Umoja Wa Afrika

Umoja wa Afrika (UA) (kwa Kiingereza: African Union (AU); Kifaransa: Union Africaine (UA); Kihispania: Unión Africana (UA) ; Kireno: União Africana (UA) ) ni muungano wa nchi 55 za Afrika ulioanzishwa mnamo Julai 2002.

Umoja Wa Afrika
Bendera ya Umoja wa Afrika
Umoja Wa Afrika
Ramani ya Umoja wa Afrika. Nchi zote za Afrika ni wanachama (baada ya Moroko kujiunga upya tarehe 30 Januari 2017).

Umoja huu unaendeleza kazi za Umoja wa Muungano wa Afrika (kwa Kiingereza: Organisation of African Union - OAU) uliokuwepo 1963 hadi 2002.

Nia ya umoja huu ni kujenga muundo na mfumo wa kisiasa, wa kiuchumi, na wa kijamii ili kufikia wakati ambapo bara la Afrika litakuwa na bunge moja, benki moja, jeshi moja, rais mmoja, sarafu moja, n.k.

Dhumuni kubwa la umoja huu ni kuunganisha nguvu za mataifa ya Afrika ili kuweza kutatua matatizo yanayokabili bara hili kama vile vita, njaa, Ukimwi, n.k.

Nchi wanachama

Umoja wa Afrika ina nchi wanachama 55, yaani nchi zote za bara la Afrika (baada ya kurudi kwa Moroko, iliyokuwa imejiondoa mwaka 1985 kwa sababu UA ilitambua Sahara ya Magharibi kuwa nchi huru wakati Moroko inadai ni eneo la majimbo yake ya kusini).

Mkutano wa kwanza wa Bunge la Umoja wa Afrika ulifanyika mwaka 2004 huko Afrika Kusini.

Mikutano mikuu ya UA

  1. Durban (Afrika Kusini): 9-11 Julai 2002.
  2. Maputo (Msumbiji): 10-11 Julai 2003.
  3. Sirte (Libya), mkutano wa dharura: Februari 2004.
  4. Addis Ababa (Ethiopia): 6-8 Julai 2004.
  5. Abuja (Nigeria): 24-31 Januari 2005.
  6. Sirte (Libya): 28 Jun. - 5 Julai 2005.
  7. Khartoum (Sudan): 16-24 Januari 2006.

Viongozi

Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya UA ni N. Dlamini-Zuma.

Spika wa Bunge la Umoja wa Afrika ni Roger Nkodo Dang.

Tanbihi

Viungo vya nje

Tags:

Umoja Wa Afrika Nchi wanachamaUmoja Wa Afrika Mikutano mikuu ya UAUmoja Wa Afrika ViongoziUmoja Wa Afrika TanbihiUmoja Wa Afrika Viungo vya njeUmoja Wa Afrika2002AfrikaKifaransaKihispaniaKiingerezaKireno

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

UmaskiniMhandisiFasihiBiashara ya watumwaBata MzingaWagogoMuundoUtumwaMaudhuiIdara ya Usalama wa Taifa (Tanzania)Uhifadhi wa fasihi simuliziJKT TanzaniaMatumizi ya lugha ya KiswahiliOrodha ya Magavana wa TanganyikaUingerezaTausiNgono zembeFasihi simuliziOrodha ya visiwa vya TanzaniaNomino za pekeeKukuChelsea F.C.Orodha ya makabila ya TanzaniaMaarifaTeknolojiaMsamahaHekalu la YerusalemuMweziGoba (Ubungo)Kassim MajaliwaMkoa wa SingidaMkoa wa LindiMkoa wa KigomaIpagalaKamusi ya Kiswahili sanifuShairiHistoria ya AfrikaAlomofuIyungaIsraelUNICEFMobutu Sese SekoOrodha ya viongoziKiboko (mnyama)Wizara za Serikali ya TanzaniaMeli za mizigoSamia Suluhu HassanUpinde wa mvuaNdoa katika UislamuKiswahiliMtandao wa kijamiiMkoa wa NjombeMazingiraFalsafaAina za ufahamuMbuSayansiKilimoMorogoro VijijiniVielezi vya idadiRamaniTafsiriTanzaniaMajiKiarabuKitomeoMaumivu ya kiunoMmeaMbooWazaramoHarmonizeKifua kikuuNileEthiopia🡆 More