Picha Takatifu

Picha takatifu (pia ikona kutoka Kigiriki εἰκών, eikōn picha kwa kupitia Kiingereza icon) kwa kawaida ni mchoro unaoheshimiwa kidini hasa katika Ukristo wa Mashariki lakini pia katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo wa Magharibi, kama vile Kanisa la Kilatini.

Picha Takatifu
Ngazi ya Kupanda kwa Mungu ni picha ya karne ya 12 inayoonyesha wamonaki wakipanda kwa Yesu mbinguni, Monasteri ya Mt. Katerina, Sinai.
Picha Takatifu
Picha ya Kirusi ya Utatu Mtakatifu iliyoiga ile maarufu ya Andrei Rublev.
Picha Takatifu
"Ushindi wa Imani Sahihi" dhidi ya wapingapicha chini ya malkia Theodora na mwanae kaisari Mikaeli III. Picha takatifu ya karne ya 14 mwishoni – 15 mwanzoni.
Picha Takatifu
Picha ya Mt. Nikolasi iliyochongwa jiweni kati ya karne ya 12 na karne ya 15, Radomysl Castle, Ukraine

Mara nyingi picha hizo zinamhusu Yesu, Bikira Maria, watakatifu wengine, malaika na msalaba.

"Sanaa ya Kikristo" inatajwa kwanza kati ya karne ya 2 na karne ya 3 katika maandishi ya Tertuliani (160 hivi - 220) na Klemens wa Aleksandria (150 hivi - 212).

Matumizi ya picha hizo yalipingwa na baadhi ya Wakristo, hasa wa mashariki, baada ya Uislamu kutokea na kuenea katika maeneo yao. Hapo kaisari Leo III wa dola la Roma Mashariki alikataza picha hizo ili kujilinganisha na Waislamu na kujenga uhusiano mzuri nao.

Kumbe wamonaki na Wakristo wengine wengi walipinga katazo hilo. Ndio mwanzo wa mabishano makubwa yasiyoishia katika hoja na maandishi, bali yalichukua uhai wa watu, hasa waliodhulumiwa na serikali.

Hatimaye Mtaguso wa pili wa Nisea (787) ulithibitisha uhalali wa picha hizo na wa heshima ambazo zinapewa, kama ulivyotetewa hasa na mtakatifu Mwarabu Yohane wa Damasko.

Pamoja na kwamba picha takatifu zinasema na mioyo ya waamini wanyofu, mara nyingi utaalamu wa ikonografia unahitajika hasa katika kufafanua picha takatifu za Ukristo wa Mashariki, kwa kuwa hizo hazilengi kuiga sura halisi zinavyoonekana na macho, bali kudokeza mafumbo ya imani ili kuona yasiyoonekana.

Tanbihi

Marejeo

  • Beckwith, John, Early Christian and Byzantine Art, Penguin History of Art (now Yale), 2nd edn. 1979, ISBN 0-14-056033-5

Marejeo mengine

Viungo vya nje

Picha Takatifu 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:


Waorthodoksi

Wakatoliki

Picha

Picha Takatifu  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Picha takatifu kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Picha Takatifu TanbihiPicha Takatifu MarejeoPicha Takatifu Marejeo menginePicha Takatifu Viungo vya njePicha TakatifuDiniKanisa la KilatiniKigirikiKiingerezaMadhehebuMchoroPichaUkristo wa MagharibiUkristo wa Mashariki

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

UajemiUjerumaniMimba za utotoniOrodha ya Marais wa ZanzibarBawasiriNuktambiliShahawaJumuiya ya Afrika MasharikiVielezi vya mahaliDaktariBonde la Ufa la Afrika ya MasharikiHekaya za AbunuwasiKamusi ya Kiswahili sanifuPasifikiMazingiraMsitu wa AmazonUlimwenguSiafuKomaMr. BlueAmina ChifupaHadithiFasihiArusha (mji)NandyHistoria ya KiswahiliJichoRicardo KakaMfumo wa upumuajiGongolambotoBiblia ya KikristoSayansi ya jamiiLiverpool F.C.Mapambano ya uhuru TanganyikaMuhammadMkoa wa SingidaBenderaClatous ChamaKenyaMajeshi ya Ulinzi ya KenyaUaMasafa ya mawimbiShambaKimara (Ubungo)Maambukizi nyemeleziHarmonizeJinsiaMikoa ya TanzaniaMbaraka MwinsheheKinyongaSanaa za maoneshoMbeya (mji)MzeituniNyati wa AfrikaMfumo wa JuaTanzaniaMbwana SamattaTupac ShakurHussein Ali MwinyiNevaKimeng'enyaNdiziWagogoUzazi wa mpango kwa njia asiliaTume ya Taifa ya UchaguziKihusishiSkeliMkoa wa Dodoma🡆 More