Latvia

Latvia (kwa Kilatvia: Latvija au Latvijas Republika, kwa Kilivonia: Lețmō au Leţmō Vabāmō) ni nchi ya Kibalti katika Ulaya ya Kaskazini.

Latvia
Latvia
Ramani ya Latvia

Imepakana na Estonia, Lithuania, Belarus na Urusi. Uswidi iko ng'ambo ya bahari ya Baltiki.

Mji mkuu ni Riga.

Latvia ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu 1 Mei 2004.

Historia

Kwa muda mrefu Estonia ilikuwa chini ya Wajerumani, Wapolandi na Waswidi, halafu (1710) sehemu ya Dola la Urusi.

Katika miaka 1918-1940 ilikuwa jamhuri halafu miaka 1940-1991 mwanachama wa Umoja wa Kisovyeti.

Baada ya umoja huo wa majimbo 15 kusambaratika, Latvia ilijitangaza nchi huru tena.

Latvia ilijiunga na Umoja wa Ulaya baada ya azimio la Halmashauri Kuu ya Ulaya ya tarehe 13 Desemba 2002 iliyokutana Kopenhagen.

Katika kura ya maoni ya tarehe 20 Septemba 2003 ni 66.9% za Walatvia wote waliokubali azimio hilo.

Latvia iliingia rasmi katika Umoja wa Ulaya tarehe 1 Mei 2004 pamoja na nchi nyingine 9 za Ulaya mashariki.

Watu

Idadi ya watu inapungua, na sasa iko chini ya milioni 2.

Wakazi wengi ni Walatvia 61.6%, halafu Warusi 25.8%, Wabelarus 3,4%, Waukraina 2,3%, Wapolandi 2,1%, Walituania 1.2% na wengine 4.8%.

Lugha rasmi ni Kilatvia, ambayo ni mojawapo ya lugha za Kibalti. Wananchi walipiga kura ya kukataa Kirusi kama lugha rasmi ya pili.

Upande wa dini, wengi (78.5%) ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali, ingawa 7% tu wanashiriki ibada mara kwa mara. Hasa ni Walutheri (34.2%), Wakatoliki (24.1%) na Waorthodoksi (19.4%). Asilimia 21.1 hawana dini yoyote.

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

    Serikali
    Taarifa za jumla
    Elimu na utamaduni
    Utalii
    Ramani


Nchi za Umoja wa Ulaya Latvia 
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Latvia  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Latvia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Latvia HistoriaLatvia WatuLatvia Tazama piaLatvia MarejeoLatvia Viungo vya njeLatviaNchi ya KibaltiUlaya ya Kaskazini

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Historia ya uandishi wa QuraniMabiboWimboP. FunkTetekuwangaOrodha ya vyama vya siasa TanzaniaWhatsAppMatiniTume ya Taifa ya UchaguziMichael JacksonMkoa wa KigomaJangwaTawahudiSheriaKinjikitile NgwaleAndalio la somoBiasharaAfrika Mashariki 1800-1845BungeSayariJKT TanzaniaMatumizi ya lugha ya KiswahiliLuhaga Joelson MpinaBunge la TanzaniaKishazi huruNdoa katika UislamuHisiaMvua ya maweRushwaUaKitunda (Ilala)Milango ya fahamuZiwa ViktoriaBendera ya KenyaMwakaRupie ya Afrika ya Mashariki ya KijerumaniHadithiNgeliMasadukayoLugha rasmiTeknolojiaKichochoSikioUgonjwa wa uti wa mgongoRejistaMkoa wa LindiMofimuMaadiliSeli za damuOrodha ya Magavana wa TanganyikaUshairiHistoria ya TanzaniaPopoInjili ya LukaFasihiUingerezaMfumo wa upumuajiUNICEFUlumbiDawatiKassim MajaliwaSintaksiSteven KanumbaNguruwe-kayaMfumo wa mzunguko wa damuMbossoKadi za mialikoMawasilianoRamaniDemokrasia🡆 More