Karafuu

Karafuu (kutoka Kiarabu قَرَنْفُل qaranful) ni matumba (macho ya maua) makavu ya mikarafuu ambayo ni miti ya familia ya Myrtaceae.

Karafuu
Karafuu kadhaa
Karafuu
Karafuu ikiangaliwa kwa karibu
Karafuu
Maua kwenye mkarafuu
Karafuu
Karafuu tayari kukauka

Karafuu hutumiwa kama kiungo cha chakula na chanzo cha mafuta yenye harufu inayopendwa na watu wengi.

Asili ya mti na pia matumizi ya matumba ni visiwa vya Indonesia. Katika karne ya 19 mikarafuu ilipelekwa Unguja na Pemba hasa na mtawala wa Omani na kuanzisha uzalishaji mkubwa saa wa karafuu kwenye visiwa hivi.

Matumizi

Karafuu hutumiwa katika upishi wa nchi nyingi za Asia, Afrika, Ulaya na hata Amerika. Hutumiwa katika kupika nyama, curry na michuzi mbalimbali pamoja na kupika matunda pamoja na vinywaji. Ni kiungo cha lazima kwenye pilau.

Hutafunwa pia mdomoni kuboresha harufu ya pumzi.

Kutafuna karafuu ni dawa ya kupunguza maumivu ya meno.

Nchini Indonesia sigara huungwa na mafuta ya karafuu.

Historia

Karafuu zilifanyiwa biashara tangu kale. Kuna ushuhuda wa karafuu katika chombo kilichopatikana nchini Syria kilichogunduliwa kuachwa huko mnamo mwaka 1721 KK.

Kuna taarifa ya kwamba mtawala nchini China alitaka watu wanaotaka kuongea naye watafune karafuu ili wawe na pumzi ya kupendeza.

Katika karne ya 17 karafuu ilikuwa kati ya vivutio vya kiuchumi vilivyoleta Uholanzi kuanzisha makoloni yake kwenye visiwa vya Indonesia.

Katika karne ya 18 Mfaransa Pierre Poivre alifaulu kuiba miche ya mikarafuu na kuipeleka Morisi ambako Wafaransa walianzisha kilimo hicho.

Soko la karafuu lilikua duniani na hii ilikuwa changamoto ya Sultani wa Omani kupeleka miti hiyo Unguja na Pemba iliyoendelea kuwa nchi ya kuzalisha karafuu nyingi zaidi duniani na kuunda utajiri wa Zanzibar ilhali kilimo hicho kilichochangia pia katika biashara ya watumwa waliotumiwa kuzalisha zao hili katika karne ya 19.

Mapato ya karafuu yalimsababisha Said bin Sultani kuhamisha makao makuu yake Unguja na baada ya kifo chake Usultani wa Zanzibar ulianzishwa kama nchi ya pekee na Omani.

Tanbihi

Marejeo

Karafuu 
WikiMedia Commons

Tags:

Karafuu MatumiziKarafuu HistoriaKarafuu TanbihiKarafuu MarejeoKarafuuFamilia (biolojia)KiarabuMachoMauaMitiMkarafuu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

StafeliMohamed HusseiniZuhuraUkwapi na utaoOrodha ya majimbo ya MarekaniUshairiBata MzingaUwanja wa Taifa (Tanzania)BaraLahaja za KiswahiliUgaidiHerufiMizimuZabibuAsili ya KiswahiliNomino za jumlaKhadija KopaOrodha ya makabila ya TanzaniaWilaya ya KigamboniKalenda ya KiislamuMkoa wa NjombeDamuVivumishi vya idadiNomino za dhahaniaIdi AminAla ya muzikiMaana ya maishaSaratani ya mlango wa kizaziHadithiTeknolojiaOrodha ya matajiri wakubwa WaafrikaMamba (mnyama)SadakaMuundo wa inshaMkoa wa Dar es SalaamAfrikaMsamahaViwakilishi vya idadiSintaksiUturukiJipuLenziUandishi wa barua ya simuUandishiKinyongaHistoria ya WapareTabiaAbedi Amani KarumeKilimanjaro (volkeno)Hekaya za AbunuwasiKenyaHistoria ya UislamuDhamiraMatumizi ya LughaKanisaMaradhi ya zinaaImaniKifua kikuuVirusi vya UKIMWIZama za MaweUhuru wa TanganyikaTulia AcksonKamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniP. FunkMimba kuharibikaMziziMichezo ya watoto🡆 More