Beirut

Beirut (pia: Beyrouth; kwa Kiarabu: بيروت) ni mji mkuu wa Lebanon, pia mji mkubwa na bandari kuu ya nchi hiyo.

Iko mwambaoni pa Bahari ya Kati.

Beirut
Kitovu cha Beirut kutoka hewani: Bandari, Ras Beirut, Uwanja wa ndege

Imekadiriwa kuwa idadi ya wakazi ni kati ya milioni moja na mbili.

Mahali pa mji ni kanda kati ya bahari na milima inayofuatana sambamba na mwendo wa pwani.

Kitovu cha kihistoria kiko kando ya rasi inayoitwa Ras Beirut penye kitovu cha mji wa kisasa kabla ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ya Lebanon kati ya miaka 1975 na 1990.

Beirut
Kanisa na msikiti kandokando mjini Beirut.

Kipindi kirefu cha vita hivyo vya ndani kilibadilisha uso wa mji katika mengi. Mji ulitenganishwa katika maeneo ya Wakristo na Waislamu hasa. Mitaa mipya ilianzishwa mbali na mstari wa mapigano, ujenzi ukaongezeka sana hasa upande wa kaskazini na kuelekea milimani.

Tangu amani ya mwaka 1990 mji ulijengwa upya. Lakini mashambulizi ya ndege za vita za Israel mnamo Julai 2006 yaliharibu tena sehemu za mji.

Beirut
Nyumba zilizofyatuliwa risasi wakati wa vita 1975-1990.

Kabla ya vita Beirut ilikuwa tangu muda mrefu kitovu cha kiuchumi na kielimu cha Mashariki ya Kati. Chuo Kikuu cha Kimarekani (American University of Beirut) pamoja na vyuo vikuu vya serikali na Kanisa Katoliki vimeendelea kufundisha hata wakati wa vita. Nafasi ya kinara cha kielimu imerudishwa kwa sababu ya uhuru kwa ajili ya magazeti na wachapishaji vitabu, lakini uongozi wa kiuchumi umehamia nchi za ghuba ya Uajemi kama vile Kuwait, Qatar na Falme za Kiarabu.

Beirut Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Beirut kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Bahari ya KatiBandariKiarabuLebanonMjiMji mkuuMwambao

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Uundaji wa manenoAmina ChifupaOrodha ya milima ya TanzaniaMaumivu ya kiunoManchester CityBiblia ya KikristoBiasharaUandishi wa inshaDubaiKhadija KopaKisononoShairiTaswira katika fasihiTabataKiambishi tamatiNamba tasaMwana FANyati wa AfrikaKidole cha kati cha kandoShahawaRicardo KakaMahakamaTulia AcksonBarua rasmiMilanoYesuMsamahaJokofuKunguruNdoaMichael JacksonHali ya hewaUmememajiMajina ya Yesu katika Agano JipyaOrodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaKifua kikuuUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaOrodha ya Magavana wa TanganyikaTashihisiMkwawaWameru (Tanzania)NdovuPunyetoUhuru wa TanganyikaHuduma ya kwanzaWahayaRejistaMapenzi ya jinsia mojaChristina ShushoMkoa wa TangaOrodha ya makabila ya TanzaniaLilithSomo la UchumiKamusiDemokrasiaAbrahamuUmoja wa MataifaCleopa David MsuyaUkutaKilimanjaro (volkeno)Ngono zembeMaambukizi ya njia za mkojoMkoa wa SimiyuOrodha ya viongoziTambikoUingerezaVivumishi vya sifaVivumishi vya kumilikiRupie ya Afrika ya Mashariki ya KijerumaniHadithi za Mtume MuhammadMiundombinuUpinde wa mvuaMkoa wa Unguja Mjini MagharibiUrusiAlfabetiKiarabu🡆 More