Saratani Ya Mapafu

Saratani ya mapafu ni ugonjwa unaohusishwa na ukuaji wa seli katika tishu za mapafu.

Tishu hii isipotibiwa, inaweza kuenea kwa njia inayoitwa metastasisi kwa tishu zilizokaribu au kwa mwili. Saratani zinazoanzia kwa mapafu, ziitwazo saratani za kwanza, ni kasinomasi zinazotoka kwa seli za epitheliumu. Aina kuu za saratani ni kasinoma ya mapafu ya seli ndogo (KMSN), pia huitwa saratani ya seli ya oat, na kasinoma ya mapafu ya seli kubwa (KMSK). Dalili inayojulikana sana ni kukohoa (pamoja na kukohoa damu), kupoteza uzito na upungufu wa pumzi.

Lung cancer
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyOncology, pulmonology Edit this on Wikidata
ICD-10C33.-C34.
ICD-9162
DiseasesDB7616
MedlinePlus007194
eMedicinemed/1333 med/1336emerg/335radio/807radio/405radio/406
MeSHD002283

Kisababishi kikuu cha saratani ya mapafu ni kuathiriwa na moshi wa tumbaku, unaosababisha asilimia 80–90 ya saratani. Wasiovuta huchangia visa hivi kwa asilimia 10-15– na mara nyingi huhusishwa na muungano wa masuala ya kijenetiki, gesi ya radoni, asbesto, na uchafuzi wa hewa pamoja na moshi kutoka kwa anayevuta sigara. Saratani ya mapafu inaweza kuonekana kwa rediografu ya kifua na tomografi ya kompyuta (ukaguzi wa CT). utambuzi hudhibitishwa kwa biopsi ambao hutekelezwa kwa bronkoskopi au mwongozo wa CT. Matibabu na matokeo ya muda mrefu hulingana na aina ya saratani, hatua (kiwango cha uenezi), na afya kwa jumla ya mtu, ikipimwa kwa hali ya utendakazi.

Matibabu ya kawaida ni pamoja na upasuaji, kemotherapi, na radiotherapi. KMSK wakati mwingine hutibiwa na upasuaji, ilhali KMSN huwa bora kwa kemotherapi na radiotherapi. Kwa jumla, asilimia 15 ya waliopatikana na saratani nchini Marekani wana kuishi miaka mitano. Ulimwenguni kote, saratani ya mapafu ni kisababishi cha kawaida cha vifo vinavyohusiana na saratani kwa wanaume na wanawake, na husababisha Vifo milioni 1.38 kwa mwaka, kufikia 2008.

Ishara na dalili

Ishara na dalili zinazoashiria saratani ya mapafu ni pamoja na:

  • Dalili za upumuaji: kukohoa, kukohoa damu, kukoroma au upungufu wa pumzi
  • Dalili za kimfumo: kupoteza uzito, homa, kupindika kwa kucha za vidole, au uchovu
  • Dalili kwa sababu ya kugandamizwa : maumivu ya kifua, maumivu ya mifupa, kuzibwa kwa vena kubwa, matatizo ya kumeza

Ikiwa saratani itatokea katika njia ya hewa, inaweza kuziba mpito wa hewa, na kusababisha matatizo ya kupumua. Uzibaji unaweza kusababisha mkusanyiko wa unyesaji nyuma ya kizibo, na kuwa nimonia.

Kulingana na aina ya tyuma, inayoitwa fenomena ya paraneoplastiki inaweza kuleta magonjwa. Katika saratani ya mapafu, nimonia zinaweza kuwa pamoja na Sindromu ya Lambert–Eaton myasthenic (udhaifu wa misuli kwa sababu ya autoantibodies), hipakalkemia, au sindromu ya homoni ya antidiuretic isiyofaa (SHAI). Tyuma katika ncha ya mapafu, inayoitwa tyuma ya Pancoast, inaweza kuingilia sehemu ya mfumo neva wa simpathetiki, na kusababisha sindromu ya Horner (kuanguka kwa kikawa cha jicho na mboni kwa upande huo), na kuharibika kwa brachial plexus.

Dalili nyingi za saratani hii (kukosa hamu ya chakula, kupoteza uzito, homa, uchovu) si bayana. Kwa wengi, saratani tayari imeenea zaidi kabla ya kuwa na dalili na kutafuta matibabu. Sehemu za kawaida inayoenea ni pamoja na ubongo, mifupa, adrenal gland, pafulililo mkabala, ini, perikadiumu, na figo. Takribani asilimia 10 ya watu walio na saratani hawana dalili wakati wa utambuzi; saratani hizi hupatikana wakati wa radiotherapi ya kifua.

Visababishi

Saratani hujitokeza kufuatia kuharibika kwa jenetiki kwa DNA. Hii huathiri utendakazi wa seli, pamoja na seli inayozaa, kufa kwa seli (apoptosis) na urekebishaji wa DNA. Uharibikaji unapoongezeka, ndivyo hatari ya saratani inavyoongezeka .

