Kimondo Cha Mbozi

9°06′28″S 33°02′14″E / 9.10778°S 33.03722°E / -9.10778; 33.03722


Kimondo Cha Mbozi
Kimondo cha Mbozi

Kimondo cha Mbozi ni kimondo ambacho kilianguka kutoka anga-nje karibu na mji wa Vwawa. Kinakadiriwa kuwa na uzito wa takriban tani 16, kilianguka katika kilima cha Mlenje, wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe, Tanzania.

Kipo kati ya vimondo vizito 10 vinavyojulikana duniani. Kina urefu wa mita 3.3, upana wa mita 1.63 na kimo cha mita 1.22.

Kina maumbile maalum tofauti na vimondo vingine vinavyopatikana ulimwenguni kwa kuwa hiki ni hasa cha chuma. Chuma ni 90.45%, nikeli 8,69%, sulfuri 0,01% na fosfori 0,11% ya masi yake. Ndani yake vipande vidogo vya silikati vinapatikana.

Wenyeji wa eneo walijua kimondo hiki tangu muda mrefu; kilielezwa kisayansi mara ya kwanza mwaka 1930 na wakati ule hapakuwa na dalili za kasoko; kwa hiyo inawezekana ya kwamba ama kilifika kwenye uso wa Dunia kwa pembe butu sana na kuvingirika hadi kukaa au muda wa kugonga uso wa dunia ni mrefu sana hadi dalili zote za kasoko asilia zilipotea tayari kutokana na mmomonyoko.

Tanbihi

Viungo vya Nje

Tags:

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

MofimuArudhiKamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniAzimio la Kimataifa juu ya Haki za BinadamuDhima ya fasihi katika maishaRiwayaUvimbe wa koromeo usababishwao na streptokokiNdoa katika UislamuShahawaWashambaaArsenal FCTanganyikaSumakuAmfibiaFasihi simuliziNishatiMalawiChepeKoloniNimoniaOrodha ya Marais wa UgandaMethaliVasco da GamaWawanjiHistoria ya ZanzibarPunyetoSemantikiMartin LutherMziziVieleziUpendoMisemoMaskiniDaudi (Biblia)Kitabu cha Yoshua bin SiraKidole cha kati cha kandoMahindiUjerumaniOrodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watuRose MhandoMtaalaKataSanaa za maoneshoP. FunkWordPressMajigamboRoho MtakatifuMfumo wa mzunguko wa damuAdhuhuriKiimboMahakamaKipindupinduOrodha ya nchi za AfrikaMbwa-mwitu DhahabuTausiWanyama wa nyumbaniNdiziUsawa (hisabati)WahayaNomino za pekeeAbrahamuMeta PlatformsIniTungo sentensiVokaliJangwaNambaLongitudoTwigaBarua pepeWema SepetuMarekaniOlduvai GorgeYesuManchester United F.C.🡆 More