Nelson Mandela: Raisi wa kwanza wa Afrika Kusini na mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi (1918-2013)

Nelson Rolihlahla Mandela (18 Julai 1918 - 5 Desemba 2013) alikuwa mwanasiasa nchini Afrika Kusini, kiongozi wa mapambano dhidi ya siasa ya ubaguzi wa rangi (Apartheid), mfungwa jela kwa miaka 27 halafu rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia katika nchi yake.

Nelson Mandela
Nelson Mandela: Maisha, Harakati dhidi ya ubaguzi wa rangi, Marejeo

Rais wa Afrika Kusini (1994-1999)
Deputy Thabo Mbeki
F. W. de Klerk
mtangulizi F. W. de Klerk
aliyemfuata Thabo Mbeki

tarehe ya kuzaliwa 18 Julai 1918
Mvezo, Afrika Kusini
tarehe ya kufa 5 Desemba 2013
Johannesburg, Afrika Kusini
chama African National Congress
ndoa Evelyn Ntoko Mase (1944–1958)
Winnie Madikizela (1958–1996)
Graça Machel (1998–2013)
watoto 6 (Makgatho, Makaziwe, Zenani, Zindziswa)
mhitimu wa University of Fort Hare
University of London
University of South Africa
University of the Witwatersrand
Nelson Mandela: Maisha, Harakati dhidi ya ubaguzi wa rangi, Marejeo

Alikuwa mwanasheria na mwanachama, baadaye kiongozi wa chama cha ANC kilichopigania haki za binadamu wote nchini Afrika Kusini.

Maisha

Utoto na ukoo

Mandela alizaliwa tarehe 18 Julai 1918 katika familia ya kabila la Waxhosa kwenye kijiji cha Mvezo karibu na Umtata iliyokuwa kwenye Jimbo la Rasi.

Alipewa jina la Rolihlahla linalomaanisha "anayevuta tawi la mti" kwa maana ya "mwenye kuleta matata" katika lugha ya Kixhosa. Baadaye alijulikana kwa jina la ukoo wake "Madiba". Jina la Nelson alilipokea kutoka kwa mwalimu wake siku alipoanza kwenda shule.

Alitoka katika familia ya kifalme. Baba wa babu yake Ngubengcuka alikuwa mfalme wa Wathembu katika maeneo ya Transkei wa jimbo la kisasa la Rasi Mashariki la Afrika Kusini.

Baba yake Gadla Henry Mphakanyiswa alikuwa chifu na mshauri wa mfalme tangu mwaka 1915 hadi 1926. Mama yake Nelson, Nosekeni Fanny, alikuwa mke wa tatu.

Miaka ya kwanza aliishi kijijini alipojifunza mila na desturi za Waxhosa na kutunza mifugo pamoja na wavulana wengine.

Baba aliaga dunia Nelson alipokuwa na umri wa miaka tisa. Alibatizwa katika Kanisa la Kimethodisti akawa Mkristo wa kanisa hilo hadi kifo chake.

Baada ya kifo cha baba, mama alimpeleka kwa chifu mkuu wa Wathembu aliyemlea kama mtoto wake. Pamoja na wazazi wake wapya alihudhuria ibada za kanisani kila Jumapili zilizoimarisha imani yake ya Kikristo.

Akaendelea kusoma katika shule ya Kimethodisti aliposoma Kiingereza, Kixhosa, historia na jiografia. Katika ikulu ya chifu alisikia masimulizi mengi kuhusu historia ya Waafrika kutoka wageni waliokuja kumwaona baba wa kambo.

Elimu

Mwaka 1925 babake alimtuma kusoma shule ndogo ya Kimethodisti alipofanyikiwa vema. Baada ya kifo cha baba aliishi kwa chifu wa Watembo na hapo kwene umri wa miaka 16 alishiriki katika sherehe ya jando alipotahiriwa na kupokea jina Dalibunga.

Baadaye aliendelea kusoma kwenye shule ya sekondari ya „Clarkebury Boarding Institute“ huko Engcobo iliyokuwa shule ya bweni kubwa kwa ajili ya vijana kutoka Wathembo.

Nelson Mandela: Maisha, Harakati dhidi ya ubaguzi wa rangi, Marejeo 
Picha ya Mandela, akiwa Umtata mwaka 1937.

