Bulgaria

Bulgaria (kwa Kibulgaria: България; jina rasmi ni Jamhuri ya Bulgaria) ni nchi ya Ulaya kusini - magharibi kwenye rasi ya Balkani.

Bulgaria

Imepakana na Bahari Nyeusi, Serbia, Makedonia Kaskazini na Ugiriki.

Ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Historia

Zamadamu walikuweko walau miaka milioni 1.4 iliyopita.

Kufikia mwaka 5000 hivi KK kulikuwa na ustaarabu mkubwa uliotengeneza vyombo vya ufinyanzi na usonara vilivyo kati ya vile vya awali zaidi duniani.

Baada ya mwaka 3000 KK, Wathraki walijitokeza katika rasi ya Balkani.

Mwishoni mwa karne ya 6 KK sehemu kubwa ya eneo hilo lilitekwa na Dola la Persia.

Katika miaka ya 470 KK, Wathraki waliunda ufalme wa Odrusia, ambao baadaye ulianguka na wenyewe walitawaliwa na Wamakedonia, Wakelti na Warumi. Mchanganyiko huo wa watu ulikuja kuungana na Waslavi, waliolowea rasi kwa namna ya kudumu baada ya mwaka 500 BK.

Mwaka 632 Wabulgaria walianzisha nchi huru kaskazini kwa Bahari Nyeusi iliyoitwa Bulgaria Kuu chini ya Kubrat hadi nusu ya pili ya karne ya 7.

Asparukh, mwandamizi wake, alihamia karibu na delta ya mto Danube akazidi kuteka maeneo ya Balkani yaliyokuwa ya Dola la Bisanti, jambo lililoendelea katika karne zilizofuata.

Huo mchanganyiko mkubwa wa watu ulipata utambulisho wa kitaifa kwa kushika dini, lugha na alfabeti moja.

Katika karne ya 11 hilo dola la Bulgaria la kwanza lilishindwa na Dola la Roma Mashariki likisaidiwa na Warusi.

Lakini mwaka 1185 ndugu Asen na Peter walifaulu kuanzisha dola la pili la Bulgaria lililofikia kilele chake katika miaka ya 1230.

Baada ya kugawanyika, falme tatu za Kibulgaria zilitekwa na Dola la Osmani mwaka 1396 kwa miaka 500 iliyofuata.

Vita kati ya Urusi na Uturuki vya miaka 1877–1878 vilileta uhuru kwa sehemu ndogo ya Bulgaria. Kwa kutaka Wabulgaria wote wawe ndani yake, nchi iliunga mkono Ujerumani katika vita vikuu vyote viwili na hatimaye ilishindwa.

Hivyo Bulgaria ikawa chini ya Wakomunisti kwa miaka 45.

Baada ya hapo Bulgaria ilijiunga na NATO mwaka 2004 na Umoja wa Ulaya mwaka 2007.

Watu

Wakazi wanazidi kupungua tangu mwanzo wa miaka ya 1990.

Wengi wao (84.8%) wanazungumza Kibulgaria, ambacho ni kati ya lugha za Kislavoni, na wanafuata dini ya Ukristo katika Kanisa la kitaifa ambalo ni kati ya Makanisa ya Kiorthodoksi.

Pia kuna makundi makubwamakubwa ya Waturuki (8.8%) Waislamu na walowezi kutoka India (4.9%).

Kwa jumla, Wakristo ni 75%, Waislamu 10%, wenye dini nyingine ni 3%, wakati wasio na dini ni 11.8%.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya Nje


Nchi za Umoja wa Ulaya Bulgaria 
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Bulgaria  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bulgaria kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Bulgaria HistoriaBulgaria WatuBulgaria Tazama piaBulgaria TanbihiBulgaria MarejeoBulgaria Viungo vya NjeBulgariaBalkaniKibulgariaKusiniMagharibiRasiUlaya

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Insha ya kisanaaRejistaFacebookUnyanyasaji wa kijinsiaOrodha ya shule nchini TanzaniaWordPressHistoria ya IsraelKabilaMapambano kati ya Israeli na PalestinaHistoria ya WapareMaktabaNyati wa AfrikaUtohoziBarack ObamaJangwaAdhuhuriShangaziHistoria ya UislamuMkutano wa Berlin wa 1885KitaluUandishi wa barua ya simuInshaHistoria ya Kanisa KatolikiHistoria ya WokovuPhilip Isdor MpangoUtamaduniUzazi wa mpangoVielezi vya namnaMkoa wa RukwaMkoa wa TangaMbwana SamattaOrodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaUaSimuKamusi elezoMishipa ya damuKylian MbappéLatitudoVivumishi vya jina kwa jinaDoto Mashaka BitekoMlongeMeliAbakuriaVita ya Maji MajiMkuu wa wilayaTausiMadhehebuOrodha ya Marais wa MarekaniInsha za hojaP. FunkOrodha ya milima mirefu dunianiMahakamaUmoja wa UlayaManchester CitySimba S.C.Kata (maana)Ugonjwa wa uti wa mgongoMavaziUngujaMkoa wa MbeyaHifadhi ya Taifa ya NyerereNabii EliyaUyahudiOrodha ya visiwa vya TanzaniaAslay Isihaka NassoroMohammed Gulam DewjiJulius NyerereDamuMnyamaUbongoHistoria ya KiswahiliMuzikiMkoa wa RuvumaBahatiBonde la Ufa la Afrika ya MasharikiBundukiJohn Magufuli🡆 More