Bahari Ya Mediteranea

Bahari ya Mediteranea (pia: Bahari ya Kati) ni bahari ya pembeni ya Atlantiki kati ya mabara ya Afrika, Ulaya na Asia ya Magharibi.

Eneo lake ni takriban milioni 2,5 km². Kina chake kirefu ni 5,267 m. Ina kanda ya hali ya hewa ya pekee pamoja na mimea na wanyama.

Bahari Ya Mediteranea
Bahari ya Mediteranea jinsi inavyoonekana kutoka chombo cha angani
Bahari Ya Mediteranea
Ramani ya Bahari ya Mediteranea

Neno "Mediteranea" limetokana na lugha ya Kilatini likiunganisha maneno ya "medium" (inamaanisha "kati ya, katikati") na "terra" (inamaanisha "bara"). Kwa hiyo neno lenyewe linamaanisha "Bahari katikati ya bara".

Katika lugha ya Biblia Kiebrania iliitwa "Bahari ya Magharibi" au "Bahari Kuu"; Waroma wa Kale waliotwala nchi zote zinazopakana na Bahari ya Mediteranea waliita "mare nostrum" yaani "bahari yetu". Waarabu na Waturuki wanaiita "Bahari Nyeupe" (kwa Kituruki: Akdeniz; kwa Kiarabu: البحر الأبيض al-baHr-al-abyaD)

Jiografia

Bahari ya Mediteranea ni bahari, si ziwa, kwa sababu imeunganishwa na Atlantiki kwa njia ya mlango wa bahari wa Gibraltar.

Ina bahari za pembeni zake ambazo ni pamoja na Bahari Nyeusi, Bahari ya Aegean, Bahari ya Tyrrheni na mengine. Bahari Nyeusi inaunganishwa kwa njia ya mlangobahari wa Dardaneli, Bahari ya Marmara na mlangobahari wa Bosporus.

Tangu mwaka 1869 kuna pia njia ya maji kati ya Mediteranea na Bahari ya Shamu ambayo ni Mfereji wa Suez.

Kuna visiwa vingi sana hasa kati ya Ugiriki na Uturuki. Visiwa vikubwa ni Korsika, Sardinia, Sisilia, Kreta, Rhodos na Kibros.

Nchi zinazopakana

Leo hii kuna nchi au madola 22 zinazopakana na Bahari ya Mediteraneo:

Viungo vya nje

Bahari Ya Mediteranea 
WikiMedia Commons

Tags:

AfrikaAsiaAtlantikiBahari ya pembeniUlaya

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

UtajiriJumuiya ya Afrika MasharikiHoma ya matumboInjili ya MathayoMkundeMaliPumuMillard AyoMafumbo (semi)UkristoMisaKifua kikuuKilimanjaro (Volkeno)Kidole cha kati cha kandoSexRejistaKatiba ya KenyaBaraWashambaaKilimoMmenyuko wa mzioSteven KanumbaMontrealHistoria ya KanisaHadithiUpendoKifupiMsalaba wa YesuHaki za binadamuUtakatifuJohn MagufuliHarmonizeWestlifeSheriaVirusi vya UKIMWISikioKonsonantiOrodha ya watu maarufu wa TanzaniaMwanzo (Biblia)Afrika Mashariki 1800-1845MisemoHisiaBawasiriMeena AllyJakaya KikweteDChama cha Wafanyakazi TanzaniaNdovuMkwawaNadhariaTaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya TanzaniaNelson MandelaVivumishi vya idadiYosefu (mume wa Maria)Ridhiwani Jakaya KikweteUtohoziWapareHoma ya mafuaMajira ya baridiKizunguzunguUvukizajiFuvuKinyongaHekimaJiniHifadhi ya SerengetiIsraelMaria (Kipindi cha televisheni)Ikulu ya TanzaniaOrodha ya Maspika wa Bunge la TanzaniaNishatiBenjamin MkapaOrodha ya miji ya ZanzibarUnyenyekevu🡆 More