Jumamosi kuu ni siku ya Juma kuu inayoadhimisha hasa pumziko la mwili wa Yesu Kristo kaburini na roho yake kushukia kuzimu kabla ya kufufuka kwa utukufu usiku wa kuamkia Jumapili ya Pasaka.
Tarehe yake inabadilikabadilika kila mwaka na hata mwaka uleule ni tofauti katika madhehebu ya Ukristo, hasa yanayofuata mapokeo ya mashariki na yale yanayofuata mapokeo ya magharibi.
Siku hiyo Misa na sakramenti mbalimbali haziadhimishwi kwa kuwa wafuasi wa Yesu wanatulia kimya wakitafakari matukio ya Ijumaa kuu na kujiandaa washangilie ufufuko wake kuanzia kesha la Pasaka hadi Jumapili ya Pentekoste siku 50 baadaye.
Jumamosi kuu inaitwa kwa namna tofauti katika lugha mbalimbali. Baadhi ya mifano ni kama ifuatavyo:
Lugha | Jina | Tafsiri |
---|---|---|
Kicheki | Bílá sobota | Jumamosi nyeupe |
Kifaransa | Samedi saint | Jumamosi takatifu |
Kihispania | Sábado Santo | Jumamosi takatifu |
Kiholanzi | Stille Zaterdag | Jumamosi ya kimya |
Kihungaria | Nagyszombat | Jumamosi kuu |
Kiingereza | Holy Saturday | Jumamosi takatifu |
Kiitalia | Sabato Santo | Jumamosi takatifu |
Kijapani | 聖土曜日 (Sei Doyoobi) | Jumamosi takatifu |
Kijerumani | Karsamstag | Jumamosi ya ombolezo |
Kipolandi | Wielka Sobota | Jumamosi kuu |
Kislovakia | Biela sobota | Jumamosi nyeupe |
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jumamosi kuu kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Jumamosi kuu, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.