Cabo Verde (Kiingereza: Cape Verde) ni nchi ya visiwa katika bahari ya Atlantiki mbele ya pwani ya Afrika ya Magharibi.
Jamhuri ya Cabo Verde | |
---|---|
República de Cabo Verde (Kireno) | |
Kaulimbiu ya taifa: Unidade, Trabalho, Progresso (Kireno) "Umoja, Kazi, Maendeleo" | |
Wimbo wa taifa: Cântico da Liberdade (Kireno) "Mkarara wa Uhuru" | |
Mahali pa Cabo Verde | |
Ramani ya Cabo Verde | |
Mji mkuu na mkubwa nchini | Praia |
Lugha rasmi | Kireno Kikaboverde |
Serikali | Jamhuri |
• Rais • Waziri Mkuu | José Maria Neves Ulisses Correia e Silva |
Eneo | |
• Eneo la jumla | km2 4 033 |
Idadi ya watu | |
• Kadirio la 2023 | 603 901 |
Pato la taifa | Kadirio la 2023 |
• Jumla | USD bilioni 2.598 |
• Kwa kila mtu | USD 4 503 |
Pato halisi la taifa | Kadirio la 2023 |
• Jumla | USD bilioni 5.717 |
• Kwa kila mtu | USD 9 909 |
Maendeleo (2021) | 0.662 - wastani |
Sarafu | Escudo ya Cabo Verde |
Eneo la visiwa vyake kwa jumla ni km² 4,033.
Funguvisiwa lake lina visiwa 15 katika vikundi viwili:
Mji mkuu ni Praia katika kisiwa cha Santiago.
Miji mikubwa zaidi ni (takwimu za mwaka 2010): Praia (wakazi 127,832), Mindelo (wakazi 70,468), Santa Maria (wakazi 23,839), Assomada (wakazi 12,026), Pedra Badejo (wakazi 9,345) na São Filipe (wakazi 8,125).
Hadi kufika kwa Wareno katika karne ya 15 visiwa vya Cabo Verde havikuwa na watu.
Wareno walianzisha mashamba ya miwa na kuleta watumwa kutoka bara la Afrika.
Cabo Verde ilikuwa pia kituo muhimu cha biashara ya watumwa kati ya Afrika na Amerika.
Wahamiaji kutoka Ulaya walikuwa pia Wahispania, Waitalia pamoja na Wayahudi na Waislamu waliokataliwa kukaa kwao Ureno.
Kutokana na historia hiyo, leo idadi kubwa ya wakazi ni machotara waliozaliwa na Waafrika (waliochangia 56% ya DNA) na Wazungu (waliochangia 44%).
Lugha rasmi ni Kireno, lakini wakazi wanazungumza zaidi aina mbalimbali za Krioli iliyotokana na lugha hiyo.
Upande wa dini, walau 89.1% ya wakazi ni Wakristo, hasa wa Kanisa Katoliki (78.7%), lakini pia wa madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti (10.4%).
Kutokana na hali ngumu ya uchumi, wananchi wanaoishi nje ya Cabo Verde ni mara mbili kuliko wale wanaoishi nchini. Kati ya waliohama baada ya uhuru (1975), 500,000 wanaishi Marekani na 150,000 Ureno. Hata hivyo kuna wahamiaji vilevile, hasa kutoka nchi za Afrika bara.
|date=
(help)
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Cabo Verde kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Cabo Verde, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.