Nuhu

Nuhu anajulikana na kuheshimiwa katika dini ya Uyahudi, Ukristo na Uislamu kama mfano wa mwadilifu aliyeokolewa na Mungu katika safina wakati wa gharika kuu.

Kadiri ya Biblia aliishi huko Mesopotamia.

Nuhu
Sadaka ya Nuhu ilivyochorwa na Daniel Maclise.

Jina lake (kwa Kiebrania נח Noah, kwa Kiarabu نوح Nuhu) linatafsiriwa na Kitabu cha Mwanzo Mfariji, lakini maana ya hakika zaidi ni Anayeendeleza ubinadamu baada ya gharika.

Anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 18 Novemba.

Katika Biblia

Nuhu 
Meli ya Nuhu, Zubdetü't-Tevarih. Kulingana na wasomi wa huria, hadithi ya mafuriko ya Gilgamesh imekopwa kutoka kwa Wababeli na kutafsiriwa tena katika Torati na katika Quran.

Mwa 6:5-9:17 inatufundisha kwamba Mungu anachukizwa na dhambi, hivyo anataka kuondoa maovu duniani ili nchi impendeze kama alivyokusudia alipoiumba. Kwa ajili hiyo zamani za Nuhu alileta maji yafunike dunia na kuzamisha waovu. Lakini alisalimisha waadilifu katika safina kubwa ya kutosha, halafu akafunga nao agano thabiti (Eb 11:7).

Kadiri ya Mtume Petro maji yanayokusudiwa kutakasa dunia yote ni yale ya ubatizo (1Pet 3:17-22), na safina ambayo iokoe watu ni Kanisa, ambalo kadiri ya Agano Jipya ni la lazima kwa wokovu kama vile ubatizo unaotuingiza ndani yake.

Uso wa nchi ulipokwishatakaswa na maji njiwa akarukaruka akachuma tawi la mzeituni unaozaa matunda ya kutengenezea mafuta.

Njiwa akaonekana tena juu ya maji siku ya ubatizo wa Yesu ambapo alipakwa Roho Mtakatifu na kuyatia maji nguvu ya kutakasa watu (Mk 1:9-11; Tito 3:3-7). Maji na mafuta ndiyo mwanzo mpya kwa binadamu.

Mara alipotoka safinani Nuhu alimtolea Mungu sadaka iliyompendeza hata akaahidi hataangamiza tena binadamu kila anapostahili.

Sadaka hiyo ni mfano wa ile ya Yesu msalabani, inayoadhimishwa katika ekaristi, ikituondolea adhabu nyingi na kutuletea huruma ya Mungu, yaani nafasi na neema ya kutubu (Tito 2:11-14). Hatimaye kutakuwa na hukumu itakayobagua waadilifu na waovu kama siku za Nuhu (Math 24:37-41).

Tazama pia

Viungo vya nje

Nuhu 
Wiki Commons ina media kuhusu:
Nuhu  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nuhu kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

BibliaDiniMesopotamiaMunguSafinaUislamuUkristoUyahudi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Taswira katika fasihiNgw'anamalundiMaeneo ya Kihistoria ya Kitaifa ya TanzaniaSemiBustaniYombo VitukaOrodha ya miji ya TanzaniaMichezo ya watotoMaktabaKigoma-UjijiFasihi simuliziPembe za ndovuKichochoHistoria ya UislamuMkoa wa LindiZiwa NatronMoscowMakabila ya IsraeliOrodha ya kampuni za TanzaniaMkoa wa IringaRuge MutahabaUajemiDiamond PlatnumzWanyakyusaMnyoo-matumbo MkubwaWokovuMamelodi Sundowns F.C.MsituMbwana SamattaTamathali za semiMazungumzoMarekaniUgirikiKunguruKamusiMwanzoKadhiKamusi ya Kiswahili sanifuMkatabaOrodha ya Maspika wa Bunge la TanzaniaIniUingerezaNdoaMfumo wa upumuajiJumapiliMaana ya maishaSayariMajira ya baridiBarua pepeAmani Abeid KarumeLakabuKifaruWitoBiashara ya watumwaMandhariNafsiVielezi vya idadiMwezi (wakati)Hekalu la YerusalemuMkoa wa MtwaraDar es SalaamJumuiya ya Afrika MasharikiNyegeOrodha ya Marais wa KenyaMatumizi ya lugha ya KiswahiliVieleziMlipuko wa virusi vya corona 2019-20BaruaMaudhuiSaratani ya mlango wa kizaziRayvannyUmojaJina🡆 More