Emirates ni ndege kuu katika bara la Arabu, iliyo chini ya kampuni ya The Emirates Group.
Ni ndege ya kitaifa iliyo mjini Dubai, miliki za kiarabuUnited Arab Emirates na inahudumu takriban wasafiri 2200 kila wiki kutoka kwa kituo chake cha Uwanja wa ndege wa kimataifa ya Dubai, Terminal 3 hadi nchi 55 na kwenye bara sita. Emirates iko chini ya The Emirates Group, ambayo ina waajiriwa zaidi ya 40,000, na inayomilikiwa na serikali ya Dubai.
Ndege hii iko kwenye ndege kumi bora kulingana na mauzo, wasafiri na kilomita.
Ndege ya kwanza ya Emirates ilisafiri kutoka mji wa Dubai hadi Karachi mnamo 25 Oktoba 1985.
Emirates ilianza kupata faida kuanzia baada ya miezi tisa. Mwaka wake wa kwanza, ilibeba wasafiri 260,000 na mizigi ya tani 10,000. Mnamo 1986, ndege hii iliongeza miji ya kusafiria kama Colombo, Dhaka, Amman, na Cairo miongoni mwa miji inayosafiria. Emirates ilianzisha ndege za kusafiri hadi London Gatwick kila siku mnamo 6 Julai 1987 kwa kutumia ndege mbili za Airbus A310. Pia, ilianzisha ndege za kuelekea mjini Singapore. Mnamo 1987, Ilianza kwenda Frankfurt kwa kupitia miji ya Istanbul, na Male.
Mauzo ya Emirates ziliongezeka kwa takriban milioni $100 kila mwaka, na kufikia milioni $500 mnamo 1993. Mwaka huu, ilibeba mizigo ya tani 68,000 na wasafiri milioni 1.6
Emirates ilipata mauzo ya milioni $643.4 katika mwaka wa 1994. Ilikuwa na wafanyikazi 4,000.
Terminal 3 kwenye Uwanja wa ndege ya Dubai ilijengewa kwa matumizi ya Emirates pekee. Iligharimu bilioni $4.5 na ilifunguliwa rasmi mnamo 14 Oktoba 2008. Terminal hii inaweza kutosheleza masafiri milioni 27.
Emirates imeajiri jumla ya watu 28,037 hadi mwaka wa 31 Machi 2009.
Year Ended | Passengers Flown | Cargo carried (thousand) | Turnover (AEDm) | Expenditure (AEDm) | Net Profit/Loss (AEDm) |
---|---|---|---|---|---|
31 Machi 1997 | 3,114.3 | 159.4 | 1,198.7 | 1,097.1 | 101.623 |
31 Machi 1998 | 3,683.4 | 200.1 | 4,089.1 | 3,826.7 | 262.413 |
31 Machi 1999 | 4,252.7 | 214.2 | 4,442.9 | 4,130.2 | 312.959 |
31 Machi 2000 | 4,775.4 | 269.9 | 5,113.8 | 4,812.9 | 300.900 |
31 Machi 2001 | 5,718.8 | 335.2 | 6,417.3 | 5,970.7 | 421.825 |
31 Machi 2002 | 6,765.1 | 400.6 | 7,274.6 | 6,783.7 | 468.231 |
31 Machi 2003 | 8,502.8 | 525.2 | 9,709.7 | 8,749.6 | 906.747 |
31 Machi 2004 | 10,441.3 | 659.8 | 13,286.3 | 11,602.1 | 1,573.511 |
31 Machi 2005 | 12,528.7 | 838.4 | 18,130.9 | 15,628.3 | 2,407.385 |
31 Machi 2006 | 14,497.5 | 1 ,018.5 | 23,050.9 | 20,489.6 | 2,474.97 |
31 Machi 2007 | 17,544.1 | 1,155.9 | 29,839.6 | 26,675.9 | 3,096.4 |
31 Machi 2008 | 21,229.2 | 1,282.1 | 40,196.6 | 35,121.7 | 5,020.4 |
31 Machi 2009 | 22,730.9 | 1,408.3 | 44,188.9 | 43,143.4 | 981.7 |
Kuanzia 2004, nembo ya Emirates ni Fly Emirates. Keep Discovering. Zingine zilizowahi kutumika ni kama:
Emirates inahudumu ndege 1,883 kila wiki, katika miji 103 kwenye nchi 65 kwenye bara 6 kutoka kwa kituo chake mjini Dubai.
Ndege hii ina vyumba vya mapumziko kwenye uwanja wa ndege katika miji ifuatayo:
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Emirates, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.