Hapa alianza mazoezi ya michezo na kupenda kazi ya bustani aliyoendelea kwa maisha yote. Baada ya miaka miwili alipokea cheti kidogo cha elimu ya sekondari.

Mwaka 1937 kwenye umri wa miaka 19 aliendelea kwenye chuo cha Wamethodisti huko [[Fort Beaufort. Hapo alikuwa mara ya kwanza rafiki na kijana nje ya kabila lake aliyekuwa Msotho akaathiriwa na mwalimu mpendwa Mxhosa aliyevunja mwiko kwa kumwoa mke kutoka kwa Wasotho Mandela alitumia muda mwingi huko Healdtown kwa kufuata michezo ya kukimbia na bondia.

Tangu 1939 alianza masomo kwa shahada ya kwanza kwenye Chuo Kikuu cha Fort Hare, chuo kwa ajili ya wanafunzi Waafrika katika jimbo la Rasi Mashariki. Masomo yake yalikuwa Kiingereza, anthropolojia, siasa na sheria. Wakati ule alitaka kuendelea kuwa mfasiri au afisa katika Idara ya Shughuli za Wazalendo (kitengo cha serikali ya Kizungu kwa maeneo ya Waafrika katika Afrika Kusini). Katika bweni lake alikuwa rafiki wa Kaiser Matanzima na Oliver Tambo aliyeendelea kuwa rafiki yake kwa miaka mingi ijayo. Pamoja na kupenda michezo Mandela alijifunza dansi ya Kizungu , alishiriki tamthiliya kuhusu about Abraham Lincoln, akatoa darasa la Biblia katika kanisa.

Harakati dhidi ya ubaguzi wa rangi

Mandela alihukumiwa kifungo cha maisha kwa miaka 27 kutokana na harakati zake za kuupinga ubaguzi wa rangi. Alifungwa katika kisiwa cha Robben.

Baada ya kuachiliwa huru mwaka 1990 alianzisha sera ya maridhiano au sera ya amani baina yake na watu weupe nchini Afrika Kusini, jambo ambalo watu wengi hawakulitegemea.

Mwaka wa 1993, pamoja na Frederik Willem de Klerk alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani ambayo ni tuzo ya nadra kutolewa duniani.

Baada ya kutengana na mke wake, Winnie Madikizela, alimuoa Graca Machel aliyewahi kuwa mke wa rais wa Msumbiji, Samora Machel.

Marejeo

Kujisomea

Nelson Mandela: Maisha, Harakati dhidi ya ubaguzi wa rangi, Marejeo  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nelson Mandela kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Nelson Mandela MaishaNelson Mandela Harakati dhidi ya ubaguzi wa rangiNelson Mandela MarejeoNelson Mandela18 Julai191820135 DesembaAfrika KusiniApartheidDemokrasiaJelaMwanasiasaRaisSiasaUbaguzi wa rangi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Bob MarleyLigi ya Mabingwa AfrikaWahayaHistoria ya TanzaniaHifadhi ya SerengetiLafudhiMfumo wa homoniOrodha ya maziwa ya TanzaniaZakayoMbuMbuga wa safariUrusiChristina ShushoMuzikiMsalaba wa YesuUislamuViganoWagogoJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaMaudhui katika kazi ya kifasihiUtataRiwayaChe GuevaraOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoNembo ya TanzaniaBikiraOrodha ya Watakatifu WakristoMichezo ya watotoApril JacksonMaambukizi ya njia za mkojoMazingiraWangoniMwarobainiItikadiNuktambiliMkoa wa MorogoroOrodha ya Marais wa TanzaniaKunguniRedioBomu la nyukliaUturukiPijiniUainishaji wa kisayansiNgeliMuungano wa Tanganyika na ZanzibarTafsidaMiundombinu ya kijani katika nchi ya Kenya, mji wa NairobiAzimio la Kimataifa juu ya Haki za BinadamuMapenziAzimio la ArushaMohammed Gulam DewjiMkoa wa RuvumaOrodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watuPasaka ya KiyahudiUchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2020Matumizi ya LughaSteve MweusiSintaksiKumaMichezoHerufi za KiarabuMaumivu ya kiunoAfyaWilaya za TanzaniaJokate MwegeloOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaWimboNgoma (muziki)UpendoKipindupinduOrodha ya vitabu vya BibliaMbwana SamattaRaiaMuundo🡆 More