Kijerumani

Kijerumani (pia: Kidachi, kwa Kijerumani: Deutsch au (die) deutsche Sprache) ni lugha ya Kigermanik ya magharibi katika jamii ya lugha za Kihindi-Kiulaya.

Hadhi ya Kijerumani katika nchi mbalimbali.
Hadhi ya Kijerumani katika nchi mbalimbali.
Kijerumani
Nchi ambako lugha ya Kijerumani huzungumzwa.

Huzungumzwa hasa katika nchi za Ujerumani, Austria, Uswisi, Liechtenstein na Luxemburg.

Kuna pia wasemaji asilia katika nchi jirani za Ujerumani / Austria kama Ubelgiji, Uholanzi, Ufaransa, Denmark, Poland na Italia ya kaskazini. Nchi nyingi za Ulaya ya Mashariki zilikuwa na wasemaji wa Kijerumani lakini wengi walifukuzwa au kuondoka wakati wa vita kuu ya pili ya dunia; vikundi vimebaki hasa katika Hungaria, Romania, Uceki, Urusi na Kazakhstan.

Vikundi vidogo vya watu waliohamia katika karne za 19 na 20 wanaoendelea kutumia Kijerumani wako katika Amerika ya Kaskazini (Marekani, Kanada), Amerika Kusini (Brazil, Chile) na Afrika (hasa Namibia na Afrika Kusini).

Kijerumani huzungumzwa na watu milioni 100 katika Ulaya. Ni lugha ya pili katika Ulaya baada ya Kirusi kushinda Kifaransa na Kiingereza.

Kijerumani kama lugha ya kitaifa

Kijerumani kinatumiwa kama lugha rasmi kitaifa katika nchi zifuatazo:

Lugha rasmi kieneo

Kijerumani kinatumiwa kama lugha rasmi ya utawala kieneo (ama kimkoa au kwenye ngazi ya miji / tarafa tu) katika nchi zifuatazo:

Umoja wa Ulaya

Kijerumani ni kati ya lugha rasmi za Umoja wa Ulaya pamoja na Kiingereza na Kifaransa. Kati ya lugha ndani ya Umoja ni lugha yenye wasemaji wengi kushinda nyingine zote.

Lugha inayofundishwa

Kijerumani kama lugha ya kigeni kinafundishwa shuleni au kwenye taasisi za elimu ya watu wazima katika nchi nyingi. Mwaka 2004 idadi ya wanafunzi wa Kijerumani ilikuwa kama ifuatayo:

Kijerumani ni lugha ya pili katika mtandao (intaneti) baada ya Kiingereza. Takriban nusu ya kurasa zote mtandaoni ni za Kiingereza, lakini Kijerumani kinafuata kikiwa na 8% za kurasa zote.

Kijerumani kimeathiri kwa kiasi fulani lugha ya Kiswahili cha Tanzania bara kama vile kukikopesha maneno mbalimbali, kwa mfano: shule, hela n.k.

Maneno machache

hujambo? – sijambo Wie geht es dir? – Mir geht es gut.
jambo Hallo!
ndiyo ja
hapana nein
mgeni Gast, Fremder
rafiki Freund
karibu Willkommen!
kwa heri Auf Wiedersehen!
asante Danke!
asante sana Vielen Dank!
safari Reise
ninakupenda Ich liebe dich.
hatari Gefahr
daktari Doktor
polepole langsam
Afya! (wakati wa kunywa na mwingine) Prost!
kijiji Dorf
mji Stadt

Tanbihi

Viungo vya nje

Tags:

Kijerumani kama lugha ya kitaifaKijerumani Lugha inayofundishwaKijerumani Maneno machacheKijerumani TanbihiKijerumani Viungo vya njeKijerumaniJamiiKidachiKigermanikLughaLugha za Kihindi-KiulayaMagharibi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

KinyongaSimuShambaTashbihaVivumishi vya idadiKitenzi kikuu kisaidiziKitenziTenziIstanbulUingerezaChristina ShushoRuge MutahabaKishazi tegemeziPentekosteKiunguliaKinembe (anatomia)Nomino za jumlaChawaJoseph ButikuNamba tasaSamakiJinsiaUhakiki wa fasihi simuliziWikipedia ya KiswahiliYvonne Chaka ChakaUchimbaji wa madini nchini TanzaniaMr. BlueMajeshi ya Ulinzi ya KenyaArusha (mji)Orodha ya makabila ya TanzaniaMaeneo ya Kihistoria ya Kitaifa ya TanzaniaLigi ya Mabingwa AfrikaKimondo cha MboziJakaya KikweteKanisa KatolikiUainishaji wa kisayansiMisemoVidonda vya tumboLatitudoNgano (hadithi)AfyaNusuirabuDagaaRaiaBarua rasmiLil WayneOrodha ya Watakatifu wa AfrikaMnyamaHisiaMlo kamiliZuchuJohn MagufuliMkoa wa ManyaraMkoa wa LindiMadiniHuduma ya ujumbe mfupiMaishaMgawanyo wa AfrikaLahaja za KiswahiliUrusiUpendoWayahudiNdoaUsawa (hisabati)Hifadhi ya SerengetiStadi za lughaNjia ya MachoziMuda sanifu wa duniaUkwapi na utaoShangaziOrodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifaIsimujamii🡆 More