Uvutaji wa sigara

[[File:saratani ya mapafu.jpg|kidole cha thumb|Picha ya pafu la binadamu: Eneo nyeupe katika ndewe ya juu ni saratani; Maeneo nyeusi ni kugeuka kwa rangi unaosababishwa na uvutaji. Uvutaji, haswa sigara, ni kisababishi kikuu cha saratani ya mapafu. Moshi wa sigara huwa na kasinojeni zaidi ya 60 inayojulikana, ikijumuisha radioisotopu kutoka uozaji wa radoni, nitrosamine, na benzopyrene. Kwa kuongeza, nikotini huonekana kuvunja matokeo ya kinga kwa uvimbe wa saratani kwa tishu zilizowazi. Katika nchi zilizoendelea, asilimia 90 ya vifo vya saratani kwa wananume mwaka wa 2000 zilihusishwa na uvutaji wa sigara (asilimia 70 kwa wanawake). Uvutaji huchangia kwa asilimia 80-90 ya visa vya saratani.

Uvutaji wa moshi kutoka kwa anayevuta sigara—uvutaji moshi kutoka kwa mvuta siagara—ni kisababishi cha saratani kwa wasiovuta sigara. Mtu asiyevuta anaweza kuainishwa kama mtu anayeishi au kufanya kazi na mvutaji. Utafiti kutoka Marekani, Ulaya, Uingereza, na Australia Umeonyesha ongezeko kubwa la hatari kati ya wasiovuta sigara. Wanaoishi na mvuta sigara huwa na asilimia 20–na 30 ya ongezeko la hatari ilhali wanaofanya kazi katika mazingira yalio na moshi uliovutwa wana asilimia 16–19 ya ongezeko la hatari. Uchunguzi kuhusu moshi kutoka kwa wanaovuta unadokeza kuwa ni hatari zaidi kuliko moshi anaovuta mvutaji mwenyewe. Uvutaji wa moshi husababisha takribani vifo 3,400 kutokana na saratani ya mapafu kila mwaka nchini marekani.

Gesi ya Radoni

Radoni ni gesi isiyo na rangi na harufu inayotokana na kuharibika kwa mnururisho radiumu, ambayo ni bidhaa zilizooza za urani, zinazopatikana katika umbo la ardhi. Bidhaa za mnururisho zilizooza ioni vitu vya jenetiki, vikisababisha mabadiliko yanayoleta saratani. Radoni ni kisababishi cha pili cha kawaida cha saratani nchini Marekani baada ya uvutaji wa sigara. Hatari huongezeka asilimia 8–16 kwa kila ongezeko la 100 Bq/m³ katika kuwepo kwa radoni . Viwango vya gesi ya radoni hutofautiana kulingana na maeneo na elementi za mchanga ulio chini na miamba. Kwa mfano, katika maeneo kama Cornwall nchini Uingereza (iliyo na granite kama safu ya chini), gesi ya radoni ni tatizo kuu, na majengo yanafaa kuwa na matundu ya kupitishia hewa na fani ili kupunguza kiwango cha gesi ya radoni. United States Environmental Protection Agency Hukadiria kuwa moja kwa maboma 15 nchini Marekani huwa na viwango vya radoni zaidi ya miongozo iliyopendekezwa ya picocurie 4 kwa kila lita (pCi/l) (148 Bq/m³).

Asbesto

Asbesto inaweza kusababisha baadhi ya magonjwa ya mapafu, pamoja na saratani yake. Uvutaji wa tumbaku na asbesto huwa na athari ya inayoshirikiana kuanza kwa saratani ya mapafu. Pia inaweza kusababisha saratani ya pleura, inayoitwa mesothelioma (ambayo ni tofauti na saratani ya mapafu).

Kuchafuka kwa hewa

Kuchafuka kwa hewa huwa na athari ndogo kwa ongezeko la hatari ya saratani ya mapafu. chembe (PM2.5) na sulfate aerosols, inayoweza kutoka kwa ekzozi ya magari barabarani, huhusishwa na hatari kidogo. Kwa naitrojeni dioksidi, ongezeko la Sehemu 10 kwa kila bilioni huongeza hatari kwa asilimia 14. Kuchafuka kwa hewa huchangia karibu asilimia 1-2 ya saratani.

Pendekezo la dhibitisho kuunga mkono ongezeko la hatari ya saratani kutoka kwa uchafuzi wa hewa unaohusiana na kuchoma kuni, makaa, kinyesi cha mnyama, au mabaki yao ili kupika au kupasha joto. Wanawake wanaoathiriwa na moshi ya makaa huwa na hatari mara dufu kama baadhi ya mabaki ya kuchoma biomasi yanajulikana au ni kasinojeni zinazodhaniwa. Hatari hii huathiri takribani watu bilioni 2.4  ulimwenguni, Na kuchangia asilimia 1.5 ya vifo vya saratani ya mapafu.

Jenetikia

Inakadiriwa kuwa asilimia 8 hadi 14 ya saratani ya mapafu husababishwa na masuala ya kuurithi. Kwa jamaa walio na saratani, hatari huongezeka mara 2.4. Hii inawezekana kwa sababu ya mchanganyiko wa jeni.s

Visababishi vingine

Vitu vingine, Kazi, na maeneo mbalimbali yamehusishwa na saratani ya mapafu. International Agency for Research on Cancer (IARC) unaeleza kuwa "dhibitisho tosha" kuonyesha yafuatayo ni pafu lililo na kasinojeni:

