Mavazi

Mavazi (kutoka kitenzi kuvaa) ni nguo ambazo huvaliwa na watu ili kufunika mwili au sehemu zake.

Mavazi huwa na makusudi mbalimbali:

  • hukinga mwili dhidi ya baridi au jua kali pamoja na athira nyingine za mazingira zinazoweza kuathiri vibaya mwili uchi.
  • huwasilisha ujumbe kwa watu wengine kwa kuonyesha mtu fulani ni sehemu ya kundi (k.m. jeshi, timu, dini, kabila) au tabaka (nguo ghali za tajiri) au anapendelea jambo (nembo kwenye nguo).
Mavazi
Kanga ni mavazi ya wanawake wa Afrika Mashariki (hapa: Pate).
Mavazi
Mwanamke akifua nguo zake

Kimsingi nguo zinalingana na hali ya hewa na mazingira. Penye joto mavazi huwa mepesi na penye baridi huwa mazito zaidi. Kila utamaduni umebuni aina zake za mavazi.

Historia inaonyesha pia ya kwamba tangu kale tamaduni mbalimbali zimepokea mavazi kutoka nje na kubadilisha mitindo yao. Hata kama katika majira ya utandawazi watu wanavaa nguo zilezile bado wanaweza kuzitumia tofauti.

Kuna mavazi ya aina nyingi, kwa mfano ya kitambaa, nguo, sufi, ngozi au plastiki.

Vilevile mavazi hutofautishwa kama ni ya wanaume, wanawake au watoto, kama ni mavazi ya kikazi au ya nyumbani au ya sikukuu.

Tofauti nyingine ni kama mavazi ya chini au ya juu, au kama ni mavazi ya sehemu mbalimbali za mwili kama vile suruali, mashati, koti au viatu.

Utengenezaji na uuzaji ya mavazi ni sehemu muhimu ya biashara na kuna kazi nyingi zinazotegemea mavazi. Mavazi pia ni tasnia kubwa duniani inayohusisha ubunifu, uzalishaji, na mauzo ya nguo. Watu wanaweza kuchagua mavazi yao kulingana na mahitaji yao binafsi, muktadha wa kijamii, na mwenendo wa wakati huo.

Viungo vya nje

Mavazi 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
Mavazi  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mavazi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

KitenziMwiliNguoWatu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Clatous ChamaHistoria ya WapareIpagalaMikoa ya TanzaniaUgaidiNyongoDoto Mashaka BitekoViwakilishi vya pekeeMadawa ya kulevyaOrodha ya nchi kufuatana na wakaziMabiboMsamahaJinaTume ya Taifa ya UchaguziOmmy DimpozMagonjwa ya machoMaudhui katika kazi ya kifasihiAgano la KaleMgawanyo wa AfrikaSakramentiMasadukayoMkoa wa TaboraMnyoo-matumbo MkubwaStephane Aziz KiChuo Kikuu cha DodomaMagomeni (Dar es Salaam)Hekaya za AbunuwasiZabibuWagogoBinadamuVitenzi vishiriki vipungufuMatiniIntanetiWamasaiNgiriNandySelemani Said JafoNgome ya YesuPombooYoung Africans S.C.Tenzi tatu za kaleManispaaMapambano ya uhuru TanganyikaMtaalaIniChanika (Ilala)MbossoMkoa wa TangaMauaji ya kimbari ya RwandaDhamiraFananiVihisishiUandishi wa inshaMuungano wa Madola ya AfrikaVivumishiMwigizajiUbunifuUchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2020SarataniAzimio la ArushaMarekaniHistoria ya Kanisa KatolikiNyotaKaaJumuiya ya Afrika MasharikiSaida KaroliFigoKanisa la Kiinjili la Kilutheri TanzaniaTamathali za semi🡆 More