Kiwanda

Kwa matumizi tofauti ya jina hili angalia Kiwanda (maana)

Kiwanda
Kiwanda cha Volkswagen huko Wolfsburg nchini Ujerumani.

Kiwanda ni mahali ambapo bidhaa mbalimbali hutengenezwa, yaani penye majengo na mashine. Bidhaa hizo zinaweza kuwa ndoo, sahani, mabakuli, vijiko, masufuria, magari, kompyuta, bati, vyakula mbalimbali, nyundo, pasi, baiskeli, pikipiki na vitu mbalimbali kwa ujumla. Hivyo kuna aina mbalimbali za viwanda: vipo viwanda vya vyakula, vya magari, vya vifaa vya ujenzi, vya vyombo mbalimbali, na vya vitu vizito, vya vyuma n.k.

Historia

Viwanda vilisambaa hasa kuanzia karne ya 19 wakati wa Mapinduzi ya viwandani ambako uzalishaji wa bidhaa ulihamishwa kutoka karakana za mafundi kwenda taasisi kubwa zaidi ambako mashine pamoja na mpangilio wa kazi viliongeza tija ya uzalishaji.

Ugunduzi wa injini ya mvuke uliunda msingi wa matumizi ya mashine katika shughuli nyingi za uzalishaji. Pamoja na hayo, mashine hizi zilikuwa na gharama kubwa, hivyo ulimbikizaji wa rasilmali uliunda tabaka mpya ya mabepari.

Kuenea kwa viwanda kulisababisha mabadiliko makubwa katika jamii za dunia. Mafundi wa weledi nyingi walipoteza nafasi zao kwa sababu bidhaa zilitengenezwa sasa kwa bei nafuu na katika muda mfupi, mara nyingi pia kwa ubora mkubwa kuliko jinsi mafundi walivyoweza kuzitoa kwa kazi ya mikono. Lakini viwanda vimeleta pia kazi mpya na ufundi tofauti na awali.

Uzalishaji wa bidhaa katika viwanda umekuwa msingi muhimu wa mchakato wa utandawazi ambako bidhaa nyingi zinazalishwa katika nchi fulani na kuuzwa kote duniani ilhali vipuli vya kutengenezea bidhaa hizi tena zinatoka katika nchi tofauti.

Zipo nchi zenye viwanda vingi zaidi; nchi yenye viwanda vingi ni nchi tajiri, kwa mfano Japani. Viwanda vyake ni vya kutengeneza bidhaa kubwa na nzito zaidi, kama vile meli, ndege, treni, magari n.k.

Faida na hasara

Kila nchi ina viwanda mbalimbali. Viwanda hivyo huisaidia nchi hiyo pindi iuzapo bidhaa hizo, pia huisaidia nchi husika kunufaika kiuchumi kwa uwepo wa viwanda hivyo.

Viwanda vina faida kubwa sana katika nchi yenye viwanda hivyo; faida hizo ni:

  • 1) Kuisaidia nchi kukua kiuchumi,
  • 2) kupata fedha za kigeni,
  • 3) kulipa madeni wanayodaiwa,
  • 4) kuajiri watu ambao hawana kazi,
  • 5) na kunufaisha taifa kwa ujumla n.k.

Tunapokuwa na viwanda tunanufaika kwa vitu vingi. Lakini viwanda vina madhara pia, tena mengi sana. Madhara hayo ni:

  • 1) moshi unaotoka viwandani huharibu anga hewa (ozon layer) ambapo anga linapotoboka husababisha kuwa na joto kali sana,
  • 2) majitaka yanayotiririshwa kwenye mito husababisha madhara kwa viumbehai wa majini na watu wanaotumia maji ya mto huo,
  • 3) uchafu unaobaki husababisha magonjwa mbalimbali ya milipuko,
  • 4) viwanda hutoa hewa chafu ambayo husababisha matatizo ya upumuaji kwa ujumla.

Kwa hiyo tuvitunze viwanda vyetu ili vilete faida, si kuangamiza watu na viumbe wengine.

Kiwanda  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiwanda kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Kiwanda (maana)

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

TanganyikaUpendoLiverpoolClatous ChamaMoyoMwamba (jiolojia)FutiMuhimbiliMadhara ya kuvuta sigaraKata za Mkoa wa MorogoroKishazi tegemeziBaraza la mawaziri TanzaniaNdovuMr. BlueWameru (Tanzania)Mapinduzi ya ZanzibarDemokrasiaLugha ya taifaSomo la UchumiOrodha ya wanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoNomino za kawaidaNdoaShambaSanaa za maoneshoKitenzi kikuuKinyongaUsawa (hisabati)TambikoRisalaRoho MtakatifuAgostino wa HippoPemba (kisiwa)RushwaTamthiliaNafsiSakramentiHaki za wanyamaUfugajiChristina ShushoSentensiOrodha ya Magavana wa TanganyikaBungeVivumishiVivumishi vya idadiKiongoziMahakama ya TanzaniaKimara (Ubungo)Cleopa David MsuyaKidole cha kati cha kandoInsha ya wasifuAlomofuTabataMkoa wa DodomaSinagogiBonde la Ufa la Afrika ya MasharikiMilanoViwakilishi vya urejeshiMwakaMkutano wa Berlin wa 1885Kiboko (mnyama)Joyce Lazaro NdalichakoNgano (hadithi)Mnyoo-matumbo MkubwaViwakilishi vya kumilikiMohammed Gulam DewjiKomaRiwayaMimba za utotoniCristiano RonaldoMuundo wa inshaMitume wa YesuKitenziUandishi🡆 More