  • Metali zingine (Utengenezaji wa aluminiamu, cadmium na elementi za kadimiamu, chromium(VI), beryllium na beriliamu, kupatikana kwa chuma na chuma cha pua, elementi za nikeli, arsenic na za aseniki isiyo hai, uchimbaji madini wa chini ya ardhi hematite)
  • Bidhaa zingine za mwako (mwako usiokamilika, makaa ya moto (moshi wa ndani kutokana na kuchoma makaa kwa nyumba), kugeuza makaa kuwa gesi, kuweka lami, utengenezaji wa makaa, masizi, utoaji dizeli kutoka kwa injini
  • Mnururisho aionishi (X-radiasheni, radoni-222 na vitu vyake vilivyooza, mnururisho wa gama, plutonium)
  • Gesi sumu ingine (methyl ether (technical grade), Bis-(chloromethyl) ether, sulfurmustard, MOPP (vincristine-prednisone-nitrogen mustard-procarbazine mixture), harufu kali ya moshi kutokana na upakaji wa rangi)
  • Utengenezaji wa raba na kristalini vumbi ya silika

Pathojenesisi

Sawa na saratani nyingine nyingi, saratani ya mapafu huanzishwa na uhai wa oncogene au kutokuwa hai kwa jeni inayokandamiza tyuma. Oncogenes zinaaminiwa huwafanya watu kuwa na uwezekano zaidi wa kupata saratani. Proto-oncogene zinaaminiwa kubadilika kuwa oncogenes zinapokutana na kasinojeni fulani. Mabadiliko katika K-ras proto-oncogene husababisha asilimia 10–30 ya adenocarcinomas ya mapafu. kipokezi cha suala la ukuaji wa epidemisi (KSUE) hudhibiti uzaaji wa seli, apoptosis, angiogenesis, na uvamizi wa tyuma. Mabadiliko na ukuaji wa KSUE hupatikana sana katika saratani ya seli kubwa ya mapafu na hupeana msingi wa kutibu kwa vizuizi vya KSUE. Her2/neu huathirika mara chache. Uharibifu wa Chromosomal unaweza kusababisha kukosekana kwa heterozygosity. Hii inaweza kusababisha kutotenda kazi kwa jeni zinazokandamiza tyuma. Kuharibika kwa chromosome 3p, 5q, 13q, na 17p ni kawaida hasa kwa kasinoma ya seli ndogo ya mapafu.p53 jeni inayokandamiza tyuma, iliyo kwa kromosomu 17p, huathirika katika asilimia 60-75 ya visa. Jeni zingine ambazo mara nyingi hubadilika au kukua ni c-MET, NKX2-1, LKB1, PIK3CA, naBRAF.

Utambuzi

[[Picha:Thorax CT peripheres Brronchialcarcinom li OF.jpg|kidole cha thumb|Ukaguzi wa CTkuonyesha tyuma ya saratani katika pafu la kushoto]] Kutekeleza radiotherapi ya kifua ni hatua ya kwanza ya uchunguzi ikiwa mtu ata ripoti dalili zinazoweza kuashiria saratani ya mapafu. Hii inaweza kuonyesha kupanuka kwa mediastinum (dokezo la kuenea kwa nodi ya limfu), atelectasis (kuvunjika), kuimarika (nimonia), au pleural effusion. Upigaji picha wa CT hutumiwa kupeana habari zaidi kuhusu aina na kiwango cha maradhi. Bronkoskopi au mwongozo wa CT biopsi mara nyingi hutumiwa kuchukua sampuli ya tyuma ili kufanyia histopatholojia.

Saratani ya mapafu hutokea kama nodu moja ya mapafu katika radiografu ya kifua. Hata hivyo, utambuzi wa kutofautisha ni mpana. Magonjwa mengine yanaweza kujitokeza hivi, pamoja na kifua kikuu, maambukizi ya kuvu, saratani ya metastasisi, au nimonia. Kisababishi kisicho cha kawaida cha nodu moja ya mapafu hujumuisha hamartoma, bronchogenic cyst, adenoma, ulemavu wa ateri na vena, pulmonary sequestration, rheumatoid nodule, Wegener's granulomatosis, au limfoma. Saratani ya mapafu pia inaweza kuwa utambuzi wa dharura, kama kifundo kimoja cha mapafu katika radiografu ya kifua au ukaguzi wa CT uliotekelezwa kwa sababu isiyohusiana. Utambuzi wa kufafanua saratani ya mapafu huzingatia histolojia uchunguzi wa tishu inayodhaniwa katika muktadha wa sifa za kliniki na radiolojia.

Uainishaji

Age-adjusted incidence of lung cancer by histological type
Histological type Incidence per 100,000 per year
All types 66.9
Adenocarcinoma 22.1
Squamous-cell carcinoma 14.4
Small-cell carcinoma 9.8

Saratani ya mapafu zimeainishwa kulingana na aina ya histolojia. Uainishaji huu ni muhimu kwa kubainisha udhibiti na kubashiri matokeo ya maradhi. Saratani nyingi za mapafu ni ya kasinoma—hatari inayotokana na seli za epithelia. Kasinoma ya mapafu huainishwa kwa ukubwa na jinsi seli hatari zinavyoonekana ikiangaliwa na histopatholojia kwa darubini. Aina zote mbili ni kasinoma ya mapafu ya seli ndogo na kasinoma ya mapafu ya seli kubwa.

Kasinoma ya mapafu ya seli kubwa

Saratani Ya Mapafu 
Mikrografu ya kasinoma ya squamous, aina ya kasinoma ya seli kubwa,sampuli ya FNA, doa la ubwabwa

Aina tatu ndogo za KMSK ni adenocarcinoma, kasinoma ya mapafu ya seli za squamous, na kasinoma ya mapafu ya seli ndogo.

