Papa

Papa (neno la mkopo kutoka Kilatini lakini lenye asili ya Kigiriki, πάππας, pappas, jina ambalo mtoto anamuitia baba yake)ni cheo cha kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani kote.

Kwa samaki anayeitwa kwa Kiswahili "papa" tazama papa (samaki)

Cheo hicho kinategemea kile cha askofu wa Roma.

Papa
Papa Pius IX, alishika cheo hicho kwa muda mrefu kuliko wote (1846-1878).
Hii ni sehemu ya mfululizo kuhusu
Kanisa Katoliki
Papa
Imani

Umoja wa Mungu
Utatu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu)
Umwilisho Maisha ya Yesu
Msalaba Ufufuko Kupaa
Historia ya Wokovu Ufunuo
Biblia Mapokeo Ualimu Dogma
Neema Dhambi Wokovu Sakramenti
Watakatifu Bikira Maria

Muundo

Papa: Fransisko
Urika wa maaskofu Mitaguso mikuu
Kundi la Makardinali
Kanisa la Kilatini
Makanisa Katoliki ya Mashariki

Historia

Historia Ukristo
Ukatoliki Mlolongo wa Kitume
Sifa nne za Kanisa Utetezi Ekumeni
Maisha ya kiroho Amri Kumi Utawa
Sala Falsafa Teolojia
Muziki Sanaa Sayansi

Ibada

Liturujia Mwaka wa Kanisa
Ekaristi Liturujia ya Vipindi

Mapokeo ya liturujia

Liturujia ya Kilatini (Roma Liturujia ya Trento Milano Toledo Braga Lyon Canterbury)
Liturujia ya Armenia Liturujia ya Misri
Liturujia ya Ugiriki Liturujia ya Antiokia
Liturujia ya Mesopotamia

Asili

Kiasili neno la Kilatini "Papa" linamaanisha "Baba", nalo likawa cheo kutokana na nia ya kumtaja askofu wa Roma kwa heshima ya pekee. Msingi wa heshima hiyo ni imani ya Wakatoliki kuwa askofu wa Roma ni mwandamizi wa Petro, mkuu wa mitume wa Yesu.

Wakatoliki huamini ya kwamba Petro alipewa na Yesu kazi ya kuongoza Kanisa lote kwa niaba yake na ya kwamba jukumu hilo linaendelea kati ya waandamizi wa Petro kwenye kiti cha askofu wa Roma ambacho kwa heshima kinaitwa Ukulu mtakatifu.

Historia

Upapa ni kati ya vyeo vya zamani zaidi duniani na umeathiri sana historia ya binadamu kwa miaka karibu 2000.Athari hiyo iliweza kuwa nzuri au mbaya, kadiri ya matendo ya mhusika.

Kwa muda mrefu mamlaka ya Papa upande wa siasa, hasa juu ya mikoa ya Italia ya Kati, ilisababisha nchi nyingine na koo tajiri za Roma zijiingize katika uchaguzi ili kupitisha watu wao, hata wasiofaa. Upande mwingine, Mapapa waliathiriwa na utamaduni na mazingira ya nyakati zao, hasa tapo la Renaissance, kiasi cha kuzama katika anasa.

Baada ya Dola la Papa kutekwa na Ufalme wa Italia (1860-1870), Mapapa wameweza kushughulikia zaidi mambo ya kiroho na kujitokeza kwa ubora.Kwa miaka ya karibuni inatosha kumfikiria Papa Yohane Paulo II na mchango wake katika kuangusha ukomunisti katika Ulaya Mashariki.

Majina ya mapapa

Papa 
Sahihi ya Papa Fransisko.

Papa huchaguliwa na makardinali wa Kanisa Katoliki baada ya mtangulizi wake kufa au kung'atuka. Baada ya kuchaguliwa papa mpya anaweza akajipatia jina jipya. Tangu tarehe 13 Machi 2013 ni Papa Fransisko, ambaye awali aliitwa Jorge Mario Bergoglio, kutoka Argentina.

Majina ya mapapa wengine wa Kanisa Katoliki yanapatikana katika orodha ya mapapa.

Mkuu wa Vatikano

Papa ni pia mkuu wa nchi huru ya Mji wa Vatikano iliyopo ndani ya mji wa Roma (ambao ni mji mkuu wa Italia).

Cheo cha "Papa" penginepo

Cheo cha Papa hutumiwa pia na baadhi ya madhehebu mengine ya Kikristo kwa viongozi wao, hasa kwa mkuu wa Kanisa la Kikopti huko Misri.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Marejeo mengine

Viungo vya nje

Papa 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
Papa  Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Papa AsiliPapa HistoriaPapa Majina ya mapapaPapa Mkuu wa VatikanoPapa Cheo cha penginepoPapa Tazama piaPapa TanbihiPapa MarejeoPapa Marejeo menginePapa Viungo vya njePapaAsiliAskofuBabaCheoDunianiJinaKanisa KatolikiKigirikiKilatiniKiongoziMtotoRoma

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

JuxMalariaOrodha ya milima ya AfrikaVielezi vya wakatiRidhiwani Jakaya KikweteMakaburuDawa za mfadhaikoWimbo wa Jumuiya ya Afrika MasharikiMzunguko wa Bahari NyekunduUvimbe wa koromeo usababishwao na streptokokiDoto Mashaka BitekoBarcelona F.C.Mtakatifu PauloSoko la watumwaKishazi tegemeziMashineMwanzo (Biblia)Google ChromeMbwana SamattaMbeyaBaraza la Wawakilishi wa ZanzibarUkimwiMendeDiniPaul MakondaNazi (tunda)TovutiTahajiaKibwagizoNabii EliyaNyukiMeta PlatformsNyangumiKamusi ya Kiswahili sanifuPichaHenokoItifakiJogooMofolojiaDemokrasia ya moja kwa mojaMaghaniOrodha ya miji ya TanzaniaKipandausoEstrojeniKinywajiRupiaMsamiatiFutiChuo Kikuu cha Dar es SalaamUenezi wa KiswahiliKodi (ushuru)Usafi wa mazingiraNominoJamhuri ya Kidemokrasia ya KongoAsili ya KiswahiliLionel MessiKasisiAli Hassan MwinyiMichoro ya KondoaUchumiMV BukobaPasaka ya KikristoWanu Hafidh AmeirBaruaPijini na krioliKilimanjaro (volkeno)NduniMatiniWasukumaUgonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofunganaUtoaji mimbaMaarifaManchester United F.C.Tetekuwanga🡆 More