Stadi za maisha ni maarifa yanayotarajiwa kumsaidia mtu kuishi vema .
Maisha ni muambatano wa muda pamoja na matukio, hivyo ni muhimu kufahamu kuwa muda unavyozidi kwenda ndipo kiumbehai kinapopata nafasi ya kupita katika matukio mbalimbali yaliyo mazuri na mabaya, amayo yote huhitaji hekima na maarifa katika kuyapitia hususan yaliyo mabaya.
Kuna msemo wa lugha ya Kiswahili unaosema kuwa "Kuishi kwingi ni kuona mengi": maana halisi ni kuwa mtu aliyemtangulia mwenzake kiumri anakuwa na uzoefu mkubwa sana kwa sababu mambo ambayo amekwisha kuyaona ni mengi katika kuishi kwake. Kupitia uzoefu huo ndivyo mtu huyo anapata mbinu nyingi za kumwezesha yeye kukabiliana na nyakati zote katika maisha yake.
Haina maana ya kwamba mtu mwenye umri mdogo, kwa sababu ya kuwa na uzoefu mdogo wa kimaisha, basi anapaswa kukosa busara na hekima za kumwezesha yeye kuishi vizuri.
Mtoto au kijana anaweza kuwa na hekima kama ya mzee kwa kujifunza stadi za maisha ambazo ni kama zifuatazo:
Hizi ni mbinu au kanuni ambazo zinamwezesha mhusika kuwa na uwezo mkubwa wa kujitambua, kwanza kiundani zaidi, kwa maana ya hisia, uwezo, madhaifu na nafasi yake katika jamii. Stadi binafsi ni muhimU sana kwa sababu zinamwezesha mhusika huyo kujijengea hali ya kujiamini kutokana na kuitambua thamani yake katika jamii inayomzunguka.
Ili kuwa bora katika stadi binafsi mhusika anapaswa kuwa na uwezo katika vitu vifuatavyo: kujitambua, kutambua mahitaji na kuweka malengo katika maisha.
Hizi ni stadi ambazo humjenga na kumwezesha mhusika kujua naamna ya kuishi na watu kwa upendo na amani na kujenga ushirikiano ulio bora. Vifuatavyo ni vipengele muhimu ambavyo vinamthibitisha mtu kuwa stadi za kijamii:
Hizi ni stadi ambazo zinamwezesha mhusika kufanya maamuzi sahihi wakati wa changamoto na yanapotokea machaguo mengi. Kama ilivyo katika stadi nyingine hizi pia zina kanuni ambazo ndizo msingi wa kupatikana kwa maamuzi sahihi, nazo ni kama ifuatavyo.
Watu hujifunza/kuiga stadi za maisha katika sehemu, makundi au watu mbalimbali ila sehemu au vitu ambavyo ndio msingi wa stadi za maisha ni hizi zifuatazo.
Hapa tunajifunza na kuiga vitu kutoka kwa wazazi au ndugu zetu kwa sababu tunaishi nao kwa muda mreefu, hususani katika kipindi cha ukuaji wetu ambacho ndicho kipindi vichwa vyetu vinapodaka na kukariri mambo mengi.
Hapa mara nyingi ni kupitia maarifa tunayopata kwa kufundishwa na wakufunzi hususadi shuleni, vyuoni na kadhalika.
Tofauti na familia kuna kundi jingine kubwa ambalo linatuzunguka, hivyo lenyewe pia lina mchango katika kutujenga kifikra na kuendeleza stadi zetu za kimaisha.
Imani tofautitofauti zimekuwa zikitoa mafunzo mengi ya kidini ambayo yamekuwa yakihusika katika kuwajenga waumini wake. Kwa mfano imani ya Kikristo imekuwa ikifundisha juu ya amri kuu ya upendo, kitu ambacho ni stadi muhimu inayowezesha mtu kuishi vizuri na watu katika jamii yake.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Stadi za maisha kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Stadi za maisha, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.