Karibu asilimia 40 ya saratani huwa adenocarcinoma, ambayo kwa kawaida huanzia kwa tishu ya mapafu iliyo pembeni. Visa vingi vya adenocarcinoma huhusishwa na uvutaji; hata hivyo, kati ya watu waliovuta sigara chini ya 100 katika maisha yao ("wasiovuta"), adenocarcinoma ni aina ya saratani ya mapafu inayopatikana. Aina ndogo ya adenocarcinoma, bronchioloalveolar carcinoma, hupatikana sana kwa wanawake wasiovuta, na inaweza kuwa na muda nzuri wa kuishi.

Kasinoma ya seli ya squamous huchangia kwa takribani asilimia 30 ya saratani za mapafu. Hutokea kwa njia za hewa zilizokubwa. Kaviti tupu na inayohusishwa kufa kwa seli kwa kawaida hupatikana katikati ya tyuma. Takribani asilimia 9 ya saratani za mapafu ni kasinoma ya seli kubwa. Huitwa hivyo kwa kuwa seli za saratani ni kubwa, na zina cytoplasm nyingi zaidi, nukliasi iliyo kubwa na inayoonekana nucleoli.

Kasinoma ya mapafu ya seli ndogo

Katika kasinoma ya mapafu ya seli ndogo (KMSD), seli huwa na granuli nene zinazotoa neurosisi (vesicles zilizo na homoni), za mfumo wa neva na endokrini zinazopatia tyuma muungano wa sindromu ya endokrini/paraneoplasti. Mara nyingi hutokea katika njia za hewa zilizokubwa zaidi bronkia(za kwanza na za pili). Saratani hizi hukua haraka na kuenea mapema wakati wa maradhi. Asilimia sitini hadi sabini huwa na maradhi ya metastiki inapotokea. Aina hii ya saratani ya mapafu huhusishwa sana na uvutaji.

Zingine

Aina nyingine nne kuu za histolojia zimetambuliwa, hata ingawa saratani zingine zinaweza kuwa na mchanganyiko wa aina tofauti za aina ndogo. Aina ndogo zilizo nadra hujumuisha tyuma za glandi, tyuma za kasinoidi, na kasinoma zisizopambanuliwa.

Metastasisi

Typical immunostaining in lung cancer
Histological type Immunostain
Squamous-cell carcinoma CK5/6 positive
CK7 negative
Adenocarcinoma CK7 positive
TTF-1 positive
Large-cell carcinoma TTF-1 negative
Small-cell carcinoma TTF-1 positive
CD56 positive
Chromogranin positive
Synaptophysin positive

Mapafu ni sehemu ya kawaida ya uenezi wa tyuma kutoka sehemu zingine za mwili. Saratani za pili zimeainishwa kutokana na chanzo chake; kwa mfano, saratani ya matiti iliyoenea kwa mapafu huitwa saratani ya matiti ya metastasisi. Metastasisi mara nyingi huwa na sifa ya kuonekana mviringo kwa radiografu ya kifua.

Saratani za kwanza za mapafu kwa kawaida huenea kwa ubongo, mifupa, ini, na glandi ya adrenali. Immunostaining ya biopsi mara nyingi husaidia kubaini kiini halisi.

Hatua ya saratani

Hatua ya saratani ni kutathmini maenezi ya saratani kutoka chanzo chake. Ni mojawapo ya masuala yanayoathiri prognosisi na uwezekano wa kutibu saratani ya mapafu.

Utathmini wa kwanza wa hatua ya saratani ya mapafu ya seli kubwa (SMSK) hutumia uainishaji wa TNM. Hii huzingatia ukubwa wa tyuma, limfu huhusishaji nodi na kwa umbalimetastasisi. Baadaye, kwa kutumia kielezi TNM, Kikundi hupeanwa, kuanzia saratani ya kwanza kupitia awamu 0, 1-A (moja A), IB, IIA, IIB, IIIA, IIIB na IV (nne). Kikundi hiki cha awamu husaidia kwa uchaguzi wa matibabu na makadirio ya prognosisi. Kasinoma ya mapafu ya seli ndogo (KMSN) kimapokeo imeainishwa kuwa 'awamu iliyo na mpaka' (iliyofungiwa kwa moja na nusu ya kifua na kati ya eneo la radiotherapi moja inayoweza kustahimiliwa) au 'awamu pana' (magonjwa yaliyoenea pakubwa zaidi). Hata hivyo, uainishaji wa TNM na upangaji ni muhimu kwa kukadiria prognosisi.

Kwa KMSK na KMSK, aina zote mbili za kawaida za utathmini wa hatua ni ule wa kliniki na upasuaji. Hatua ya saratani hubainishwa kabla ya upasuaji wenyewe. Huzingatia matokeo ya masomo ya picha (kama vile uchunguzi wa CT na uchunguzi wa PET) na matokeo ya biopsi. Hatua ya upasuaji hutathminiwa wakati wa au baada ya upasuaji, na huzingatia muunganisho wa matokeo ya upasuaji na kliniki, pamoja na kuchukua sampuli za nodi za limfu za kifua.

