Mayote: Département ya Ufaransa

Mayote ni eneo la ng’ambo la Ufaransa (kwa Kifaransa: Départment de Mayotte).

Mayote
Départment de Mayotte (Kifaransa)
Flag of France Coat of Arms of Mayotte
(Bendera ya Mayote) (Nembo la Mayote)
Wimbo wa taifa: La Marseillaise
Mahali pa Mayotte
Lugha za Taifa Kiswahili (shimaore)
Kifaransa
Mji Mkuu Mamoudzou
Rais
Rais wa Ufaransa
Emmanuel Macron
Eneo
 - Jumla
 - 0.4% Maji
Kadiriwa 185 duniani
374 km²
Umma
 - Kadirio 2019 (270,372)
 - Sensa, julai 2002 (160,265)
 - Umma kugawa na Eneo (kilomita) 720
Kadiriwa 187 duniani
; (11 duni)
Chumo cha uchumi
 - Jumla
 - kwa kipimo cha umma
$466.8 billion (208 kadir)
$2,600 (165)
Uhuru
 - Kadirifu
 - Barabara
Eneo la Ufaransa
Kura ya maoni kubaki eneo la Ufaransa
Fedha Euro
Saa za Eneo UTC +3
Wimbo wa Taifa La Marseillaise
Intaneti TLD .yt
kodi za simu 269

Linaundwa na visiwa vya Maore na Pamanzi pamoja na vingine vidogo. Eneo hili kijiografia ni hasa muungo wa funguvisiwa la Komori lakini si kisiasa.

Mayote: Historia, Lugha na dini, Utalii
Ramani ya Komori na Mayote.

Mayote iko katika kaskazini ya Mfereji wa Msumbiji kwenye Bahari Hindi, kati ya Madagaska upande wa mashariki-kusini na Msumbiji bara upande wa magharibi. Iko kilometa 295 magharibi kwa Madagaska na km 67 kusini mashariki mwa Nzwani.

Ardhi ya Mayote ina eneo la takriban km² 374. Ni mwamba wa matumbawe.

Mji mkuu ni Mamoudzou tangu mwaka 1977. Mji mkuu wa zamani ni Dzaoudzi kwenye kisiwa cha Pamanzi.


Historia

Mayote: Historia, Lugha na dini, Utalii 
Andriantsoly, Sultani wa mwisho wa Mayote, 1832-1843.

Mayote inaonekana kuwa imekaliwa na watu kutoka karne ya 7, wakitokea Madagaska, wengine wenye asili ya Asia na wengine wenye asili ya Afrika.

Kati ya karne ya 8 na karne ya 11 wakazi walisilimu, na kuna msikiti mkongwe (katika Tsingoni) wa karne ya 14, pamoja na mirhab ya matumbawe (1532). Visiwa vyote vya Komori vinafuata utamaduni wa Kiswahili vikiwa pamoja na Mayote.

Mwaka wa 1841, wakati idadi ya watu ilipungua kwa wakazi chini ya 3000, sultani wa mwisho Andriansoly (kutoka Madagaska) aliuza kisiwa kwa Ufaransa kwa kubadilishana ya ulinzi wa nchi hiyo, hivyo Mayote ikawa koloni la Kifaransa.

Mwaka 1974, wakati visiwa vingine vitatu vya Komori walidai uhuru na kuunda Umoja wa Komori, Mayote iliomba kubaki na Ufaransa, na mwaka 2011 ilipewa hali ya eneo la ng'ambo la Ufaransa kwa kura ya maoni.

Lugha na dini

Kuna lugha tatu ambazo huzungumzwa kisiwani Mayote, yaani Kifaransa (lugha rasmi), Kimaore ya Komori (55.1%), na Kibushi ya Madagaska.

Upande wa dini, asilimia 97 ni Waislamu na 3% ni Wakristo.

Utalii

Kisiwa cha Mayote kina mchanga wa pwani ya rangi tofauti (nyeusi, kahawia, kijivu, nyekundu, beige, nyeupe). Rasi yake ni kubwa (km² 1500).

Usafiri

Mayote: Historia, Lugha na dini, Utalii 
Bahari karibu na Mamoudzou.

Tazama pia

Viungo vya nje


Nchi za Afrika Mayote: Historia, Lugha na dini, Utalii 
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira

Tags:

Mayote HistoriaMayote Lugha na diniMayote UtaliiMayote UsafiriMayote Tazama piaMayote Viungo vya njeMayoteEneo la ng’ambo la UfaransaFunguvisiwaJiografiaKifaransaKomoriMaore (kisiwa)PamanziSiasaVisiwa

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Orodha ya Marais wa KenyaJohn Raphael BoccoUbongoOrodha ya matajiri wakubwa WaafrikaLakabuReal MadridMwanaumeHistoria ya KanisaKamusi ya Kiswahili sanifuNdoaAmri KumiMkoa wa ManyaraMapambano kati ya Israeli na PalestinaZiwa ViktoriaMkanda wa jeshiKata (maana)KengeYoung Africans S.C.WajitaMafumbo (semi)Mamelodi Sundowns F.C.Vita Kuu ya Kwanza ya DuniaDesturiUturukiNgeliMaumivu ya kiunoKakakuonaMaudhuiKassim MajaliwaWilaya ya KaratuWagogoUgonjwa wa kuharaTetekuwangaWahaKumaMisriHistoria ya MsumbijiDolar ya MarekaniVirusi vya UKIMWILongitudoRoho MtakatifuSimuAzimio la ArushaMmeaMaambukizi ya njia za mkojoMwislamuMauaji ya kimbari ya RwandaMohammed Gulam DewjiKiingerezaKarafuuNdovuWahayaUingerezaJinsiaVietnamNathariIdi AminDodoma (mji)Mwanza (mji)Kidole cha kati cha kandoOrodha ya Watakatifu WakristoKwararaMaktabaBintiJoseph Sinde WariobaMagonjwa ya machoUtegemezi wa dawa za kulevyaKen WaliboraNdege (mnyama)UkristoRayvannyKipindupinduWatutsiMselaBonde la Ufa la Afrika ya Mashariki🡆 More