Jipu

Jipu (kwa Kiingereza: boil au furuncle, yaani mwizi mdogo, kutoka neno la Kilatini fur, mwizi) ni tatizo la ngozi linalotokana na maambukizi ya kina ya folikuliti au maambukizi ya folikoli za nywele za jasho; mara nyingi unasababishwa na bakteria Stafilokokasi aureasi, ambayo husababisha kuvimba kwa eneo chungu lililo juu ya ngozi kutokana na mkusanyiko wa usaha na tishu mfu.

Jipu
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyDermatology Edit this on Wikidata
ICD-10L02.
ICD-9680.9
DiseasesDB29434
MeSHD005667

Majipu yakijikusanya huitwa kimeta.

Dalili na ishara

Majipu ni vijivimbe vyekundu, ambavyo hujaa na usaha ulioko karibu na vinyweleo ambavyo ni laini, vya moto, na vinanavyouma sana. Yana ukubwa mbalimbali, kuanzia punje hadi ukubwa wa mpira wa golfu. Sehemu ya njano au nyeupe katikati ya uvimbe inaweza kuonekana wakati jipu likiwa tayari kutoa au kutokwa na usaha.

Katika maambukizi makali, mtu anaweza kuhisi homa, kuvimba tezi au mtoki, pamoja na uchovu.

Jipu linalojirudia mara kwa mara linaitwa ngozi-jipu.

Sababu

Kwa kawaida bakteria, kama vile stafilokoki, ndio husababisha jipu kutokea kwenye ngozi. Ukoloni wa bakteria huanza katika vinyweleo na inaweza kusababisha seluli ya chini ya ngozi na kuvimba. Zaidi ya hayo, maiasisi inayosababishwa na wadudu wa kuruka aina ya Tumbu katika Afrika, kawaida huonesha majipu.

Sababu hatarishi za ngozi-jipu ni pamoja na bakteria katika tundu la pua, ugonjwa wa kisukari, fetma, neoplasmi s lymphoproliferative, utapiamlo, na matumizi ya madawa yanayokandamiza kingamwili.

Matatizo yanayojitokeza

Matatizo kawaida yanayotokana na kuambukizwa na majipu ni makovu na maambukizi au usaha wa ngozi, uti wa mgongo, ubongo, figo na viungo vingine. Maambukizi pia huweza kuenea hadi kwenye mfumo wa damu (sepsisi) na kuwa tishio kwa uhai.

Matibabu

Majipu yote lazima yafyonzwe ili kupona. Kunyonywa kunawezekana kwa kutumia kitambaa kilicholowa kwenye maji moto yenye kutiwa chumvi. Kuosha pamoja na kufunika jipu na krimu ya antibiotiki au mafuta ya antiseptiki (kwa jina maarufu tea tree oil) na kufunga bendeji kunasababisha kupona kwa haraka. Majipu hayastahili kufinywa au kutobolewa bila idhini ya daktari au muuguzi yeyote, kwani kunaweza kusababisha maambukizi mengine.

Katika hatari ya kutosababisha matatizo makubwa ni lazima majipu yakatwe au yafyonzwe na daktari. Hii ni pamoja na majipu makubwa yanayokaa zaidi ya wiki mbili, ama yale yanayopatikana katikati ya uso au kwenye uti wa mgongo.

Tiba ya antibiotiki linahimizwa haswa kwa kupigana na majipu makubwa yanayopatikana kwenye sehemu nyeti kama vile pua na ndani ya masikio.

Tanbihi

Viungo vya nje

Jipu 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
Jipu  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jipu kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Jipu Dalili na isharaJipu SababuJipu Matatizo yanayojitokezaJipu MatibabuJipu TanbihiJipu Viungo vya njeJipuBakteriaJashoKiingerezaKilatiniMaambukiziNenoNgoziNywele

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

VolkenoWenguUajemiBloguUjerumaniSitiariHaki za binadamuBahari ya HindiUfupishoVihisishiTendo la ndoaVita Kuu ya Pili ya DuniaKajala MasanjaHadithiUjuziKimondo cha MboziMshororoUkabailaVita vya KageraUchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2020WakingaAfrikaSteven KanumbaHistoria ya BurundiKinjikitile NgwaleNdovuPijiniNyangumiAmfibiaAli Hassan MwinyiUfilipinoKinyongaMjasiriamaliAdolf HitlerMobutu Sese SekoMsitu wa AmazonKishazi tegemeziLigi ya Mabingwa UlayaUmoja wa MataifaBenjamin MkapaOrodha ya Magavana wa TanganyikaInsha ya kisanaaMaktabaJakaya KikweteSensaMunguOrodha ya vyama vya siasa TanzaniaMajigamboTeknolojiaHuzuniOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoOrodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaUongoziUwanja wa Taifa (Tanzania)Vivumishi vya pekeeMkoa wa SimiyuNg'ombeMr. BlueWachaggaVita ya Maji MajiAlama ya barabaraniNadhariaKaswendeMafua ya kawaidaMfumo wa homoniRisalaStephane Aziz KiMkutano wa Berlin wa 1885Hifadhi ya NgorongoroNdege (mnyama)Sisimizi🡆 More