Jumatatu: Moja ya siku saba za wiki

Jumatatu ni siku ya pili katika juma (wiki) ya siku saba yenye asili ya kiyahudi-kikristo.

Iko kati ya siku za Jumapili na Jumanne.

Siku ya pili au siku ya kwanza?

Kuna nchi zilizobadilisha hesabu kufuatana na kawaida ya "wikendi" kwenye siku za Jumamosi/Jumapili ambako Jumatatu ni siku ya kwanza katika juma ya kazi hivyo inahesabiwa kama siku namba "1" ya wiki katika kalenda rasmi za serikali hata kama jumuiya za kidini zinasisitiza hesabu ya kibiblia.

Kiswahili, Kiarabu na utamaduni wa Kiislamu

Katika lugha ya Kiswahili jina la siku lina namba "3" ndani yake. Hii ni dokezo la asili ya Kiswahili katika utamaduni ya Kiislamu pasipo na athira ya Uyahudi unaoanza hesabu baada ya sikukuu ya Kiislamu ya Ijumaa siku ya sala ya pamoja: Jumamosi kama siku ya kwanza baada ya Ijumaa, Jumapili kama siku ya pili, Jumatatu kama siku ya tatu n.k.. Tabia hii katika Kiswahili ni ya pekee hasa kwa sababu Kiarabu ambacho ni lugha ya Korani takatifu na lugha ya kimataifa ya Waislamu kinafuata hesabu ya Kiyahudi na kuiita siku "ya pili".

Siku ya mwezi

Katika lugha mbalimbali za Ulaya siku hii ina jina la "mwezi". Lugha hizi kama Kiingereza, Kifaransa au Kijerumani zinaendeleza urithi wa Roma ya Kale na zaidi wa Babiloni ambako kila siku ya wiki ilikuwa chini ya mungu fulani aliyeonekana kama nyota.

Jumatatu katika lugha mbalimbali

Majina ya Jumatatu katika tamaduni mbalimbali
Lugha Matamshi Maana Maelezo
Kiebrania יום שני
jom schenai
siku ya pili
Kigiriki Δευτέρα
deutéra
(siku) ya pili
Kiarabu الاثنين
al-ithnayn
(siku) ya pili ي
Kiajemi دوشنبه
do-schanbe
siku ya pili
Kireno Segunda-feira
siku ya pili
Kilatini dies lunae Siku ya mwezi
Kiitalia lunedì Siku ya mwezi
Kihispania lunes Siku ya mwezi
Kifaransa lundi Siku ya mwezi
Kijerumani Montag Siku ya mwezi
Kiingereza Monday Siku ya mwezi
Kituruki Pazartesi baada ya Jumapili (=pazar)
Siku za juma (wiki)
Jumapili - Jumatatu - Jumanne - Jumatano - Alhamisi - Ijumaa - Jumamosi

Tags:

Jumatatu Siku ya pili au siku ya kwanza?Jumatatu Kiswahili, Kiarabu na utamaduni wa KiislamuJumatatu Siku ya mweziJumatatu katika lugha mbalimbaliJumatatuJumaJumanneJumapiliUkristoUyahudi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

WabondeiDubaiHeshimaMjombaMichezoHuduma ya ujumbe mfupiYoung Africans S.C.Homa ya matumboFisiMofolojiaMfumo wa homoniWahangazaKunguniNambaVivumishi vya kumilikiWachaggaWenguMunguMtandao wa kompyutaWanyakyusaNomino za wingiNusuirabuMadhehebuBawasiriJoseph ButikuMbadili jinsiaKamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniMartin LutherKampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya MasharikiNgano (hadithi)Orodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaMwanzo (Biblia)Afrika KusiniRaiaMajigamboWabunge wa Tanzania 2020Orodha ya Watakatifu WakristoAli Hassan MwinyiAngahewaWagogoMitume wa YesuWhatsAppMsalaba wa YesuBonde la Ufa la Afrika ya MasharikiMsumbijiWimbo wa Jumuiya ya Afrika MasharikiDamuVivumishi vya idadiUmoja wa KisovyetiRayvannySemi23 ApriliOrodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaOrodha ya volkeno nchini TanzaniaMkoa wa PwaniTarakilishiAlfabetiJogooHafidh AmeirWanyamweziAjuzaElimuRwandaVipera vya semiKishazi tegemeziKalenda ya KiislamuHoma ya mafuaOrodha ya viongoziEthiopiaLigi ya Mabingwa AfrikaAlama ya uakifishajiReal MadridEdward Ngoyai LowassaKifua kikuuSamaki🡆 More