Burkina Faso

Burkina Faso ni nchi ya Afrika ya Magharibi isiyo na pwani kwenye bahari yoyote.

Burkina Faso
Burkĩna Faso (Kimoore)
𞤄𞤵𞤪𞤳𞤭𞤲𞤢 𞤊𞤢𞤧𞤮 (Kifulani)
ߓߎߙߞߌߣߊ ߝߊߛߏ (Kijula)
Nembo ya Burkina Faso
Nembo
Kaulimbiu ya taifa:
Unité–Progrès–Justice (Kifaransa)
"Umoja–Maendeleo–Haki"
Wimbo wa taifa: Ditanyè (Kifaransa)
"Wimbo wa ushindi"
Mahali pa Burkina Faso
Mahali pa Burkina Faso
Ramani ya Burkina Faso
Ramani ya Burkina Faso
Mji mkuu
na mkubwa nchini
Wagadugu
12°22′ N 1°32′ W
Lugha rasmiKimoore
Kibisa
Kijula
Kifulani
Idadi ya watu
 • Kadirio la 202322 489 126
Burkina Faso
Ramani ambayo inaonyesha mikono ya mto Volta nchini.

Imepakana na nchi zifuatazo: Mali upande wa kaskazini, Nijeri upande wa mashariki, Benin, Togo, Ghana na Kodivaa upande wa kusini.

Historia

Historia ya awali

Koloni la Wafaransa

Nchi ilianzishwa na Wafaransa kwa njia ya kugawa koloni la Cote d'Ivoire mwaka 1919. Jina la koloni jipya lilikuwa Volta ya Juu (kwa Kifaransa: Haute Volta). Jina limetokana na mto Volta unaoanzia hapa.

Kati ya miaka 1932 na 1947 eneo lake lilitawaliwa na makoloni ya jirani.

Baada ya uhuru

Tangu mwaka 1960 nchi ikawa huru.

Kiongozi wa nchi Thomas Sankara alibadilisha jina la nchi tarehe 4 Agosti 1984 kuwa Burkina Faso, yaani nchi ya watu waadilifu (kwa lugha ya Kimossi).

Jiografia

Eneo

Eneo la Burkina Faso liko kwa kimo cha wastani ya mita 400 juu ya UB. Hakuna tofauti kubwa sana.

Mlima wa juu ni Ténakourou (katika kusini) wenye m. 749. Sehemu ya chini ni bonde la mto Pendjari mpakani kwa Benin.

Nchi iko kusini kwa pinde la mto Niger

Utawala

Tazama pia: Orodha ya Miji ya Burkina Faso

Nchi imegawiwa kwa mikoa 13 (inaitwa region). Ndani ya mikoa kuna wilaya 45 (provinces) na tarafa 301 (departement). Kila mkoa husimamiwa na mkuu anayeitwa gouverneur.

Mito na maziwa

Burkina Faso ina chanzo cha matawimto ya mto Volta ambayo ni Mouhoun (pia Volta Nyeusi), Nakambé (pia Volta Nyeupe) na Nazinon (pia Volta Nyekundu). Mouhoun ni mto pekee wenye maji mwaka mzima.

Sehemu za kaskazini na mashariki za nchi ambazo ni takriban robo ya eneo lake lote ni beseni yala mto Niger. Matawimto ya Niger (Béli, Gorouol, Goudébo na Dargol) yana maji kwa muda wa miezi 4-6 kila mwaka.

Kuna pia maziwa kadhaa, hasa Tingrela, Bam na Dem.

Hali ya hewa

Hali ya hewa ni ya kitropiki. Majira ya mvua ni kati ya Mei na Septemba.

Wakati wa kiangazi kuna upepo wa Harmattan unaotoka katika jangwa la Sahara.

Kuna kanda tatu ya hali ya hewa, kuanzia Sahel katika kaskazini hadi Sudan-Guinea katika kusini kwenye mvua zaidi.

Katika maeneo yabisi ya kaskazini serikali mbalimbali zimejitahidi kupanda miti, jumla ya milioni 23 katika miaka 1996-2000.

Watu

Burkina Faso 
Wakulima wa Burkina Faso

Wakazi wa nchi huitwa "Waburkina" kutokana na jina la Burkina.