UKingaji

Ukingaji ndio gharama ya chini ya kuzuia kukua kwa saratani ya mapafu. Ilhali katika mataifa mengi kasinojeni za viwanda na zile za nyumbani zimetambuliwa na kupigwa marufuku, uvutaji tumbaku ungali umeenea pakubwa. Kukomesha uvutaji wa tumbaku ni lengo la kwanza katika ukingaji kukomesha uvutaji ni kifaa muhimu katika utaratibu huu.

Sera za kupunguza uvutaji wa moshi ya sigara Kwenye maeneo kama vile hoteli na pahali pa kufanyia kazi umekuwa wa kawaida katika mataifa mengi ya magharibi. Bhutan imepiga marufuku uvutaji wa sigara tangu mwaka wa 2005 ilhali India ilipiga marufuku uvutaji wa tumbaku mwezi wa kumi 2008. Shirika la Afya la Ulimwengu limetoa wito kwa serikali kuanzisha upigaji marufuku wa kutangaza tumbaku ili vijana wasianze kuvuta. Hutathmini unaonyesha kuwa uvutaji umepungua kwa asilimia 16%.

Utumiaji wa nyongeza ya vitamini A kwa muda mrefu, vitamini C, vitamini D au vitamin E Hupunguzi hatari ya saratani ya mapafu. Uchunguzi mwingine unapendekeza kuwa watu wanaokula chakula kilicho na kiwango cha juu zaidi cha mboga na matunda wana hatari ya chini, lakini hii inawezekana kwa sababu ya kushangaza. Uchunguzi mkali zaidi haujaonyesha ushirikiano dhahiri.

Uchunguzi

Uchunguzi ni matumizi ya uchunguzi wa matibabu ili kubaini ugonjwa kwa watu wanaoonyesha dalili. Uwezekano wa vipimo vya kuchuja saratani ya mapafu ni pamoja na sputum saitolojia, radiografu ya kifua, na tomografia ya digitali. Utaratibu wa uchunguzi unaotumia radiografu ya kifua au saitologia haijaleta manufaa. Kuchuja walio katika hatari kuu (yaani, miaka 55 hadi 79 waliovuta zaidi ya   pakiti 30 kwa mwaka au wale wamewahi kupata saratani ya mapafu hapo awali) kwa mwaka na dozi iliyo chini ya uchunguzi wa picha inaweza kupunguza uwezekano wa kifo kutokana na saratani ya mapafu kwa kiasi kamili ya asilimia 0.3 (hatari kiasi ya asilimia 20). Hata hivyo, kuna kiwango cha juu ya matokeo duni kinachoweza kusababisha utaratibu wa upasuaji vile vile gharama kubwa ya fedha. Kwa kila tokeo la kipimo halisi kuna zaidi ya 19 ya matokeo duni. Kuwa wazi kwa mnururisho ni njia nyingine ya madhara inayoweza kuwa kutokana na kuchuja.

Udhibiti

Matibabu ya saratani ya mapafu hulingana na seli maalum ya saratani kuenea, na hali ya utendaji wa mtu. Matibabu ya kawaida hujumuisha huduma ya kupunguza maumivu, upasuaji, kemotherapi, na therapi ya mnururisho.

Upasuaji

Ikiwa uchunguzi utathibitisha KSMK, hatua inatathminiwa ili kuamua ikiwa kuna ugonjwa katika eneo maalum na inaweza kutibiwa kwa upasuaji au iwapo imeenea kwa kiwango kisichoweza kufanyiwa upasuaji. Uchunguzi wa picha na picha ya kompyuta ya miale ya gama inatumika kwa uamuzi. Ikiwa unashuku tezi ya mediastinamu inahusika, upasuaji wa mediastinamu inaweza kutumika kutengeneza sampuli nodi na kutathmini kiwango. Upimaji wa damu na uchunguzi wa utendakazi wa mapafu hutumika kutathmini iwapo mtu atafanyiwa upasuaji. Ikiwa matokeo ya uchunguzi wa utendakazi wa mapafu yataonyesha kuwa mapafu hayana hewa ya kutosha, upasuaji hautawezekana.

Katika hali nyingi za kwanza KSMK, kutoa tundu la pafu matibabu ya upasuaji ya (lobektomia) huchaguliwa. Watu wasio sawa kwa lobektomia mzima, sublobar kiasi (kuondoa kipande cha tishu) inaweza kutekelezwa. Hata hivyo, kuondoa kipande hiki kina hatari kubwa ya kurudi tena kuliko lobektomia. Mnururisho iodini brachytherapy ukingoni mwa kuondoa kipande cha tishu unaweza kupunguza hatari ya kurudi tena. Ni nadra, kutoa pafu lote (numonektomi) hufanywa. Upasuaji wa thoracoscopic unaosaidiwa na video na lobektomia ya VATS hutumia njia itakayoingia ndani katika upasuaji. Lobektomia ya VATS inapendekezwa kwa usawa kulingana na lobektomia ya wazi iliyo kawaida, na magonjwa baada ya upasuaji.

Kwa KSMN, kemotherapi na/au radiotherapi hutumika. Hata hivyo jukumu la upasuaji kwa KSMN inastahili kufikiriwa tena. Upasuaji unaweza kuboresha matokeo itakapowekwa kwa kemotherapi na mnururisho katika hatua ya kwanza ya KSMN.

