Melilla

Melilla (tamka: me-li-ya; kwa Kiarabu: مليلية, Meliliya; jina rasmi: Ciudad Autónoma de Melilla = Mji wa kujitawala wa Melilla) ni mji wa Hispania kwenye pwani ya Mediteranea unaozungukwa na eneo la Moroko upande wa bara.

Umbali na Hispania bara ni takriban km 170 kuvuka bahari. Mji ulio karibu upande wa Moroko ni Nador kwenye umbali wa km 15.

Melilla
Kisiwa cha Melilla
Melilla
Ramani ya mji wa Melilla

Pamoja na mji wa Ceuta kisiasa ni sehemu ya Hispania na Umoja wa Ulaya, kijiografia ni sehemu ya Afrika. Moroko inadai ni sehemu ya eneo lake la kitaifa.

Watu

Melilla ina wakazi 65,500 (mwaka 2005) katika eneo la km² 20. Zamani wakazi walio wengi walikuwa Wakatoliki wenye asili ya Hispania pamoja na Wayahudi na Waislamu Waarabu au Waberber wenye asili ya Moroko. Miaka ya nyuma idadi ya Waislamu imeongezeka ambao wengi wao wanapendelea kujiita Waberber kuliko Waarabu; Wayahudi wamepungua sana. Inasemekana ya kwamba wakazi karibu wote wanajiangalia kuwa Wahispania bila kujali kama ni Wakatoliki au Waislamu.

Uchumi unategemea uvuvi pamoja na biashara ya mpakani. Pesa rasmi ni Euro.

Historia

Historia yake ilianza zaidi ya miaka 2000 iliyopita ikaundwa kwa jina la Rusadir. Ikawa sehemu ya Dola la Roma katika jimbo la Mauretania Tingitana. Eneo lake lilipiganiwa kuanzia mwaka 429 BK kati ya wavamizi Wavandali na Bizanti.

Karibu kabla ya mwaka 700 BK Waarabu Waislamu walivamia eneo la pwani ya Moroko wakielekea Hispania. Mji ulipata jina la Meliliya ukabaki chini ya utawala wa Kiislamu hadi mwaka 1497 ulipotekwa na Wahispania.

Wahispania walifaulu kubaki na mji katika vita mbalimbali za karne zilizofuata. Mwaka 1936 vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Hispania vilianza Melilla kwa uasi wa wanajeshi dhidi ya serikali ya Jamhuri ya Hispania.

Melilla  Makala hii kuhusu maeneo ya Hispania bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Melilla kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Nchi za Afrika Melilla 
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira

Tags:

BahariHispaniaKiarabuKmMediteraneaMjiMorokoNadorPwani

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

TarafaMivighaAlama ya uakifishajiUshairiMange KimambiAmina ChifupaMkoa wa MwanzaUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaShambaMzabibuUkooMnara wa BabeliJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaTulia AcksonMchwaMadiniWajitaKidole cha kati cha kandoYesuMavaziHistoria ya TanzaniaLionel MessiWilaya ya KinondoniMfumo wa mzunguko wa damuUkwapi na utaoVitenzi vishirikishi vikamilifuAbrahamuUhifadhi wa fasihi simuliziMwenge wa UhuruHifadhi ya mazingiraWabunge wa Tanzania 2020Maji kujaa na kupwaVipera vya semiOrodha ya Maspika wa Bunge la TanzaniaHuduma ya kwanzaKoloniUandishi wa barua ya simuShikamooDawatiMashuke (kundinyota)Mkutano wa Berlin wa 1885MariooUzalendoTashihisiOrodha ya Magavana wa TanganyikaWilaya ya TemekeMwanaumeMkoa wa Unguja Mjini MagharibiMshubiriMkoa wa SimiyuUpendoMbadili jinsiaUkoloniNomino za kawaidaKishazi huruShangaziNyangumiAgano la KaleMlima wa MezaDiamond PlatnumzUharibifu wa mazingiraMimba kuharibikaChristopher MtikilaKifaruMapinduzi ya ZanzibarUturukiUtalii nchini KenyaTupac ShakurNafsiMbagalaRoho MtakatifuTambikoUtamaduni🡆 More