Mfereji Wa Suez

Mfereji wa Suez (kwa Kiarabu: قناة السويس, qanā as-suways) ni mfereji mkubwa nchini Misri.

Mfereji Wa Suez
Manowari ikipita katika Mfereji wa Taabah Rafah Straights.
Mfereji Wa Suez
Mfereji wa Suez kutoka angani kati ya Mediteranea (juu) na Bahari ya Shamu (chini).

Mahali pake

Unaunganisha Bahari ya Mediteranea na Bahari ya Shamu, hivyo na Bahari Hindi pia.

Mfereji uko upande wa magharibi wa rasi ya Sinai. Urefu wake ni km 163 na upana ni kuanzia mita 300.

Unaanza mjini Port Said (Būr Sa'īd) upande wa Mediteranea na kuishia mjini Suez (al-Suways) upande wa Bahari ya Shamu.

Historia

Ulijengwa na kampuni ya Kifaransa kati ya miaka 1859 na 1869.

Kuna mifereji mbalimbali iliyotangulia huko kuanzia karne ya 14 KK hadi wakati wa Waarabu katika karne ya 8 BK. Lakini yote haikudumu kwa sababu ya matatizo ya kuondoa mchanga mara kwa mara kwa mitambo iliyopatikana zamani. Tena katika mifereji ya zamani ilikuwa serikali ya Misri tu iliyotaka kurahisisha usafiri na ubebaji wa mizigo.

Tangu kupatikana kwa meli za kisasa idadi ya meli kati ya Ulaya na Asia iliongezeka sana katika karne ya 19. Zote zilipaswa kuzunguka Afrika yote au kuondoa mizigo na abiria upande wa Mediteranea na kuwasafirisha hadi Suez. Hivyo ilikuwa jitihada ya kimataifa yaliyoleta mfereji wa kisasa.

Meli ya kwanza ilipitia mfereji mpya tarehe 17 Februari 1867. Mtunzi wa muziki Giuseppe Verdi aliandika opera yake Aida hasa kwa nafasi hiyo.

Umuhimu wa mfereji wa Suez

Mfereji Wa Suez 
Njia za usafiri baharini kabla na baada ya kupatikana kwa Mfereji wa Suez

Mfereji wa Suez unafupisha umbali wa safari ya meli kati ya Ulaya na Asia kwa kilomita 8,000 hivi; kwa mfano safari baina ya Rotterdam (bandari kubwa ya Ulaya) na Dubai ni takriban kilomita 20,900 na siku 24 kwa njia ya kuzunguka Afrika; kupitia Mfereji wa Suez ni kilomita 12,000 na siku 12 pekee. Mfereji umeharakisha na kurahisisha usafiri kati ya Ulaya, Asia na Afrika ya Mashariki. Zipatao meli 15,000 zinapita kwenye mfereji kila mwaka.

Mafanikio ya mfereji wa Suez yalihamasisha mianzo ya Mfereji wa Panama.

Kutaifishwa kwa mfereji 1956

Mfereji ulikuwa mali ya Compagnie universelle du canal maritime de Suez au kampuni ya mfereji wa Suez na hisa zake zilikuwa mikononi mwa serikali za Ufaransa na Uingereza.

Mwaka 1956 serikali ya Misri chini ya rais Gamal Abdel Nasser ilitaifisha mfereji na tendo hilo likasababisha vita ya Suez ya 1956 ambako Uingereza, Ufaransa na Israel zililazimishwa na mataifa makubwa kujiondoa katika Misri baada ya uvamizi wao.

Tags:

Mfereji Wa Suez Mahali pakeMfereji Wa Suez HistoriaMfereji Wa Suez Umuhimu wa mfereji wa SuezMfereji Wa Suez Kutaifishwa kwa mfereji 1956Mfereji Wa SuezKiarabuMferejiMisri

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Uvimbe wa sikioSamia Suluhu HassanOrodha ya majimbo ya MarekaniFasihi simuliziMsokoto wa watoto wachangaWizara za Serikali ya TanzaniaMmeaSaratani ya mlango wa kizaziMwanamkeTanganyika (ziwa)Ricardo KakaMkoa wa DodomaUgonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofunganaMarekaniUturukiNdoaMpira wa miguuMkoa wa NjombeMkoa wa MorogoroHistoria ya KanisaHali ya hewaNomino za kawaidaMnyamaMaana ya maishaAlizetiUtawala wa Kijiji - TanzaniaAmina ChifupaRohoMapinduzi ya ZanzibarMfumo wa mzunguko wa damuAfrikaAla ya muzikiJinsiaMahakamaBurundiPunda miliaAbrahamuHistoriaVitenzi vishirikishi vikamilifuRadiKanisaIntanetiOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoNambaBenjamin MkapaKonsonantiMtakatifu PauloPentekosteMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaMkoa wa MwanzaMvuaFonolojiaWaziriTanganyika African National UnionImaniKunguruHekaya za AbunuwasiMbezi (Ubungo)Kishazi huruIdi AminMaumivu ya kiunoMtumbwiFamiliaTabianchiSentensiUshairiKitenzi kikuuVivumishi vya kuoneshaUzazi wa mpango kwa njia asiliaTungo kishaziDemokrasiaUjimaBunge🡆 More