Radiotherapi

Radiotherapi hutolewa mara kwa mara pamoja na kemotherapi, na inaweza kutumika pamoja na dhamira ya kuponya kwa watu walio na KSMK wasioweza kufanyiwa upasuaji. Hali iliyo kali sana huitwa radiotherapi ya radikali. Mabadiliko ya utaratibu huu hugawanywa kulingana na makali ya radiotherapi unaoendelea, ambapo dozi kali ya radiotherapi hutolewa kwa muda mfupi. Radiotherapi ya kifua baada ya upasuaji haipaswi kutumika baada ya upasuaji wa dhamira ya kuponya kwa watu waliona KSMK. Baadhi ya watu walio na mediastinamu ya limfu nodi ya N2 inayohusika wanaweza kufaidika kutokana na radiotherapi ya baada ya upasuaji.

Kwa hali ya KSMN, radiotherapi mara nyingi inapendekezwa zaidi pamoja na kemotherapi.

Ikiwa ueneaji wa saratani itaziba sehemu ya bronkasi, brachytherapy (radiotherapi maalum) inaweza kupewa moja kwa moja ndani ya njia ya hewa ili njia ifunguke. Kulingana na mwali wa mwanga ya nje ya radiotherapi, brachytherapy inaruhusu kupungua kwa muda wa matibabu na upungufu wa uwazi kwa mnururisho kwa wahudumu wa afya.

Prophylactic cranial irradiation (PCI) ni aina ya radiotherapi kwa akili, hutumika kupunguza hatari ya metastasisi. (PCI) hutumika sana kwa KSMN. Katika hatua za ugonjwa mdogo, (PCI) huongeza miaka mitatu za maisha kutoka asilimia 15 hadi 20; kwa ugonjwa uliozidi, kuishi mwaka mmoja huzidi kutoka asilimia 13 hadi 27.

Maendeleo ya hivi karibuni yanayolenga na kutoa picha yameleta maendeleo ya upasuaji kwa kutumia mnururisho kwa kutibu saratani iliyo katika hatua ya kwanza. Katika aina hii, dozi kali hutolewa kwa idadi ndogo ya vipindi kwa kutumia mbinu ya kulenga upasuaji. Matumizi yake hasa ni kwa wagonjwa wasiofanyiwa upasuaji kwa sababu ya matibabu comorbidities.

Kwa wagonjwa walio na KSMK na KSMN, dozi kiasi cha mnururisho kwa kifua inaweza kutumika ili kudhibiti dalili (radiotherapi ya inayopunguza maumivu).

Kemotherapi

Mazoezi ya kemotherapi inalingana na aina ya tyuma. Kasinoma ya mapafu ya seli ndogo (KMSN), hata kiasi kidogo ya hatua ya kwanza ya ugonjwa, hutibiwa hasa kwa kemotherapi na mnururisho. Kwa KMSN, cisplatin na etoposide kwa kawaida hutumika zaidi. Zikiunganishwa na carboplatin, gemcitabine, paclitaxel, vinorelbine, topotecan, na irinotecan pia zinatumika. Kwa kasinoma ya mapafu ya seli kubwa (KMSK) iliyozidi, kemotherapi huboresha maisha na hutumika kama tiba ya kwanza, bora mtu awe sawa kwa kupokea matibabu. Kwa kawaida, dawa mbili hutumika, moja yazo mara nyingi huwa besi ya platinamu (ama cisplatin au carboplatin). Dawa zingine zinazotumika ni gemcitabine, paclitaxel, docetaxel, pemetrexed, etoposide au vinorelbine.

Kemotherapi ya adjuvant inamaanisha matumizi ya kemotherapi baada ya matibabu ya upasuaji ili kuboresha matokeo. Katika KMSK, sampuli huchuliwa karibu na limfu nodi wakati wa upasuaji ili kusaidia hatua. Ikiwa ugonjwa wa kiwango cha II au cha III kitatambulika, kemotherapi ya adjuvanti inaboresha maisha kwa asilimia 5 kwa miaka mitano. Matumizi ya vinorelbine pamoja na cisplatin yana matokeo bora kuliko mazoezi. Kemotherapi ya adjuvanti kwa watu waliokuwa na saratani iliyo kiwango IB haijakubalika, kama vipimo vya kliniki havijaonyesha manufaa. Vipimo vya kemotherapi kabla ya upasuaji (kemotherapi ya neoadjuvant) kwa KMSK yanayoweza kugawanywa hayajahitimishwa.

Huduma ya kupunguza maumivu

Kwa wagonjwa walio na ugonjwa usiotibika, huduma ya kupunguza au udhibiti wa hospitali inafaa. Mbinu hizi hukubali majadiliano zaidi ya matibabu na kutoa nafasi kuafikia kwa maamuzi yaliyozingatiwa vilivyo na yanaweza kuepushwa na huduma isiyosaidia katika maisha.

Kemotherapi inaweza kuunganishwa na huduma ya kupunguza maumivu kwa matibabu ya KMSK. Kwa hali zilizozidi, kemotherapi inayofaa huboresha maisha wastani zaidi ya huduma ya kusaidia pekee, vile vile kuboresha ubora wa maisha. Pamoja na ubora wa mwili unaofaa, kuendeleza kemotherapi wakati wa kutuliza saratani ya mapafu huzidisha maisha kwa miezi 1.5 hadi 3, kutuliza dalili, na kuboresha maisha, pamoja na matokeo mema zinazoonekana na maajenti wa kisasa. Kikundi cha chambuzi cha KMSK inapendekeza kwamba iwapo mgonjwa anahitaji na anaweza kuvumilia matibabu, basi kemotherapi inapaswa kutumiwa kwa KMSK iliyoendelea.

