Michezo

Michezo ni amali au mazoezi ya kimwili ambayo mara nyingi yana ushindani ndani yake.

Yanatendeka kufuatana na kawaida na taratibu maalumu zilizokubaliwa kati ya wachezaji au katika jamii.

Michezo
Mashindano ya mbio ya masafa marefu sana, maarufu kama Marathon.

Michezo ni ya aina nyingi ikiwemo michezo ya juu angani, majini, kwenye nchi kavu na pia kwenye barafu. Watu hushiriki kwenye michezo kushindania zawadi, kama aina ya mazoezi au kujiburudisha tu.

  • Kuna michezo ambayo huhusisha mwili kama vile mbio ambazo huwa na vitengo tofautitofauti, miereka, dodi, kareti, judo, taekwondo, kuruka juu, kuruka urefu, kuogelea n.k.
  • Kuna michezo inayohusisha akili kama vile chesi, sarantanji, bao n.k.
  • Kuna michezo inayohusisha wanyama kama vile msabaka na mpira wa polo.
  • Kuna pia michezo inayotumia vifaa kama vile mipira, silaha, viatu na mbao telezi (zijuilikanazo kwa Kiingereza kama skating shoes/roller skates and skating boards) n.k.

Mifano maarufu ya michezo ni mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa mikono, mpira wa magongo, aina za mbio, mashindano ya kuogelea na kadhalika.

Watu wengi hupenda kutazama mashindano ya michezo. Tabia hii imekuwa msingi kwa wachezaji wanaotekeleza michezo yao si kwa kujiburudisha, bali kikazi na kwa malipo, pengine makubwa ajabu.

Tangu kale watu wamekutana kwa mashindano makubwa ya michezo kati ya jamii, makabila au mataifa. Kati ya mashindano mashuhuri hasa ni Michezo ya Olimpiki iliyofanyika awali Ugiriki wa Kale na sasa inafanyika kwa ushiriki wa mataifa yote duniani kila baada ya miaka minne.

Kwa nchi ya Tanzania michezo inayopendwa sana ni: mpira wa miguu, riadha, mpira wa pete, mpira wa wavu; pia kuna hamasa kubwa kwa watu kusoma magazeti kuhusu michezo ili kupata dondoo na habari muhimu kuhusu michezo mbalimbali inayoendelea huko viwanjani.

Tanbihi

Tazama pia

Kwa Kiswahili

Kwa Kiingereza

Viungo vya nje

Michezo  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Michezo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Michezo TanbihiMichezo Tazama piaMichezo Viungo vya njeMichezoJamiiMwiliZoezi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Vivumishi vya sifaShuleBongo FlavaDagaaAlasiriNetiboliViwakilishi vya idadiKanisa KatolikiHistoria ya KanisaUtumbo mwembambaMrijaMtoto wa jichoUzazi wa mpango kwa njia asiliaAkili ya binadamuVivumishi vya pekeeSumbawanga (mji)KomaKidole cha kati cha kandoShairiUgonjwa wa kuharaWanyamaporiMfumo wa nevaWanyamweziBarua rasmiMkoa wa SongweMamba (mnyama)Java (lugha ya programu)MahakamaLigi Kuu Uingereza (EPL)MaigizoMkoa wa LindiNamba tasaHifadhi ya SerengetiUharibifu wa mazingiraSaidi NtibazonkizaSayariHistoria ya EthiopiaMfumo katika sokaKadi za mialikoUkristo barani AfrikaMtandao wa kompyutaKiimboUchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2020TenziKitenzi kikuuMaskiniMachweoVivumishi vya urejeshiMaana ya maishaOrodha ya mito nchini TanzaniaKajala MasanjaMaji kujaa na kupwaAfrika ya MasharikiUlumbiMungu ibariki AfrikaMeja JeneraliMkoa wa SingidaVoliboliZabibuWairaqwKiunzi cha mifupaUkwapi na utaoMamaAli Hassan MwinyiAustraliaDaktariIdi AminAnwaniJohn MagufuliNadhariaBabeli🡆 More