Dubai (kwa Kiarabu: دبيّ) ni mji mkuu wa ufalme wenye jina hilo katika katika Shirikisho la Falme za Kiarabu kwenye rasi ya Uarabuni.
Uko kwenye mwambao wa Ghuba ya Uajemi kati ya Sharjah na Abu Dhabi.
Jiji la Dubai lilikuwa mji mdogo wenye wakazi 20,000 tu hadi vita kuu ya pili ya dunia. Leo hii kuna wakazi zaidi ya 1,200,000. Nyumba zote za Dubai ni mpya.
Kukua kwa Dubai kulitokana na mapato ya mafuta ya petroli. Lakini akiba za mafuta hayo si kubwa kama kwa majirani yake. Mapato ya mafuta ni 6% pekee za pato la taifa.
Viongozi wa ufalme wa Dubai wamefaulu kuweka msingi mpya wa uchumi katika biashara na utalii.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Dubai (mji), which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.