Prognosisi

Outcomes in lung cancer according to clinical stage
Clinical stage Five-year survival (%)
Non-small cell lung carcinoma Small cell lung carcinoma
IA 50 38
IB 47 21
IIA 36 38
IIB 26 18
IIIA 19 13
IIIB 7 9
IV 2 1

Prognosisi huwa duni. Kwa watu wote walio na saratani ya mapafu, asilimia 15 huishi kwa miaka mitano baada ya kutambuliwa. Mara kwa mara kiwango huzidi wakati wa utambuzi. Wakati wa kujitokeza, asilimia 30-40 ya hali ya KMSK huwa kiwango cha IV, na asilimia 60 ya KMSN huwa kiwango cha IV.

Visababishi vya prognosisi katika KMSK ni pamoja na kuwepo na kutokuwepo kwa dalili za mapafu, ukubwa wa tyuma, (histologia) ya aina ya seli, kiwango cha kuenea (hatua) na metastasisi kwa limfu nodi yaliyozidi, na kuathiriwa kwa mishipa. Kwa watu walio na ugonjwa usiofanyiwa upasuaji, matokeo huwa mabaya kwa walio na hali ya utendakazi mbaya na upungufu wa uzito zaidi ya asilimia 10. Visababishi vya prognosisi kwa saratani ya mapafu kwa seli ndogo inahusisha hali ya utendakazi, jinsia, kiwango cha ugonjwa, na kuhusika kwa mfumo wa kati wa neva au ini wakati wa utambuzi.

Kwa KMSK, prognosisi bora imefanikishwa na upasuaji kamili wa kiwango cha IA cha ugonjwa, ikiwa na asilimia 70 ya kuishi miaka mitano. Kwa KMSK, maisha kwa ujumla ni angalau asilimia 5. Watu walio na kiwango kilichozidi cha KMSK kawaida huwa kiasi cha miaka mitano ya kiwango cha maisha iliyo chini ya asilimia 1. Muda wa kawaida wa kuishi wa kiwango kidogo cha ugonjwa ni miezi 20, na kiwango cha miaka mitano za kuishi zilizo asilimia 20.

Kulingana na utafiti wa Taasisi ya kimataifa ya saratani, umri wa kati ya kutambua saratani ya mapafu kule Marekani ni miaka 70, na umri kati ya kifo ni miaka 72. Nchini Marekani, walio na bima ya matibabu hupata matokeo bora zaidi.

Epidemiolojia

Saratani Ya Mapafu 
Umri uliosanifishwa vifo kutokana na trakea, bronkasi, na saratani ya mapafu kwa 100,000 walioishi mwaka wa 2004
     no data      ≤ 5      5-10      10-15      15-20      20-25      25-30
     30-35      35-40      40-45      45-50      50-55      ≥ 55
Saratani Ya Mapafu 
Mgawanyo wa saratani ya mapafu nchini Marekani

Ulimwenguni, saratani ya mapafu ni ya kawaida katika swala la tukio na kifo. Katika 2008, kulikuwa na milioni 1.61 za hali mpya, na vifo milioni 1.38 kwa sababu ya saratani ya mapafu. Viwango vilivyo juu sana kiko Uingerezani na Kaskazini Marekani. Sehemu ya watu wanaoweza kupata saratani ya mapafu zaidi ni wale waliozidi umri wa miaka 50 wanao historia ya uvutaji wa sigara. Kwa kutofautisha kiwango cha vifo kwa wanaume, iliyoanza kushuka zaidi miaka ishirini iliyopita, viwango vya vifo kutokana na saratani ya mapafu kwa wanawake vimeongezeka zaidi katika kipindi cha miaka kumi zilizopita, na vinaanza kutulia. Nchini Marekani, hatari ya kupata saratani ya mapafu ni asilimia 8 kwa wanaume na asilimia 6 kwa wanawake.

Kwa kila milioni 3-4 ya sigara iliyovutwa, kifo kimoja hutokea kutokana na saratani ya mapafu. Ushawishi wa "Tumbaku Kubwa" huchukua jukumu kubwa katika utamaduni wa uvutaji wa sigara. Vijana wasiovuta sigara wanao tazama matangazo ya uvutaji wa sigara huenda wakavuta. Jukumu la kuvuta moshi ya sigara inaendelea kutambulika kama hatari ya saratani ya mapafu, inayoelekeza kwa sera ya kuingilia upungufu wa wasiovuta kutotaka kuwa karibu wavutaji wanapovuta. Moshi kutoka magari, viwanda, na vituo vya umeme pia vinaweza kuwa hatari.

Ulaya Mashariki ina vifo vilivyosababishwa na saratani ya mapafu vilivyo juu kwa wananume, bali kaskazini mwa Uingereza na Marekani huwa na vifo vingi kwa wanawake. Nchini Marekani, wanaume na wanawake weusi huwa na hali iliyo juu zaidi. Viwango vya saratani kwa sasa viko chini kwa nchi zinazoendelea. Pamoja na ongezeko la uvutaji kwa nchi zinazoendelea, viwango vinatarajiwa kuongezeka kwa miaka michache yanayokuja, hasa Uchina na India.