Idadi kubwa sana ya wananchi hukaa mashambani. Lakini miji inakua haraka.

Mji mkuu, Wagadugu, umeshapita idadi ya wakazi milioni moja.

Miji mingine muhimu ni Bobo-Dioulasso (wakazi 366,383), Koudougou (wakazi 89,374), Ouahigouya (wakazi 62,325) na Banfora (wakazi 61,762). (takwimu za Januari 2006)

Kabila kubwa nchini ni la Wamossi (karibu nusu ya wananchi wote) wakikaa karibu na Wagadugu. La pili ni la Wabobo hasa katika eneo la Bobo-Dioulasso. Kanda la Sahel katika kaskazini wako Wafula.

Lugha ya Kifaransa ndiyo lugha rasmi. Lugha kuu za mawasiliano ni Kimossi na Kidiula. Kwa ujumla kuna lugha 68 nchini Burkina.

Upande wa dini, wakazi Waislamu ni 63.8%, Wakristo ni 26.3% (Wakatoliki 20.1% na Waprotestanti 6.2%) na wafuasi wa dini asilia za Kiafrika ni 9%.

Tazama pia

Marejeo

  • Engberg-Perderson, Lars, Endangering Development: Politics, Projects, and Environment in Burkina Faso (Praeger Publishers, 2003).
  • Englebert, Pierre, Burkina Faso: Unsteady Statehood in West Africa (Perseus, 1999).
  • Howorth, Chris, Rebuilding the Local Landscape: Environmental Management in Burkina Faso (Ashgate, 1999).
  • McFarland, Daniel Miles and Rupley, Lawrence A, Historical Dictionary of Burkina Faso (Scarecrow Press, 1998).
  • Manson, Katrina and Knight, James, Burkina Faso (Bradt Travel Guides, 2011).
  • Roy, Christopher D and Wheelock, Thomas G B, Land of the Flying Masks: Art and Culture in Burkina Faso: The Thomas G.B. Wheelock Collection (Prestel Publishing, 2007).
  • Sankara, Thomas, Thomas Sankara Speaks: The Burkina Faso Revolution 1983–1987 (Pathfinder Press, 2007).
  • Sankara, Thomas, We are the Heirs of the World's Revolutions: Speeches from the Burkina Faso Revolution 1983–1987 (Pathfinder Press, 2007).

Viungo vya nje

Burkina Faso 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
    Trade


Nchi za Afrika Burkina Faso 
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Burkina Faso  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Burkina Faso kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Burkina Faso HistoriaBurkina Faso JiografiaBurkina Faso WatuBurkina Faso Tazama piaBurkina Faso MarejeoBurkina Faso Viungo vya njeBurkina FasoAfrika ya MagharibiBahariPwani

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Dolar ya MarekaniUandishi wa barua ya simuGoogleJohn Raphael BoccoKipandausoKipepeoHekaluKifaduroDhahabuYouTubeGeorge WashingtonKiebraniaBarua rasmiMpira wa miguuNgeliKiboko (mnyama)Uzazi wa mpango kwa njia asiliaUingerezaJoyce Lazaro NdalichakoUandishi wa inshaAli KibaViwakilishiWimboZiwa ViktoriaUbatizoUmoja wa MataifaNg'ombeAsia ya Kusini-MasharikiHoma ya manjanoTanganyika African National UnionRonaldoShengWanyihaHistoria ya Kanisa KatolikiPichaAlfabetiMfumo katika sokaHistoria ya WapareIniNathariPijini na krioliUrusiNomino za jumlaMisemoTundaMaajabu ya dunia50 CentMohamed HusseinNyweleMaktabaMkoa wa TaboraMshubiriWanyama wa nyumbaniMtume PetroMarekaniTanzaniaBinamuNembo ya TanzaniaUandishi wa ripotiLigi ya Mabingwa AfrikaUzazi wa mpangoMwanzo (Biblia)MautiAntibiotikiMartha MwaipajaBarua pepeWayahudiOsama bin LadenAsili ya KiswahiliTupac ShakurMafua ya kawaidaSalamu MariaMboo🡆 More