Belarus (kwa Kibelarus: Беларусь (Kikyrili) au Biełaruś (Kilatini); kwa Kirusi:Белоруссия ) ni nchi ya Ulaya ya Mashariki inayopakana na Urusi, Ukraine, Poland, Lithuania na Latvia.
Belarus |
---|
Mji mkuu ni Minsk na miji mingine ni pamoja na Brest, Grodno, Gomel, Mogilev na Vitebsk.
Idadi ya wakazi inapungua: ni watu 9,498,700 (2016).
Belarus haikuwahi kuwa nchi ya pekee hadi karne ya 20. Maeneo yake yalikuwa chini ya himaya mbalimbali kama vile Poland, Lithuania na Urusi. Belarus ilikuwa kitengo cha Umoja wa Kisovyet tangu 1919/1922 hadi 1991.
Wakazi walio wengi ni Wabelarus (83.7%) ambao wanaongea ama Kibelarus au Kirusi ambavyo vyote viwili ni lugha rasmi. Lugha hizi mbili zina asili moja. Takriban 11% za wakazi ni Warusi.
Kuna pia vikundi vidogo vinavyotumia lugha za pekee kama vile Kipoland, Kiukraine, Kilatvia, Kilituanya na nyingine.
Walio wengi ni wafuasi wa Ukristo katika Makanisa ya Kiorthodoksi (48.3%) na katika Kanisa Katoliki (7.1%).
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Belarus kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Belarus, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.