Slovenia ni nchi ya Ulaya ya Kati, mashariki kwa milima ya Alpi.
Slovenia |
---|
Imepakana na Italia, ghuba ya Adria ya bahari ya Mediteranea, Kroatia, Hungaria na Austria.
Mji mkuu pia mji mkubwa ni Lyublyana (kwa Kislovenia: Ljubljana).
Ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa na wa Umoja wa Ulaya.
Watu wengi (83%) ni wa kabila la Waslovenia, wenye lugha ya Kislovenia ambayo ni kati ya lugha za Kislavoni.
Waslavi walihamia Slovenia ya leo katika karne ya 6 BK.
Tangu zamani waliishi chini ya utawala wa madola mbalimbali kama vile Dola la Roma, Austria na Yugoslavia hadi kupata uhuru wa kisiasa mara ya kwanza kabisa mwaka 1991 baada ya mwisho wa Shirikisho la Yugoslavia.
Kati ya nchi zote zilizotokana na Yugoslavia ya zamani Slovenia ni nchi yenye uchumi imara zaidi.
Upande wa dini, 57.8% ni Wakatoliki. 10% wanajitambulisha kama Wakanamungu.
Nchi za Umoja wa Ulaya | |
---|---|
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Slovenia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Slovenia, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.