Diego Garcia ni atolli ya Kiingereza katika Bahari Hindi, kati ya Tanzania na Indonesia.
Ni sehemu ya funguvisiwa la Chagos na leo kisiwa pekee chenye wakazi ambao ni wanajeshi wa Marekani. Ni kituo kikubwa cha kijeshi cha Marekani katika Bahari Hindi.
Kati ya miaka 1850 na 1965 kisiwa kilikuwa sehemu ya koloni la Morisi. Mwaka 1965 kilitengwa na Morisi pamoja na funguvisiwa lote. Mwaka 1971 Uingereza ilikodisha Diego Gracia kwa jeshi la Marekani ambao walitaka kuwa na kituo cha kijeshi kwenye Bahari Hindi katika mashindano yao na Umoja wa Kisovyeti.
Katika miaka miwili iliyofuata wenyeji wote wa funguvisiwa waliondolewa visiwani, wakahamishiwa na watoto wao huko Mauritius, Shelisheli na Uingereza. Wengi wao wanapigania haki ya kurudi. Mahakama ya Uingereza iliwaruhusu mwaka 2000 warudi tena lakini serikali imekataa mwaka 2004.
Diego Garcia ilikuwa kituo muhimu katika vita vya Marekani huko Afghanistan na Irak. Ndege za kijeshi za aina B-52 zinatoka hapa pamoja na ndege za kubeba petroli.
Marekani ina pia kituo cha manowari zake kisiwani.
British Indian Ocean Territory travel guide kutoka Wikisafiri
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Diego Garcia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Diego Garcia, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.