Juma

Juma (kutoka neno la Kiarabu) au wiki (kutoka Kiingereza week) ni kipindi cha siku saba.

Kila siku ina jina lake.

Katika mwaka wa kalenda ya Gregori mna majuma 52 pamoja na siku moja au mbili za ziada. Hesabu ya majuma inaendelea mfululizo bila ya kuanza upya wakati wa mwaka mpya.

Ufuatano wa majuma haulingani na mgawanyo mwingine wa wakati kwa njia ya miezi au mwaka.

Mapokeo ya Kiyahudi-Kikristo

Asili ya juma ni katika utamaduni wa kale wa Mashariki ya Kati tangu Babiloni. Imeenea duniani kote kupitia Biblia na desturi za Uyahudi na Ukristo.

Ufuatano wa siku katika mapokeo hayo huanza na Jumapili. Majina ya siku ni kama yafuatayo:

Katika mwaka juma moja la Machi mwishoni au la Aprili linaadhimishwa na Wakristo wengi kama Juma kuu, ambapo wanaadhimisha matukio makuu ya imani yao kadiri ya historia ya wokovu, yaani mateso, kifo na ufufuko wa Yesu Kristo.

Siku za Jumamosi na Jumapili mara nyingi huitwa "wikendi" (kutoka Kiingereza: "weekend", yaani mwisho wa juma). Hata hivyo katika mapokeo hayo Jumapili ni mwanzo wa wiki mpya, si mwisho wake.

Majina ya siku kwa Kiswahili

Majina ya siku tano kwa Kiswahili ni ya namba zinazoanza kuhesabiwa baada ya siku ya Ijumaa (ambayo ni siku ya sala kuu katika Uislamu): Ijumaa - Jumamosi - Jumapili - Jumatatu - Jumanne - Jumatano.

Alhamisi na Ijumaa ni majina ya lugha ya Kiarabu inayofuata mapokeo ya Kiyahudi kuhusu majina ya siku.

Hivyo "Alhamisi" ina maana ya "siku ya tano" (baada ya Jumamosi inayoitwa "sabat" kwa Kiarabu, sawa kama "shabbat" kwa Kiebrania (lugha ya Wayahudi).

"Ijumaa" ni matamshi ya Kiswahili ya jina la Kiarabu la "jum'a" inayomaanisha "siku ya mkutano" (= ya kusali pamoja).

Siku za juma (wiki)
Jumapili - Jumatatu - Jumanne - Jumatano - Alhamisi - Ijumaa - Jumamosi
Juma  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Juma kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

JinaKiarabuKiingerezaNenoSabaSiku

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa TanzaniaKifaruRejistaStashahadaHistoria ya IranMajiLatitudoMuhimbiliJakaya KikweteTupac ShakurTabianchiMkoa wa MorogoroShahawaMaumivu ya kiunoNgono zembeMichael JacksonAlama ya uakifishajiWanyama wa nyumbaniKiboko (mnyama)Ala ya muzikiRupie ya Afrika ya Mashariki ya KijerumaniMapambano kati ya Israeli na PalestinaKiraiSwalaYoung Africans S.C.Orodha ya Makamu wa Rais TanzaniaMaandishiPaul MakondaMwanaumeMaktabaShangaziVivumishi vya urejeshiTulia AcksonTendo la ndoaVivumishi vya kumilikiMohammed Gulam DewjiBabeliMkopo (fedha)Christopher MtikilaLady Jay DeeBenjamin MkapaNafsiManchester CityUsafi wa mazingiraChama cha MapinduziMwanza (mji)Mkoa wa TaboraUfahamuOrodha ya Marais wa KenyaMahakamaRita wa CasciaMkoa wa SongweHadithi za Mtume MuhammadSaidi Salim BakhresaUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaLughaKaaBonde la Ufa la Afrika ya MasharikiNusuirabuJulius NyerereWashambaaJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaVisakaleMlima wa MezaHistoria ya Kanisa KatolikiWaziriKitenzi kishirikishiMavaziStephane Aziz KiMoses KulolaUrusiInsha🡆 More