Utao

Utao (pia: udao) ni aina ya imani katika nchi ya China inayoitwa wakati mwingine falsafa na wakati mwingine dini.

Utao
Alama ya Yin-yang ni nembo ya Utao.

Asili yake ni katika karne ya 4 KK wakati mzee Laotze alipoandika kitabu cha Tao te king. Mafundisho yake ni msingi wa Utao.

Nembo yake ni alama ya taijitu inayojulikana zaidi kama yin-yang inayoonyesha jinsi gani vilivyo kinyume ni umoja.

Pamoja na Ukonfusio na Ubuddha ni moja ya imani tatu zilizoathiri na kuumba utamaduni wa China. Mafundisho yake huonekana katika Siasa, uchumi, sanaa, falsafa, fasihi, chakula, tiba, kemia, jiografia na elimu ya vita.

Tao au Dao kiasili ni neno la Kichina la kutaja "njia". Katika Utao imekuwa njia ya kutaja nguvu inayoratibu ulimwengu. Wafuasi wa Utao huamini ya kwamba hakuna maneno ya kibinadamu yanayoweza kueleza tao yenyewe. Kwa hiyo wanaona umuhimu wa kufuata utaratibu wa maisha badala ya majadiliano ya kinadharia. Tao ina nia yake na mtu anatakiwa kwenda sambamba iwezekanavyo na mwendo asilia wa maisha.

Mafundisho yake hukazia sifa za huruma, upole na unyenyekevu.

Watao wanaokazia upande wakidini wanatafuta raha ya milele. Katika imani yao kuna miungu mingi kwenye ngazi mbalimbali ya enzi. Miungu wa juu ni "watatu walio safi".

Wakati wa ukomunisti mkali chini ya Mao Zedong utao uligandamizwa pamoja na dini zote na mahekalu mengi yaliharibiwa. Wamonaki na makuhani walifungwa gerezani, wengine kuuawa na kulazimihswa kuacha kazi yao. Lakini imani iliendelea kwa siri. Leo hii kuna makadirio ya kwamba labda Wachina milioni 80 hufuata tena Utao pamoja na wengine nje ya Jamhuri ya Watu wa China kama huko Taiwan, Singapur na penginepo.

Viungo vya nje

Utao  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

ChinaDiniFalsafaImani

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Ugonjwa wa uti wa mgongoJumaPonografiaMjombaOrodha ya viwanja vya ndege nchini TanzaniaKiboko (mnyama)Manchester United F.C.UtumwaMapafuRushwaJamhuri ya Watu wa ChinaLugha ya kwanzaYouTubeParisMkoa wa TaboraKiimboChuraFacebookSteven KanumbaPumuUKUTAThrombosi ya kina cha mishipaMkoa wa GeitaCosta TitchUshairiLionel MessiMsitu wa AmazonSayari ya TisaUkraineWangoniHistoria ya WapareKata za Mkoa wa MorogoroFonetikiBabeliHomoniViwanja vya Afrika (Kwa Ukubwa)Mfumo wa upumuajiNomino za pekeeHoma ya matumboTahajiaPilipiliBungeKiranja MkuuMaambukizi ya njia za mkojoSumakuWapareMkoa wa MaraMsengeAdhuhuriPichaKisaweTanzaniaVivumishi vya kuoneshaZama za MaweAli KibaUyahudiMajiMethaliMohamed HusseinMeno ya plastikiUhuruKikohoziUhifadhi wa fasihi simuliziKusiniTarakilishiAla ya muzikiUrusiWanyamaporiMkoa wa Unguja Mjini MagharibiAurora, ColoradoDiraViwakilishi vya -a unganifuKwaresimaNomino za kawaidaJomo KenyattaSanaa za maoneshoDar es SalaamMuziki🡆 More