya nje

Dar Es Salaam 
Wiki Commons ina media kuhusu:

Tags:

Dar Es Salaam JinaDar Es Salaam HistoriaDar Es Salaam UtawalaDar Es Salaam Wakazi na uchumiDar Es Salaam Wakazi na uchumiDar Es Salaam Huduma za jijiDar Es Salaam ElimuDar Es Salaam PichaDar Es Salaam MarejeoDar Es Salaam Viungo vya njeDar Es SalaamMkoa wa Dar es Salaam

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

InshaKidole cha kati cha kandoShairiHifadhi ya SerengetiLahaja za KiswahiliAbedi Amani KarumeDodoma (mji)AlomofuMkwawaMuungano wa Tanganyika na ZanzibarUgonjwa wa uti wa mgongoNomino za pekeeLugha za KibantuWamasaiIntanetiSwalaInstagramBurundiMkoa wa NjombeKalenda ya GregoriIrene PaulHassan MwakinyoHedhiTabianchiMamba (mnyama)KomaKaswendeUkoo wa YesuSanaaDiamond PlatnumzTanescoAsubuhiVinícius JúniorZambiaMkoa wa Unguja Mjini MagharibiDavid LivingstoneUti wa mgongoHistoria ya TanzaniaRupie ya Afrika ya Mashariki ya KijerumaniSarufiYordaniKunguniKadi ya adhabuOrodha ya nchi kufuatana na wakaziSimba (kundinyota)MajigamboTarakilishiUingerezaTulia AcksonPamba S.C.Barua rasmiMaumivu ya kiunoHistoria ya BurundiBahari ya HindiNenoHaki za binadamuChuraIkulu ya TanzaniaNikki wa PiliUandishiMkoa wa PwaniMzeituniViunganishiMitume na Manabii katika UislamuMimba kuharibikaChotaraOrodha ya miji ya TanzaniaUzalendoMfumo katika sokaNgano (hadithi)MpwaOrodha ya wanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoAfrika ya Mashariki ya Kijerumani🡆 More