Kutoka 1960, viwango vya adenocarcinoma vilianza kuzidi kulingana na aina zingine za saratani ya mapafu. Hii ndio sababu ndogo ya kuanzishwa kwa sigara yenye chujio. Matumizi ya chujio hutoa moshi nzito kutoka tumbaku, hivyo kupunguza mabaki kwa njia za kupumua. Hata hivyo, mvutaji lazima avute moshi ndani sana ili apate kiasi sawa cha nikotini, na kuzidisha moshi kuingia kwa njia ndogo za hewa ambapo adenocarcinoma ina panda. Hali ya adenocarcinoma ya mapafu huzidi kupanda.

Historia

Saratani ya mapafu haikujulikana kabla ya matangazo ya uvutaji wa sigara; haikutambulika kama ugonjwa tofauti hadi mwaka wa 1761. Vipengele tofauti vya saratani ya mapafu yameelezwa zaidi mwaka wa 1810. Tyuma ya mapafu ya kuhatarisha yamechangia asilimia 1 pekee kwa saratani yaliyoonekana kwa otopsi mwaka 1878, lakini yalizidi asilimia 10-15 mwanzoni mwa mwaka 1900. Ripoti za uchunguzi katika maandiko ya matibabu yalikuwa 374 pekee duniani mwaka 1912, lakini uchunguzi wa otopsi ulionyesha hali ya saratani ya mapafu yaliongezeka kutoka asilimia 0.3 mwaka 1852 hadi asilimia 5.66 mwaka 1952. Nchini Ujerumani mwaka 1929, fizishiani Fritz Lickint alitambua uhusiano baina ya uvutaji wa sigara na saratani ya mapafu, iliyoelekeza kwa kampeni ya kupinga uvutaji wa sigara ulio mkali. Uchunguzi ya madaktari wa Uingereza, uliochapishwa wa 1950, ili kuwa ya kwanza epidemiolojia ili kuwa ushahidi kuu ya kiunganishi baina saratani ya mapafu na uvutaji wa sigara. Kama matokeo, mwaka 1964 Mpasuaji Mkuu nchini Marekani aliwashauri wavutaji sigara kuwacha kuvuta.

Uhusiano na gesi ya radoni ulitambuliwa na wachimbuaji wa madini katika Milima za Ore karibu na Schneeberg, Saxony. Fedha ime chimbuliwa hapo tangu mwaka wa 1470, na machimbo haya yana urani nyingi, ikitanguliwa na radiamu na gesi ya radoni. Wachimbuaji madini walipata kiasi isiyolingana na saratani ya mapafu, baadae kujulikana kama saratani ya mapafu mwaka wa 1870. Licha ya utambulizi huu, kuchimbuliwa kulizidi hadi mwaka wa 1950, kwa sababu ya madai ya urani kutoka Urusi. Radoni ilitambulika kama kisababishi cha saratani ya mapafu mwaka wa 1960.

Mafanikio ya kwanza ya numonektomi ya saratani ya mapafu ulifanywa mwaka wa 1933. Radiotherapi ya kupunguza maumivu imetumika tangu mwaka wa 1940. Radiotherapi ya radikali, iliyotumika awali mwaka wa 1950, ilikuwa jaribio la kutumia dozi kubwa ya mnururisho kwa wagonjwa walio na kiasi cha saratani kinachoanza, lakini hawawezi kufanyiwa upasuaji vinginevyo. Mwaka wa 1997, mkeneko mkali wa radiotherapi uliochapuzwa unaoendelea ulionekana ukiendelea kuliko radiotherapi ya radikali iliyo ya kawaida. Kwa SMSD, majaribio ya hapo awali mwaka wa 1960 katika upasuaji na radiotherapi ya radikali hayakufaulu. Mwaka wa 1970, kemotherapi ya mazoezi yaliyofaulu yaliendelezwa.

Marejeo

Tags:

Saratani Ya Mapafu Ishara na daliliSaratani Ya Mapafu VisababishiSaratani Ya Mapafu PathojenesisiSaratani Ya Mapafu UtambuziSaratani Ya Mapafu UKingajiSaratani Ya Mapafu UdhibitiSaratani Ya Mapafu PrognosisiSaratani Ya Mapafu EpidemiolojiaSaratani Ya Mapafu HistoriaSaratani Ya Mapafu MarejeoSaratani Ya MapafuDaliliMapafu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

PamboMkoa wa SingidaRupiaUsawa (hisabati)PalestinaSiasaMkoa wa PwaniMkoa wa KageraShairiSaratani ya mlango wa kizaziNandyChakulaNyaniSah'lomonAlfabetiMaghaniKoroshoRisalaNimoniaVielezi vya idadiMartin LutherUNICEFNgiriVivumishi vya kumilikiUgandaVivumishi vya -a unganifuWimboKoloniAgano la KaleLahajaMsamiatiMbezi (Ubungo)Steve MweusiWilaya ya KinondoniWikipediaHurafaVasco da GamaMadiniVitenzi vishiriki vipungufuVichekeshoHistoria ya WapareKonsonantiNgeliWajitaDamuUshairiNuktambiliMusaMadawa ya kulevyaKitenzi kikuu kisaidiziKiingerezaUaMandhariWaluguruMshubiriHarmonizeUvimbe wa koromeo usababishwao na streptokokiAmri KumiOrodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaTambikoKitenziMisemoJamhuri ya Watu wa ZanzibarMethaliFasihiDawatiAli Hassan MwinyiArsenal FCMkoa wa MorogoroImaniJumuiya ya Afrika MasharikiBaraAndalio la somo🡆 More