Kadi za adhabu hutumika katika michezo mingi sana: ni aina ya onyo, karipio au kutoa adhabu kwa mchezaji, kocha au afisa wa timu.
Kadi za adhabu hutumiwa hasahasa na refa au mwendesha mchezo, na Huonyeshwa endapo mchezaji kafanya kosa. Refa hunyoosha kadi juu huku akimuangalia au akimnyoshea kidole mchezaji aliyefanya kosa. Kitendo hicho ni kwa kusudi la kuonyesha wazi wachezaji wengine pamoja na watazamaji kwamba mchezaji fulani kapewa adhabu fulani. Rangi na umbo la kadi huelezea kiwango cha kosa, vilevile kiwango cha adhabu kwa mchezaji husika. Kadi zinazotumika sana ni kadi ya njano na kadi nyekundu.
Wazo la kutumia lugha isiyo na upande ya kadi za rangi kama njia ya mawasiliano baina ya wachezaji na refa ulianza katika mchezo wa soka, refa wa Uingereza Ken Aston ndiye aliyetoa wazo hilo. Bwana Aston aliwahi kuwa mjumbe wa bodi ya FIFA na alikuWa msimamizi wa marefa wote katika fainali za kombe la dunia za mwaka 1966. Katika hatua ya robo fainali timu ya taifa ya uingereza ilikutana na timu ya taifa ya Argentina katika uwanja wa Wembley. Baada ya mchezo huo, magazeti yaliandika habari zinazohusu refa wa mchezo Rudolf Kreitlein kuwapa onyo wachezaji wa Uingereza Bobby Charlton na Jack Charlton, vilevile kumtoa nje mchezaji wa Argentina Antonio Rattín. Refa hakuweka wazi maamuzi yake wakati wa mchezo, baadaye kocha wa Uingereza Alf Ramsey alienda kwa Mwakilishi wa FIFA kupata ufafanuzi zaidi. Tukio hilo lilimfanya Aston afikirie njia mbadala zitakazotumika na refa ili kueleza maamuzi yake kwa wachezaji na watazamaji kwa urahisi zaidi. Aston alibaini kwamba matumizi ya rangi hufuata taratibu zinazofanana (kama tu zile zinazotumika katika taa za barabarani njano – simama kama ni salama, nyekundu – simama) na huvunja vikwazo vya lugha na ingeelezea vizuri kama mchezaji kapewa onyo au kaondolewa kabisa uwanjani.
Matokeo yake, kadi ya njano ilimaanisha mchezaji kapewa onyo na kadi nyekundu mchezaji katolewa nje ya uwanja kabisa na hii ilianza kutumika katika fainali za kombe la dunia mwaka 1970 nchini Mexico. Kuanzia wakati huo, matumizi ya kadi yamekua kwa kasi na kila mchezo ukiongeza sheria zake na kuongeza aina za kadi katika michezo husika.
Kadi ya njano hutumika katika sharia za ishara ya michezo mingi tofauti. Tafsiri yake hotafautiana baina ya michezo; hata na hivyo, kwa kawaida huashiria onyo kwa mchezaji kutokana na tendo Fulani, au huweza kumaanisha kutolewa nje ya mchezo kwa muda mfupi. Mifano hujumuisha:
kadi nyekundu hutumiwa kama ligha ya ishara katika michezo mingi. Tafsiri yake hutofautiana baina ya michezo, lakini kwa kawaida huonyesha kitendo kibaya kisicho cha kimchezo na mchezaji aliyetenda kitendo hicho hutolewa nje ya uwanja. Katika michezo mingi, mchezaji akitolewa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu, nafasi atakayoiacha uwanjani haitaweza kuzibwa kwa kuingiza mchezaji mwingine. Mifano huumuisha:
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Kadi ya adhabu kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Kadi ya adhabu, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.