Bahari Ya Baltiki

Bahari ya Baltiki ni bahari ya kando ya Atlantiki katika Ulaya ya Kaskazini.

Imezungukwa na nchi kavu pande zote isipokuwa kati ya Denmark na Uswidi kuna mlangobahari mwembamba wa kuiunganisha na Bahari ya Kaskazini.

Bahari Ya Baltiki
Ramani ya Bahari ya Baltiki.

Mipaka yake

Bahari ya Baltiki imepakana na nchi za Uswidi, Ufini, Urusi, Estonia, Latvia, Lituanya, Poland, Ujerumani na Denmark.

Sehemu ya kaskazini kabisa iko mpakani mwa Uswidi na Ufini katika Ghuba ya Botnia, sehemu ya mashariki kabisa katika Ghuba ya Ufini kwenye mji wa Sankt Petersburg. Sehemu ya kusini iko kwenye mpaka wa Poland na Ujerumani na sehemu ya magharibi kwa mji wa Flensburg karibu na mpaka wa Ujerumani na Denmark.

Njia ya kuunganisha Baltiki na Bahari ya Kaskazini ni milangobahari ya Kattegat na Skagerak. Mwanzoni wa Kattegat njia inapita kwenye visiwa vya Denmark na kuigawa katika njia tatu ndogo zinazoitwa Oresund, Belt Kubwa (Kidenmark: Storebælt) na Belt Ndogo (Kidenmark: Lillebælt).

Enzi ya Barafu

Kijiografia Baltiki ni mabaki ya Enzi ya Barafu iliyopita. Takriban miaka 12,000 iliyopita Ulaya yote ya Kaskazini ilifunikwa na ganda la barafu lenye unene wa mita mia kadhaa. Wakati wa kupungua kwa baridi barafu ilianza kuyeyuka na kusababisha kutokea kwa ziwa kubwa sana ambalo ni mwanzo wa Baltiki. Ziwa hili lilipata njia ya kujiunga na bahari na kiasi cha maji ya chumvi yaliingia ndani. Hivyo maji ya Baltiki ni mchanganyiko wa maji ya chumvi na maji matamu. Kiasi cha chumvi ndani ya maji yake ni kidogo kulingana na maji ya bahari ya kawaida.

Bahari yenye chumvi kidogo

Kiasi cha chumvi ni kikubwa zaidi kwenye kina kuliko kwenye maji ya juu. Wakati maji yenye chumvi kidogo inatoka kwenye Kattegat kuelekea Bahari ya Kaskazini kuna pia mwendo wa maji ya chumvi chini yake ya kuingia katika Baltiki. Maji ya chumvi ni mazito kuliko maji matamu, hivyo yanakaa kwenye vilindi vya bahari na kuwa na mwendo wa kuingia ilhali wakati huohuo maji ambayo ni matamu zaidi yanapita juu yake kutoka Baltiki.

Mito ya Baltiki

Mito mikubwa inaingia katika Baltiki na kusababisha mwendo wa maji ya kutoka katika Kattegat na kuingia Atlantiki. Baadhi ya mito hiyo ni: Oder, Vistula, Neman, Daugava na Neva.

Visiwa na mafunguvisiwa

Miji

Miji mikubwa kando ya Baltiki ni:

Bahari Ya Baltiki  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bahari ya Baltiki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Bahari Ya Baltiki Mipaka yakeBahari Ya Baltiki Enzi ya BarafuBahari Ya Baltiki Bahari yenye chumvi kidogoBahari Ya Baltiki Mito ya BaltikiBahari Ya Baltiki Visiwa na mafunguvisiwaBahari Ya Baltiki MijiBahari Ya BaltikiAtlantikiBahari ya KaskaziniBahari ya kandoDenmarkMlangobahariUlaya ya KaskaziniUswidi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Mobutu Sese SekoDuniaWizara za Serikali ya TanzaniaUtendi wa Fumo LiyongoBidiiNguruwe-kayaTaswira katika fasihiHaitiRohoKanga (ndege)Chumba cha Mtoano (2010)Usafi wa mazingiraMahakama ya TanzaniaSimu za mikononiShangaziMasafa ya mawimbiBawasiriNimoniaAunt EzekielWaheheKisononoUnyagoJohn MagufuliPemba (kisiwa)Utoaji mimbaUaJichoWanyama wa nyumbaniFasihi simuliziSakramentiInjili ya MarkoUkooWagogoMkoa wa Dar es SalaamBenderaHifadhi ya SerengetiMwenge wa UhuruShairiUjerumaniTafsiriMartha MwaipajaNembo ya TanzaniaIsraelBunge la TanzaniaSayansiMkoa wa RukwaVielezi vya mahaliFamiliaMbossoRose MhandoUlayaWahayaArusha (mji)MchwaUtumbo mpanaUandishi wa barua ya simuC++MahindiMaghaniUislamuHistoria ya uandishi wa QuraniBendera ya KenyaSteven KanumbaNikki wa PiliWasukumaOrodha ya Marais wa KenyaMlongeMaambukizi ya njia za mkojoVirusi vya CoronaHistoria ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoKihusishiGoba (Ubungo)VitendawiliWilayaWilaya ya Arusha🡆 More