Uainishaji Wa Kisayansi

Uainishaji wa kisayansi (ing.

Inaweza kuitwa pia taksonomia.

Uainishaji Wa Kisayansi
Ngazi za uainishaji katika biolojia; ngazi ndogo za kati hazionyeshwi.

Tangu muda mrefu watu walitambua ya kwamba wanyama au mimea mbalimbali wanafanana kati yao kwa namna moja au nyingine. Wataalamu walijaribu kupanga aina hizo kwa vikundi vyenye tabia za pamoja. Carolus Linnaeus alianza kuzipanga kwa muundo ulioeleweka kulingana na tabia za maumbile yao.

Mfumo wa Linnaeus uliendelezwa baadaye kulingana na nadharia ya Charles Darwin inayoona ya kwamba spishi mbalimbali huwa na chanzo cha pamoja, kwa hiyo inawezekana kupanga uhai wote kama mti yenye matawi makubwa, tena madogo yanayotoka kwenye makubwa.

Ujuzi wa kisasa kutokana na utafiti wa DNA ndani ya seli za viumbehai unaendelea kuongeza ujuzi wetu kwa hiyo katika mengi uainishaji ni utaalamu unaozidi kubadilika.

Majina ya Kisayansi

Uainishaji Wa Kisayansi 
Carl Linnaeus, anayejulikana kama baba wa uainishaji wa kisayansi.

Kila spishi ya viumbehai inapewa jina la kisayansi lenye maneno mawili kufuatana na muundo wa uainishaji. Jina la Kisayansi linaanza kwa kutaja jenasi inayoandikwa kwa herufi kubwa, halafu neno la pili kama sehemu maalumu ya jina la spishi ile. Maneno hayo huandikwa kwa herufi za italiki. Kwa mabano hufuata jina la mtaalamu wa spishi pamoja na mwaka alioandika maelezo yake.

Kwa mfano paka anaitwa Felis silvestris (Linnaeus, 1758) na spishi hii inajumlisha paka wa porini na paka wa nyumbani.

  • Felis ni jina la jenasi. Jenasi huandikwa kwa herufi kubwa.
  • "silvestris" ni sehemu ya pili ya neno; linasema "wa msituni" kwa sababu inaaminiwa ya kwamba asili ya paka hizi zote ni aina ya paka wa porini wa Asia, Ulaya na Afrika Kaskazini.

Paka wa nyumbani anayefugwa na watu anatazamwa kama nususpishi, na nususpishi hii inaweza kutofautishwa kwa kuongeza neno la tatu "catus" kuwa "Felis silvestris catus". Hili ni jina la nususpishi ya paka wanaofugwa na watu. Nususpishi hii ina aina nyingi ndani yake, kutokana na ufugaji na uteuzi lakini zote zimo ndani ya nususpishi ileile.

Katika mabano lipo jina la mtaalamu aliyeeleza spishi hii mara ya kwanza kwa namna ya kisayansi pamoja na mwaka alipoandika. Katika mfano wa paka ni Carolus Linnaeus anayefupishwa mara nyingi kama "L.". Aliandika kitabu chake mwaka 1728.

Umbo la majina katika uinishaji

Katika uainishaji wataalamu wamepatana jinsi ya kutumia majina kwa ngazi mablimbali. Umbo la majina haya hufuata sarufi ya Kilatini.

Ngazi Mimea
(planta)
Mwani
(algae)
Uyoga
(fungi)
Wanyama
(animalia)
Faila -phyta -mycota
Nusufaila -phytina -mycotina
Ngeli -opsida -phyceae -mycetes
Nusungeli -idae -phycidae -mycetidae
Oda ya juu -anae
Oda -ales
Nusuoda -ineae
Familia ya juu -acea -oidea
Familia -aceae -idae
Nusufamilia -oideae -inae
Kabila -eae -ini
Nusukabila -inae -ina
Uainishaji Wa Kisayansi  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uainishaji wa kisayansi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

BiolojiaIng.MimeaViumbehaiWanyamaWataalamuen:taxonomy (biology)simple:biological classification

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Hekalu la YerusalemuMaziwa ya mamaAngahewaMuhimbiliGoba (Ubungo)MarekaniViwakilishiAfrika ya MasharikiNgw'anamalundiUenezi wa KiswahiliPombooOrodha ya kampuni za TanzaniaFasihiOrodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watuNomino za wingiKupatwa kwa JuaTawahudiMohamed HusseiniStadi za lughaIsimuOrodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaViwanja vya Afrika (Kwa Ukubwa)Mafua ya kawaidaMaajabu ya duniaTabianchiKaswendeArsenal FCIniChristina ShushoRushwaWajitaMjasiriamaliLugha rasmiMatiniMatumizi ya lugha ya KiswahiliMobutu Sese SekoAkiliMziziBenki ya DuniaMariooWilaya ya IlalaKarafuuMkoa wa MwanzaHistoria ya ZanzibarUtamaduni wa KitanzaniaMpwaOrodha ya visiwa vya TanzaniaBinadamuMweziUkimwiSitiariKalenda ya KiislamuMabiboMazungumzoMkoa wa NjombeBungeMungu ibariki AfrikaMlongeUmoja wa MataifaKatibaMeena AllyMaudhuiMunguCristiano RonaldoNyegeMoyoSalim Ahmed SalimMsamiatiAla ya muzikiMohamed HusseinOrodha ya Marais wa TanzaniaMatumizi ya LughaHeshima🡆 More