Libya

Libya ni nchi ya Afrika ya Kaskazini kwenye Bahari ya Mediteraneo, inayopakana na Misri, Sudan, Niger, Chad, Algeria na Tunisia.

ليبيا
(Lībiyya)
Libya
Libya
Bendera ya Libya
Libya
Nembo la Libya
Lugha rasmi Kiarabu
Mji Mkuu Tripoli
Serikali Jamhuri ya Kiislamu
Mkuu wa Dola Mohamed al-Menfi
Waziri Mkuu Abdul Hamid Dbeibeh
Eneo km² 1.759.541
Idadi ya Wakazi 7,054,493 (Julai 2022)
Wakazi kwa km² 3,74
JPT/mkazi 4.293 US-$ (2004)
Uhuru kutoka Italia tarehe 24 Desemba 1951
Pesa Dinari ya Libya
Wakati UTC+1
Wimbo la Taifa "Libya, Libya, Libya"
Libya
Mahali pa Libya katika Afrika
Libya
Ramani ya Libya
Libya
Ziwa la Um el Maa huko Libya

Eneo kubwa la nchi (90%) ni sehemu ya jangwa la Sahara. Chini yake kuna akiba kubwa ya petroli, ambayo ndiyo utajiri wa nchi.

Miji mikuu ni Tripoli, Benghazi na Misratah.

Historia

Wakazi asili walikuwa Waberber. Baadaye wakaja Wafoinike upande wa magharibi na Wagiriki upande wa mashariki.

Hatimaye Libya ikamezwa na Dola la Roma, na Ukristo ukaenea.

Baada ya dola hilo kuanguka, Wavandali waliteka sehemu kubwa ya nchi.

Katika karne ya 7 Waarabu waliingiza Uislamu na utamaduni wao.

Mwaka 1551 Waturuki walifukuza Wazungu kutoka Tripoli wakatawala hadi karne ya 20.

Nchi ilitawaliwa na Waitalia tangu mwaka 1911 hadi 1941 ilipotekwa na Waingereza ambao, baada ya Vita vikuu vya pili kwisha, waliacha nchi mwaka 1951 mikononi mwa mfalme mwenyeji, Idris I, aliyekuwa amepinga ukoloni tangu mwaka 1920 (Vita vya Libya dhidi ya Italia).

Kisha kumpindua mfalme huyo, Muammar al-Gaddafi alitawala kidikteta tangu mwaka 1969 hadi alipopinduliwa na kuuawa mwaka 2011 kwa mkono wa N.A.T.O.

Baada ya hapo wananchi wanazidi kupigana katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Mwaka 2020 kulikuwa na makubaliano ya kusimamisha vita na kuunda serikali ya pamoja ili kuandaa uchaguzi mkuu.

Watu

Wakazi wa Libya ni hasa mchanganyiko wa Waberberi, Waarabu na Waturuki (74%), mbali na Waberberi (25%) ambao ndio wakazi asilia, lakini wengi wao wameanza kutumia lugha ya Kiarabu pia. Kuna pia wahamiaji kutoka nchi za jirani, za kandokando ya Bahari ya Kati na kutoka Bara Hindi.

Wakazi wameongezeka tangu mwaka 1970 kutoka milioni 2.5 hadi kuwa karibu milioni 7 mwaka 2022. Nusu ya wakazi wote ni vijana chini ya umri wa miaka 16. Sehemu kubwa kabisa (80%) huishi sehemu za pwani.

Lugha kuu ni Kiarabu pamoja na lugha kadhaa za Kiberberi. Ndizo:

  • Kinafusi (wasemaji 101.000)
  • Kighadames (wasemaji 42.000)
  • Kitamascheq (Tuareg; wasemaji 17.000)

Upande wa dini, unatawala Uislamu (97%). Wakristo ni zaidi ya 100,000, wakiwemo hasa Wakopti (60,000) na Wakatoliki (40,000).

Tazama pia

Viungo vya nje

Libya 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:


Nchi za Afrika Libya 
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Libya  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Libya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Libya HistoriaLibya WatuLibya Tazama piaLibya Viungo vya njeLibyaAfrikaAlgeriaBahariChadMediteraneoMisriNigerSudanTunisia

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

PichaHoma ya manjanoLebanoniIniLady Jay DeeIdara ya Usalama wa Taifa (Tanzania)Historia ya UrusiShetaniNgono zembeBahariNamba ya mnyamaWayahudiSayansiWimboOrodha ya kampuni za TanzaniaKumaOrodha ya makabila ya KenyaMbuni (maana)Bibi Titi MohammedAdhuhuriSteven KanumbaUwanja wa Taifa (Tanzania)Blandina ChangulaPemba (kisiwa)Muungano wa Madola ya AfrikaMwanzoMitume wa YesuDoto Mashaka BitekoUyahudiMkoa wa MwanzaKukiYohane MbatizajiJokate MwegeloUtoaji mimbaParadigma ya programuHistoria ya IranTaswira katika fasihiHoma ya iniAlomofuOrodha ya majimbo ya MarekaniSalaKibodiTasifidaVivumishi vya pekeeSaa za Afrika MasharikiRiwayaKatekisimu ya Kanisa KatolikiMsalaba wa YesuAmri KumiLigi Kuu Tanzania BaraWatu weusiMwanaumeSentensiTanganyikaMchungaji mwemaKamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniKataAfrika ya MasharikiYesuLionel MessiTungo kishaziFarasiKitabu cha DanieliAnwaniOrodha ya milima ya TanzaniaBawasiriMiikka MwambaKitabu cha YoshuaHoma ya matumboMkoa wa IringaBendera ya KenyaMalariaKonsonantiNevaNadhiriVielezi🡆 More