Karachi

Karachi (Kiurdu: كراچى) ni mji mkubwa wa Pakistan na mji mkuu wa jimbo la Sindh.

Hadi 1959 ilikuwa mji mkuu wa kitaifa. Mji ni kitovu cha kibiashara cha Pakistan.

Karachi كراچىا
Karachi
Kaburi la Baba wa Taifa Mohammed Ali Jinnah (1876-1948) mjini Karachi (Pakistan)
Habari za kimsingi
Jimbo Sindh
Anwani ya kijiografia Latitudo: 24°51'3"N - Longitudo: 67°1'5"E
Kimo 22 m juu ya UB
Eneo 591 km² (mji pekee)
3,527 km² (wilaya ya Karachi)
Wakazi 11,969,284 (2006)
Msongamano wa watu watu 3,394 kwa km²
watu 18,000/km² mjini pekee
Simu +92 (nchi), 21 (mji)
Mahali
Karachi

Karachi iko kando la delta ya mto Indus mwambaoni wa Bahari Arabu. Kuna mabandari mawili na viwanda vingi.

Mohammed Ali Jinnah anayekumbukwa kama baba wa taifa la Pakistan alizaliwa pia kuzikwa mjini.

Historia

Eneo la Karachi lilikaliwa na watu tangu muda mrefu na miji mbalimbali ya kihistoria imeaminiwa kuwepo katika eneo lake tangu zamani za Aleksander Mashuhuri aliyepita hapa. Katika karne ya 17 palikuwa na kijiji cha wavuwi kilichoitwa "Kolachi". Kikakua kuwa bandari ya biashara na Bara Arabu. Baada ya kuungwa kwa Sindh katika Uhindi wa Kiingereza mnamo 1843 Waingereza waliona nafasi nzuri ya bandari hiyo wakaanza kupanga na kukuza mji. 1864 mawasiliano ya simu ilianzishwa kati ya Karachi na London. 1878 mji ukaunganishwa na reli za Uhindi. Mwisho wa karne ya 19 idadi ya wakazi ilipita lakhi moja.

Wakati wa utengano wa Uhindi wa Kiingereza nusu ya wakazi walikuwa Wahindu waliopaswa kukimbia Uhindi. Wakimbizi Waislamu kutoka Uhindi walichukua nafasi yao wako sasa takriban nusu ya wakazi wote wa mji.

Baada ya Uhuru wa Pakistan Karachi ilikuwa mji mkuu hadi 1959.


Viungo vya Nje

Tags:

KiurduMji mkuuPakistan

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Jakaya KikweteMkoa wa MorogoroRaiaVieleziMkoa wa LindiNenoNguzo tano za UislamuUaminifuNeemaKatekisimu ya Kanisa KatolikiMnyamaLenziMasadukayoWilaya ya UbungoKatibaArusha (mji)MafarisayoJamhuri ya Kidemokrasia ya KongoWimbo wa Jumuiya ya Afrika MasharikiVita Kuu ya Kwanza ya DuniaWilayaMkoa wa SimiyuMisriNduniUgaidiHeshimaKiunzi cha mifupaNamba tasaMahakama ya TanzaniaTabiaNahauBonde la Ufa la Afrika ya MasharikiLigi Kuu Uingereza (EPL)LafudhiFananiOrodha ya Marais wa MarekaniKaaFalsafaTanganyikaMapenzi ya jinsia mojaGhuba ya UajemiVielezi vya idadiVitenzi vishiriki vipungufuUmoja wa AfrikaMkoa wa RukwaMkoa wa SongweOrodha ya Watakatifu wa AfrikaAfrikaGoba (Ubungo)Mbezi (Ubungo)TabianchiKishazi tegemeziHistoria ya KanisaAlama ya uakifishajiOrodha ya milima mirefu dunianiFonolojiaPumuNafsiAina za udongoWabunge wa kuteuliwaChuo Kikuu cha PwaniKitomeoKamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniKongoshoShinikizo la juu la damuUandishi wa barua ya simuIdi AminManchester United F.C.WasukumaVita Kuu ya Pili ya DuniaMachweo🡆 More