Ahmedabad ni jiji kubwa katika jimbo la Gujarat kwenye magharibi ya Uhindi, pia ni makao makuu ya mkoa wa Ahmedabad.
Ilikuwa mji mkuu wa Gujarat tangu mwaka 1960 hadi 1970. Jiji liko kwenye ufuko wa mto Sabarmatin a kupakana na mji mkuu mpya Gandhinagar.
Nchi | Uhindi |
Jimbo / Mkoa | Gujarat |
Anwani ya kijiografia | 23.03,72.58 |
Kimo | mita 53 |
Eneo | 8,087 km2 |
Wakazi | 7,486,573 (2,014) |
Msongamano wa watu | 12,000/km2 |
Simu | 079 |
Eneo la jiji ni kama km28,087 na mkoa wote una wakazi 7,486,573 (2014), ilhali mji wenyewe una wakazi 6,357,693.
Ahmedabad ilianzishwa na sultani Ahmed Shah mnamo mwaka 1411 BK upande wa mashariki wa mto Sabarmati.
Mwaka 1487 mji ulizungushiwa ukuta wenye urefu wa km 10. Ukuta huu ulikuwa na mageti 12.
Mnamo mwaka 1573 Ahmedabad ilivamiwa na milki ya Mughali na kuwa sehemu yake.
Mwaka 1758 ilihamishwa kutoka Wamughali kwenda utawala wa Wamaratha. Chini ya utawala wao ilikuwa na tasnia ya vitambaa vilivyouzwa hadi Ulaya.
Mnamo mwaka 1818 mji ulifikishwa chini ya utawala wa Kampuni ya Kiingereza kwa Uhindi ya Mashariki. Tangu mnamo 1850 viwanda vya nguo vilianzishwa Ahmedabad na mji ulikuwa kitovu cha tasnia hiyo nchini. Hivyo ilitwa mara nyingi "Manchester of the East" kwa kulinganishwa na mji ule wa Uingereza wenye viwanda vingi vya nguo.
Katika karne ya 20 mji ulikuwa muhimu katika harakati ya kupigania uhuru wa Uhindi. Mahatma Ghandi aliunda vituo viwili vya harakati hiyo karibu na mji, na mwaka 1930 alianzisha hapa maandamano ya chumvi iliyokuwa hatua muhimu kukabili mamlaka ya ukoloni wa Kiingereza.
Wakati wa uhuru na ugawaji wa Uhindi Ahmedabad iliona mapigano makali baina ya Wahindu na Waislamu na wakimbizi wengi Wahindu kutoka Pakistan walihamia hapa.
Ahmedabad imeendelea kuwa mji wa viwanda. Pamoja na viwanda vya nguo kuna pia viwanda vya magari ya kampuni za Tata na Peugeot na madawa.
Ahmedabad ni sehemu ya mtandao wa reli ya Uhindi. Kituo cha Kalupur iko katikati ya jiji kinaunganishwa na mfumo wa metro na mabasi ya mwendokasi.
Mji unaunganishwa na mfumo wa barabara kuu za kijimbo na kitaifa.
Ahmedabad inahudumiwa na Uwanja wa Ndege wa Sardar Vallabbhai Patel ulioko kwa umbali wa kilomita 9 kutoka kitovu cha jiji ukihudumia pia mji mkuu wa Gandhinagar.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Ahmedabad, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.