Waziri Mkuu ni cheo cha kiongozi wa serikali.
Neno lasema ya kwamba yeye ni mkubwa kati ya mawaziri wa serikali. Madaraka yake hutegemea na katiba ya nchi. Kwa kawaida cheo hiki kipo katika nchi ambako mkuu wa dola ambaye mara nyingi huitwa rais au pia mfalme (malkia) hashughuliki mwenyewe mambo ya serikali.
Lugha inaweza kuwa tofauti kati ya nchi na nchi. Anaweza kuitwa pia "Rais wa Mawaziri", "Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mawaziri" au "Chansella".
Kuna hasa aina mbili za mawaziri wakuu kufuatana na katiba za nchi mbalimbali:
Katiba inaweza kusema ya kwamba rais ni huru kumchagua waziri mkuu hata bila kujali idadi ya wabunge wake bungeni. Katika mfumo huu waziri mkuu ni zaidi kama meneja wa kazi ya serikali.
Lakini kuna mifano ambako katiba inampa rais na pia waziri mkuu kila mmoja madaraka yake. Kwa mfano rais kusimamia mambo ya jeshi na usalama pamoja na siasa ya nje na waziri mkuu kusimamia siasa ya ndani na ya kiuchumi. Hapo waziri mkuu atakuwa na uhuru zaidi mbele mkubwa wake.
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Waziri mkuu, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.